-
AganoUfahamu wa Kina wa Maandiko
-
-
Agano la Kuwa Kuhani Kama Melkizedeki. Agano hilo linatajwa kwenye Zaburi 110:4, na mwandikaji wa kitabu cha Biblia cha Waebrania analitumia kumhusu Kristo kwenye 7:1-3, 15-17. Ni agano ambalo limefanywa na Yehova pamoja na Yesu Kristo peke yake. Inaonekana Yesu alilirejezea alipokuwa akifanya agano kwa ajili ya ufalme na wafuasi wake. (Lu 22:29) Kwa kiapo cha Yehova, Yesu Kristo, Mwana wa Mungu wa kimbingu, angekuwa kuhani kulingana na ile namna ya Melkizedeki. Melkizedeki alikuwa mfalme na kuhani wa Mungu duniani. Yesu Kristo angeshikilia vyeo vyote viwili vya kuwa Mfalme na Kuhani Mkuu huko mbinguni, wala si duniani. Yeye aliwekwa akae daima kwenye cheo baada ya kupanda mbinguni. (Ebr 6:20; 7:26, 28; 8:1) Agano hilo ni lenye kutenda kazi milele, kwa kuwa Yesu atatenda akiwa Mfalme na Kuhani Mkuu milele chini ya mwelekezo wa Yehova.—Ebr 7:3.
-
-
AganoUfahamu wa Kina wa Maandiko
-
-
Agano la Yesu Pamoja na Wafuasi Wake. Kwenye usiku wa Nisani 14, 33 W.K., baada ya kusherehekea Mlo wa Jioni wa Bwana, Yesu alifanya agano hili pamoja na mitume wake waaminifu. Yeye aliwaahidi mitume wake waaminifu 11 kwamba wangeketi juu ya viti vya ufalme. (Lu 22:28-30; linganisha 2Ti 2:12.) Baadaye, alionyesha kwamba ahadi hiyo iliwahusisha ‘washindi’ wote waliozaliwa kwa roho. (Ufu 3:21; ona pia Ufu 1:4-6; 5:9, 10; 20:6.) Kwenye siku ya Pentekoste yeye aliwazindulia agano hili kwa kuwatia mafuta kwa roho takatifu wanafunzi wale waliokuwapo katika chumba cha juu katika Yerusalemu. (Mdo 2:1-4, 33) Wale ambao wangeshikamana naye kupitia majaribu, wafe kifo cha aina aliyokufa (Flp 3:10; Kol 1:24), wangetawala pamoja naye, waushiriki utawala wake wa Ufalme. Agano hilo linaendelea kutenda kazi milele kati ya Yesu Kristo na wafalme hawa wenzi.—Ufu 22:5.
-