-
Sababu Iliyonifanya Niache Ukasisi kwa Ajili ya Huduma Bora ZaidiAmkeni!—1993 | Septemba 8
-
-
Niliona maoni hayo yote mawili kuwa yasiyokubalika, kwa kuwa yalikosa kweli ya Gospeli. Hayo yanapotoa Mathayo 16:18, 19 na yanaruhusu mafundisho yote yasiyo ya kimaandiko ya wakati uliopita na wakati ujao na masharti ya kanisa.b Niliona kwamba maneno ya Kigiriki yanayotumiwa katika andiko hili, peʹtra (namna ya kike), kumaanisha “mwamba,” na peʹtros (namna ya kiume), kumaanisha “kipande cha mwamba,” hayakutumiwa na Yesu kuwa ya maana sawa. Zaidi ya hilo, ikiwa Petro alikuwa amepewa uwezo wa kuwa mwamba, kama jiwe la pembeni, hakungelikuwa na mabishano miongoni mwa mitume baadaye juu ya ni nani aliyekuwa mkuu zaidi kati yao. (Linganisha Marko 9:33-35; Luka 22:24-26.) Pia, Paulo hangethubutu kumkemea Petro hadharani kwa ‘kutoenda sawasawa na ile kweli ya Injili.’ (Wagalatia 2:11-14) Niliamua kwamba wafuasi wote wa Kristo wapakwa kwa roho ni kama jiwe sawasawa, Yesu akiwa jiwe kuu la pembeni.—1 Wakorintho 10:4; Waefeso 2:19-22; Ufunuo 21:2, 9-14.
-
-
Sababu Iliyonifanya Niache Ukasisi kwa Ajili ya Huduma Bora ZaidiAmkeni!—1993 | Septemba 8
-
-
b Andiko hili kwa sehemu lasema hivi, kulingana na New American Bible ya Katoliki: “Nami nakuambia wewe, wewe ni ‘Mwamba,’ na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu . . . Lolote utakalotangaza kuwa limefungwa duniani litafungwa mbinguni; lolote utakalotangaza kuwa limeachiliwa duniani litafunguliwa mbinguni.”—Ona sanduku, ukurasa 23.
-