-
Je, Utakwazika kwa Sababu ya Yesu?Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2021 | Mei
-
-
(3) YESU HAKUFUATA DESTURI NYINGI ZA KIYAHUDI
13. Ni jambo gani lililofanya watu wengi wamkatae Yesu?
13 Katika siku za Yesu, wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walishangaa kwa sababu wanafunzi wa Yesu hawakuwa wakifunga. Yesu alifafanua kwamba hawakuwa na sababu ya kufunga alipokuwa angali hai. (Mt. 9:14-17) Hata hivyo, Mafarisayo na wengine waliompinga Yesu walimshutumu kwa sababu hakufuata desturi zao. Walikasirika walipoona akiponya wagonjwa siku ya Sabato. (Marko 3:1-6; Yoh. 9:16) Kwa upande mmoja, walidai kwamba walishika Sabato; lakini kwa upande mwingine, walikuwa wakifanya biashara hekaluni. Viongozi hao walikasirika sana Yesu alipowashutumu kwa sababu hiyo. (Mt. 21:12, 13, 15) Na wale ambao Yesu aliwahubiria katika sinagogi huko Nazareti, walikasirika sana Yesu alipotumia mfano wa historia ya Waisraeli kuwaonyesha kwamba walikuwa na ubinafsi na hawakuwa na imani. (Luka 4:16, 25-30) Watu wengi walimkataa Yesu kwa sababu hakutenda kwa njia ambayo walitarajia.—Mt. 11:16-19.
14. Kwa nini Yesu alishutumu desturi za wanadamu ambazo hazikupatana na Maandiko?
14 Maandiko yanasema nini? Yehova alisema hivi kupitia nabii Isaya: “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao nao huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali sana nami; na hofu yao kunielekea inategemea amri za wanadamu ambazo wamefundishwa.” (Isa. 29:13) Yesu alikuwa sahihi kushutumu desturi za wanadamu ambazo hazikupatana na Maandiko. Wale walioona sheria na desturi za wanadamu kuwa muhimu kuliko Maandiko walimkataa Yehova na yule aliyemtuma akiwa Masihi.
-
-
Je, Utakwazika kwa Sababu ya Yesu?Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2021 | Mei
-
-
(4) YESU HAKUTATUA MATATIZO YA KISIASA KWA WAKATI HUO
17. Ni matarajio gani yaliyowafanya watu wengi wakwazike na kumkataa Yesu?
17 Baadhi ya watu katika siku za Yesu walitaka mabadiliko ya haraka ya kisiasa. Walitarajia kwamba Masihi angewaweka huru kutokana na utawala wenye kukandamiza wa Waroma. Lakini walipojaribu kumweka Yesu kuwa mfalme wao, alikataa. (Yoh. 6:14, 15) Wengine—kutia ndani makuhani—waliogopa kwamba Yesu angeleta mabadiliko ya kisiasa ambayo yangewakasirisha Waroma ambao walikuwa wamewapa viongozi hao wa kidini nguvu na mamlaka ya kadiri. Masuala hayo ya kisiasa yaliwafanya Wayahudi wengi wamkatae Yesu.
18. Watu wengi walipuuza unabii gani mbalimbali kumhusu Masihi?
18 Maandiko yanasema nini? Ingawa unabii mwingi ulitabiri kwamba mwishowe Masihi angekuja kuwa Shujaa mshindi, unabii mwingine ulionyesha kwamba ilikuwa lazima kwanza afe kwa ajili ya dhambi zetu. (Isa. 53:9, 12) Basi kwa nini walikuwa na matarajio yasiyo sahihi? Watu wengi katika siku za Yesu walipuuza unabii wowote ambao haukuahidi kutatua matatizo yao wakati huo.—Yoh. 6:26, 27.
-