-
Kuokolewa Kutoka “Kizazi Kiovu”Mnara wa Mlinzi—1995 | Novemba 1
-
-
11. (a) Ni mwenye mamlaka yupi ambaye hasa anapaswa kutuongoza katika kujua jinsi ya kutumia he ge·ne·aʹ hauʹte? (b) Mwenye mamlaka huyo alitumiaje usemi huo?
11 Bila shaka, Wakristo wanaochunguza jambo hili hasa hukazia akili jinsi waandikaji wa Gospeli wenye kupuliziwa walivyotumia usemi wa Kigiriki he ge·ne·aʹ hauʹte, au “kizazi hiki,” katika kuripoti maneno ya Yesu. Sikuzote huo usemi ulitumiwa kwa njia hasi. Hivyo, Yesu aliwaita viongozi wa kidini wa Kiyahudi “nyoka, wana wa majoka” naye akaendelea kusema kwamba hukumu ya Gehena ingetekelezwa juu ya “kizazi hiki.” (Mathayo 23:33, 36) Hata hivyo, je, hukumu hiyo ilihusu viongozi wa kidini wenye unafiki peke yao? La hasha. Katika pindi kadhaa, wanafunzi wa Yesu walimsikia akisema juu ya “kizazi hiki,” sikuzote akitumia maneno hayo kwa maana pana zaidi. Maana gani hiyo?
-
-
Kuokolewa Kutoka “Kizazi Kiovu”Mnara wa Mlinzi—1995 | Novemba 1
-
-
13. Wanafunzi wake wakiwapo, Yesu aliwatambulisha nani na kuwashutumu kuwa ‘kizazi hiki kiovu’?
13 Baadaye katika 31 W.K., Yesu na wanafunzi wake walipofunga safari yao ya pili ya kuhubiri Galilaya, “baadhi ya waandishi na Mafarisayo” walimuuliza Yesu awape ishara. Aliwaambia pamoja na “umati” uliokuwapo: “Kizazi kiovu na chenye uzinzi chafuliza kutafuta ishara, lakini hakuna ishara kitakayopewa ila ishara ya Yona nabii. Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa katika tumbo la samaki mkubwa mno siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu atakavyokuwa katika moyo wa dunia siku tatu mchana na usiku. . . . Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia kwa kizazi kiovu hiki.” (Mathayo 12:38-46, NW) Kwa wazi, ‘kizazi hiki kiovu’ kilitia ndani viongozi wa kidini na “umati” ambao hawakupata kuelewa ishara iliyotimizwa katika kifo na ufufuo wa Yesu.d
-