-
Je! Wewe Unafanya Mapenzi ya Mungu?Mnara wa Mlinzi—1994 | Machi 1
-
-
“Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Je! katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye?”—Mathayo 21:28-31.
Jibu ni wazi. Kama vile ule umati uliomsikia Yesu, sisi tungeitikia, “Ni yule wa pili.” Lakini zaidi ya jambo hilo la wazi, kupitia kielezi hicho, Yesu alikuwa akituonyesha kwamba kufanya yale ambayo baba alitaka ndilo lililokuwa jambo la maana. Ingawa mwana wa pili alisema kwamba hakutaka kwenda, alienda hata hivyo akapongezwa kwa kufanya hivyo. Kufanya kazi ya aina ifaayo ni jambo la maana vilevile. Mwana wa pili alitenda kwa kufanya kazi katika shamba la mizabibu la babake; naye hakwenda kufanya kazi katika shamba la mizabibu lake mwenyewe.
-
-
Je! Wewe Unafanya Mapenzi ya Mungu?Mnara wa Mlinzi—1994 | Machi 1
-
-
Ni nani wafanyao mapenzi ya Mungu leo? Miongoni mwa wale watu wapatao bilioni mbili wanaodai kuwa wafuasi wa Yesu Kristo, ni wangapi walio kama yule mwana mchanga zaidi katika kielezi cha Yesu, aliyekwenda na kufanya mapenzi ya babake? Si ngumu kupata jibu. Wafuasi wa kweli wa nyayo za Yesu Kristo wangekuwa wakifanya kazi aliyosema wangefanya: “Na sharti Injili [habari njema, NW] ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.” (Marko 13:10) Mashahidi wa Yehova, ambao ni zaidi ya milioni nne na nusu ulimwenguni pote, wanahubiri kwa bidii habari njema za Ufalme wa Mungu na kufundisha wengine, wakielekezea Ufalme kuwa tumaini pekee la ainabinadamu la kupata amani na usalama. Je! wewe unashiriki kikamili katika kufanya mapenzi ya Mungu? Je! wewe unahubiri juu ya habari njema za Ufalme kama vile Yesu alivyofanya?—Matendo 10:42; Waebrania 10:7.
-