Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Umati Mkubwa Ukamjia”
    ‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
    • 2 Baada ya Yesu kuwa na mazungumzo muhimu pamoja na viongozi fulani wa dini, kunakuwa na vurugu kidogo. Watu wanawaleta watoto wao wamwone. Inaonekana watoto hao wana umri mbalimbali, kwa kuwa Marko anawataja kwa kutumia neno lilelile alilotumia alipokuwa akizungumzia mtoto wa miaka 12, na Luka anatumia neno linaloweza kutafsiriwa ‘watoto wadogo.’ (Luka 18:15; Marko 5:41, 42; 10:13) Bila shaka, kwa kawaida mahali popote penye watoto huwa na kelele na vurugu. Wanafunzi wa Yesu wanawakemea wazazi, labda wakifikiri kwamba Bwana ana shughuli nyingi sana hivi kwamba hawezi kuwa pamoja na watoto. Yesu anafanya nini?

  • “Umati Mkubwa Ukamjia”
    ‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
    • 4, 5. (a) Ni nini kinachotuonyesha kwamba ilikuwa rahisi kumkaribia Yesu? (b) Tutachunguza maswali gani katika sura hii?

      4 Ikiwa Yesu angekuwa mtu mkali, asiye na urafiki, au mwenye kiburi, huenda watoto hao hawangevutiwa naye wala wazazi wao hawangekuwa huru kumkaribia. Hebu wazia jinsi wazazi wa watoto hao wanavyohisi mtu huyo mwenye fadhili anapowaonyesha upendo watoto wao, anapowabariki na kusema kwamba watoto hao ni wenye thamani machoni pa Mungu! Kwa kweli, ingawa Yesu alikuwa na majukumu mazito sana, watu walipenda kumkaribia zaidi kuliko mwanadamu mwingine yeyote.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki