Sarafu za Kale Zashuhudia Ukweli wa Kiunabii
ZILE sarafu ambazo zinalia-lia katika mfuko wako au kibeti chako huenda zikawa hazina ujumbe wa maana sana isipokuwa ule wa kwamba wewe unaweza kununua kitu fulani kidogo. Lakini sarafu fulani-fulani zina ujumbe mzito zaidi ya huo.
Muda mfupi tu kabla ya kifo chake, Yesu alitoa unabii kwamba uharibifu mbaya sana ulikuwa unakuja juu ya Yerusalemu, mji mkuu wa lile taifa la Israeli lisilo na uaminifu. (Mathayo 23:37–24:2) Yesu alisema: “Wakati ninyi mtaona Yerusalemu umezungukwa na majeshi yenye kupiga kambi, ndipo mjue kwamba kule kuachwa ukiwa kwa huo kumekaribia. Ndipo acheni wale walio katika Yudea waanze kukimbia kwenda kwenye ile milima . . . kwa sababu hizi ni siku za kupimilia haki, kwamba mambo yale yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa.”—Luka 21:20-22, NW.
Wakati huo, Wayahudi walikuwa chini ya uongozi mkali wa Roma yenye nguvu nyingi. Basi, ni jinsi gani unabii wa Yesu ungeweza kuja kuwa kweli? Haya basi, Wayahudi walifanya maasi ya kutafuta mapinduzi katika 66 W.K., Sesio Galo aliongoza majeshi ya Kiroma yenye uwezo mwingi dhidi yao na hata akazingira Yerusalemu, kama vile Yesu alivyokuwa ametabiri. Ndipo, bila sababu yo yote yenye kuonekana, wale Waroma wakafanya haraka kujiondoa. Waasi wale walifanya shangwe katika ushindi ambao ulionekana kama kwamba ulionyesha walikuwa wamepata uhuru hatimaye. Hata walipiga chapa ya sarafu-sarafu, kama ile moja inayoonwa hapa. (Namba 1,2)
Lakini wanafunzi wa Kristo, hawakudanganywa. Kwa kutii onyo lake ‘kukimbia kwenda kwenye milima,’ wao waliacha makao yao katika Yudea. Wao walikimbia wakashuka kwenda kwenye ule Mto Yordani na kuvuka ng’ambo yao, halafu wakaenda kaskazini kutulia katika Pella. Lakini je! jambo hilo Iilihitajiwa kabisa, kwa kuwa miaka kadha ilipita na wale Wayahudi waliokuwa katika Yerusalemu walibaki wakiwa huru? Ingawa Wayahudi hao walikuwa na sarafu zao wenyewe, karibuni wao hawangepata chakula cho chote cha kununua kwa sarafu hizo. Kwa sababu gani?
Tazama sarafu iliyoelezwa kwa picha namba 3 na 4. Wewe unaona kile kichwa cha jenerali Mroma Vespasian, ambaye aliwekwa rasmi kuchukua mahali pa Sesio Galo. Kulingana na Encyclopsedia Britannica, Vespasian alipaswa “kuendesha vile vita katika Yudea, ambayo ilikuwa ikitisha kutokeza zahama kubwa katika sehemu zote za ile Mashariki, kwa sababu ya wazo lililoenea kote kote katika sehemu hizo kwamba kutokana na Yudea wangekuja watawala wa wakati ujao wa ulimwengu. Vespasian, ambaye alikuwa na tabia imara ya ushirikina, alifanywa awe na itikadi ya kwamba yeye mwenyewe ndiye angetimiza taraja hilo.” Mwanahistoria Yosefo anasimulia kwa uwazi mwingi mapigano yaliyotokea. Baada ya Vespasian kuwa maliki katika 69 W.K., Tito mwana wake aliendeleza vita, hata akaleta mazingiwa Yerusalemu. Ukosefu mkubwa wa chakula na ogofyo vilikumba wale walionaswa mtegoni humo ndani. Wakati mji huo ulipoanguka, kuta zao zilibomolewa-bomolewa na hekalu lao likaharibiwa.
Ni nini iliyokuwa gharama ya kibinadamu kwa wale ambao walikuwa wamepuuza onyo la Yesu? “Ijapokuwa wao walikuwa wanaume waliokuwa wamefikia nusu ya kufa njaa, wao walikinga ngome yao kwa kujinata kiajabu sana, wakipoteza zaidi ya mia moja elfu ya washiriki wao katika mwendeleo huo. Wengi tena wa karibu hesabu ile ile, baada ya kulazimika kushuhudia ule mwono wenye maumivu makali sana wa kuona hekalu lao takatifu likiteketezwa kwa moto, likiporwa, na kuharibiwa kwa ukamili, walichukuliwa katika utumwa, wengi wao wakilazimishwa . . . kutumikia wakiwa wapigana-na-nduli katika nyanja za maonyesho wasio na tumaini kuepa kifo au wakiwa mawindo hohehahe kwa hayawani-mwitu katika yale ‘machezo’ ya kutazamisha ambayo yule Tito mwenye shangwe ya ushindi aliweka jukwaani.”—Coins of Bible Days.
Kitabu hicho kinaeleza kwamba katika 71 W.K., Vespasian na Tito walipiga miguu ya vishindo kwa shangwe ya ushindi wakipitia Roma ili kuadhimisha ushindi huo. Lakini “zenye kudumu zaidi ya magwaride yo yote au sherehe za miadhimisho zilikuwa zile sarafu nyingi sana ‘za ushindi.’” Moja ilikuwa sarafu hii ya dhahabu (Namba 5) iliyopigwa chapa na Vespasian ili kukumbuka ule ushindi wa Kiroma juu ya Yudea.
Ingawa labda Wayahudi wengi walikuwa wamedhihaki taarifa ya Yesu ya kiunabii juu ya ule mwisho wa mfumo wa Kiyahudi, maneno yake yalikuja kuwa kweli, kama vile sarafu hizi zinavyoshuhudia. Unabii wa Yesu una utimizo mkubwa leo, ukieleza kwenye afa linalokaribia mfumo uliopo wa mambo wa ulimwenguni pote. Wewe una deni kwako mwenyewe kujifunza ni nin ujumbe huu wa kisasa na ni jinsi gani wewe unavyoweza kuepuka kuwa jeruhi wa afa hili linalokaribia.
[Sanduku/Pictures katika ukurasa wa 31]
1. Upande wa usoni: Pruta (peruta) ya shaba-nyeusi ambayo ilipigwa chapa baada ya lile Asi la Kwanza la kutaka mapinduzi (66-70 W.K.), ikionyesha gudulia (chombo chenye vishikio viwili.) Ule mpangilio wa herufi za Kiebrania unasema “Mwaka namba mbili,” maana yake 67 W.K., ule mwaka wa pili wa serikali ya Wayahudi kujitawala wenyewe
2.Upande wa nyuma: Jani la mzabibu likiwa limezungukwa na yale maneno “Uhuru wa Sayuni” au “Kukombolewa kwa Sayuni”
3.Upande wa usoni: Sarafu-sestertioya shaba-nyeusi ambayo ilipigwa chapa na Maliki Vespasia ili kukumbuka ule ushinde wa Yudea. Mfupisho ws zile herufi za Kilatini zilizozunguka taswira yake n IMPjeratorj (Maliki) CAES[ar] VESPASIAN[us] AVG[ustus], P[ontifexj M[aximusj (kuhani mkuu),Tr[ibuniciaj P[otestate] (mshika mamlaka ya utawala) P[ater] Pfatriae] (baba ya nchi-baba ya kuzaliwa), Co[n]S[ul] III (katika mara yake ya tatu kuwa na cheo cha kuwa mwakilishi wa mashauri ya nchi yake), na hiyo inaonyesha tarehe ya sarafu hiyo kuwaya71 W.K.
4.Upande wa nyuma: Kushoto yuko Maliki Vespa sian (au Jenerah Tito) mchachawa akiwa na silahi katika silaha za kijeshi, akiwa ameshika mkuki na sime, wayo wa mguu ukiwa umetulia juu ya helmet Kuume yuko Myahudi wa kike akiwa ameketi juu y deraya chini ya mtende; yeye yumo katika maombolezo na kilio. Yale maneno IVDAEA CAPTA yanamaanisha “Yudea Yenye Kutekwa.” Sarafu hii ilipigwa chapa ya herufi S[enatus] C[onsulto], maana yake “kwa idhini ya Seneti’’
5.Upande wa nyuma: Sarafu ya kidhahabu iliyotokezwa na Vespasian ikionyesha Yudea katika maombolezo
[Credit Line]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.