HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MATHAYO 18-19
Uwe Mwangalifu Usijikwaze na Usiwakwaze Wengine
Yesu alitumia mifano kufundisha jinsi lilivyo jambo zito kukwazwa au kuwakwaza wengine.
“Kikwazo” kinamaanisha tendo au hali inayomwongoza mtu kufuata njia isiyofaa, kujikwaa au kuanguka kimaadili, au kuanguka katika dhambi
Ingekuwa afadhali kwa mtu anayemfanya mwingine akwazike kuanguka baharini akiwa amefungwa jiwe la kusagia shingoni
Yesu aliwashauri wafuasi wake waondoe hata kitu kilicho na thamani kama mkono au jicho ikiwa linawafanya wakwazike
Afadhali kuacha kitu tunachopenda sana ili tuingie katika Ufalme wa Mungu badala ya kukishikilia na hatimaye tutupwe Gehena, inayowakilisha uharibifu wa kudumu
Ni nini maishani mwangu ambacho kinaweza kuwa kikwazo, na ninaweza kuepukaje kujikwaza mwenyewe au kuwakwaza wengine?