“Njia Iliyo Pana na Rahisi”
“Laiti watu wangalijikaza iwapasavyo, laiti wasingelemewa na ugoigoi na utepetevu wao, laiti wangeshinda pupa yao, laiti wangekuwa imara kiadili, laiti hawangekuwa na ubinafsi na akili zenye kufikiria upande mmoja tu, laiti hawangeshughulikia vijambo visivyo vya maana na wasiwe wenye madharau na wapumbavu, laiti wangekuwa wenye moyo mkuu wa kutojali udhia mdogo-mdogo, laiti wangejua ni nini kilicho hatarini, laiti hawangekuwa wanafiki, laiti wangaliikanyaga chini ya nyayo zao njia iliyo pana na rahisi.”—Charles Malik, aliyekuwa hapo zamani msimamizi wa Kusanyiko Kuu la UM.
“Laiti wangejua ni nini kilicho hatarini,” akasema Malik. Zaidi ya karne 19 zilizopita, Kristo Yesu alinena juu ya ‘njia pana’ na ‘njia nyembamba iliyosonga,’ na akaeleza ni nini kilicho hatarini: “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”—Mathayo 7:13, 14.
Njia iliyo pana na yenye nafasi nyingi hufikia kikomo kamili; njia iliyo nyembamba na yenye kusonga hupanuka na haina kikomo.