-
Alikuwa Mshikamanifu Licha ya MajaribuIgeni Imani Yao
-
-
Alidumisha Ushikamanifu Aliporekebishwa
11. Yesu aliwaongoza wafuasi wake kwenda wapi? (Ona pia maelezo ya chini.)
11 Muda mfupi baadaye, Yesu aliongoza mitume na baadhi ya wanafunzi wake, katika safari ndefu kuelekea kaskazini. Nyakati nyingine, Mlima Hermoni wenye theluji, ulio upande wa kaskazini mwa Nchi ya Ahadi, ulionekana kutoka kwenye Bahari ya Galilaya. Kadiri walivyokaribia mlima huo ulizidi kuonekana wazi, huku wakipanda kuelekea vijiji fulani karibu na Kaisaria Filipi.b Wakiwa katika mandhari hii yenye kuvutia, ambapo waliona sehemu kubwa ya Nchi ya Ahadi upande wa kusini, Yesu aliwauliza wafuasi wake swali muhimu.
12, 13. (a) Kwa nini Yesu alitaka kujua maoni ya umati kumhusu? (b) Petro alionyeshaje imani ya kweli alipomjibu Yesu?
12 Akawauliza: “Umati unasema mimi ni nani?” Tunaweza kuwazia Petro akimtazama Yesu kwa makini, na kwa mara nyingine akitambua jinsi Bwana wake alivyokuwa mwenye fadhili na hekima. Yesu alitaka kujua maoni ya wasikilizaji wake kuhusu mambo waliyoona na kusikia. Wanafunzi wa Yesu walijibu swali hilo na kutaja maoni yaliyoenea yenye makosa kuhusu utambulisho wa Yesu. Lakini Yesu alitaka kujua mengi zaidi. Je, wafuasi wake wa karibu walikuwa na maoni kama hayo? Basi akawauliza, “Ingawa hivyo, ninyi mnasema mimi ni nani?”—Luka 9:18-20.
-
-
Alikuwa Mshikamanifu Licha ya MajaribuIgeni Imani Yao
-
-
b Safari hiyo ya kilomita 50, ilihusisha kuondoka kwenye fuo za Bahari ya Galilaya, zilizo mita 210 hivi chini ya usawa wa bahari na kupanda mpaka eneo lililo mita 350 hivi juu ya usawa wa bahari kupitia maeneo yenye kuvutia sana.
-