-
Yesu Ajapo Katika Utukufu wa UfalmeMnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
-
-
3, 4. (a) Yesu alisema nini siku sita kabla ya mgeuko-umbo? (b) Fafanua yale yaliyotukia wakati wa mgeuko-umbo.
3 Siku sita kabla ya mgeuko-umbo, Yesu aliwaambia wafuasi wake hivi: “Mwana wa binadamu akusudiwa kuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, na ndipo atakapomlipa kila mmoja kulingana na mwenendo wake.” Maneno hayo yangetimizwa kwenye “umalizio wa mfumo wa mambo.” Yesu aliendelea kutaarifu hivi: “Kwa kweli nawaambia nyinyi kwamba kuna baadhi ya wale ambao wamesimama hapa ambao hawataonja kifo hata kidogo mpaka kwanza wamwone Mwana wa binadamu akija katika ufalme wake.” (Mathayo 16:27, 28; 24:3; 25:31-34, 41; Danieli 12:4) Mgeuko-umbo ulitukia ukiwa utimizo wa maneno hayo ya mwisho.
-
-
Yesu Ajapo Katika Utukufu wa UfalmeMnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
-
-
5. Mgeuko-umbo ulimwathirije mtume Petro?
5 Mtume Petro tayari alikuwa amemtambua Yesu kuwa “Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16) Maneno ya Yehova kutoka mbinguni yalithibitisha utambulisho huo, na ono la kugeuka umbo kwa Yesu lilikuwa mwonjo wa kimbele wa kuja kwa Kristo katika nguvu na utukufu wa Ufalme, kuwahukumu wanadamu hatimaye. Miaka zaidi ya 30 baada ya mgeuko-umbo, Petro aliandika hivi: “Haikuwa kwa kufuata hadithi zisizo za kweli zilizotungwa kwa usanifu mwingi kwamba tuliwafahamisha nyinyi juu ya nguvu na kuwapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, lakini ilikuwa kwa kupata kuwa mashahidi wa kujionea fahari yake. Kwa maana alipokea kutoka kwa Mungu Baba heshima na utukufu, wakati maneno ya namna hii yalipopelekwa kwake kwa utukufu wenye fahari: ‘Huyu ni mwana wangu, mpendwa wangu, ambaye mimi mwenyewe nimemkubali.’ Ndiyo, maneno haya tuliyasikia yakipelekwa kutoka mbinguni tulipokuwa tungali pamoja naye katika mlima mtakatifu.”—2 Petro 1:16-18; 1 Petro 4:17.
-
-
Yesu Ajapo Katika Utukufu wa UfalmeMnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
-
-
7. (a) Ono la mgeuko-umbo lilianza kutimizwa lini? (b) Yesu aliwalipa baadhi ya watu kulingana na mwenendo wao lini?
7 Tangu mwanzo wa “siku ya Bwana” mwaka wa 1914, mengi ya maono ya Yohana yametimizwa. (Ufunuo 1:10) Namna gani ‘kuja kwa Yesu katika utukufu wa Baba yake,’ kama vile kulivyowakilishwa kimbele na mgeuko-umbo? Ono hilo lilianza kutimizwa wakati wa kuzaliwa kwa Ufalme wa kimbingu wa Mungu mwaka wa 1914. Yesu, kama vile nyota ya mchana, alipozuka katika mazingira ya ulimwengu wote mzima akiwa Mfalme aliyeketishwa karibuni katika kiti cha ufalme, tendo hilo, kwa kitamathali, lilikuwa kupambazuka kwa siku mpya. (2 Petro 1:19; Ufunuo 11:15; 22:16) Je, Yesu alilipa baadhi ya watu kulingana na mwenendo wao wakati huo? Ndiyo. Kuna uthibitisho wenye nguvu kwamba punde baada ya hapo, ufufuo wa kimbingu wa Wakristo watiwa-mafuta ulianza.—2 Timotheo 4:8; Ufunuo 14:13.
8. Ni mambo gani yatakayoutia alama upeo wa utimizo wa ono la mgeuko-umbo?
8 Lakini, hivi karibuni Yesu atawasili “katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye” ili kuhukumu wanadamu wote. (Mathayo 25:31) Wakati huo, atajifunua katika utukufu wake wote wenye fahari na kumpa “kila mmoja” malipo ya haki kwa mwenendo wake. Wale wenye mfano wa kondoo watarithi uhai udumuo milele katika Ufalme uliotayarishwa kwa ajili yao, na wale wenye mfano wa mbuzi wataondoka kuingia katika “kukatiliwa-mbali kudumuko milele.” Huo utakuwa umalizio mtukufu kama nini wa utimizo wa ono la mgeuko-umbo!—Mathayo 25:34, 41, 46; Marko 8:38; 2 Wathesalonike 1:6-10.
-
-
Yesu Ajapo Katika Utukufu wa UfalmeMnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
-
-
12. Katika kikao cha mgeuko-umbo, Musa na Eliya ni mifano ya nani?
12 Basi, Musa na Eliya wanawakilisha kimbele nani katika kikao cha mgeuko-umbo? Luka asema kwamba walionekana pamoja na Yesu “wakiwa na utukufu.” (Luka 9:31) Kwa wazi, wanawakilisha kimbele Wakristo ambao wametiwa mafuta kwa roho takatifu wakiwa “warithi-washirika” pamoja na Yesu na ambao hivyo walipokea lile tumaini la ajabu la “kutukuzwa pamoja” naye. (Waroma 8:17) Watiwa-mafuta wanaofufuliwa watakuwa pamoja na Yesu ajapo katika utukufu wa Baba yake ili ‘kumlipa kila mmoja kulingana na mwenendo wake.’—Mathayo 16:27.
-