-
Watawala Katika Makao ya RohoMnara wa Mlinzi—1995 | Julai 15
-
-
Muda mfupi baada ya ubatizo wake, Yesu alijaribiwa na kiumbe cha roho kisichoonekana kiitwacho Shetani Ibilisi. Ikieleza moja la majaribu hayo, Biblia husema: “Ibilisi akamchukua [Yesu] mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha (“falme zote za ulimwengu,” New World Translation) milki zote za ulimwengu, na fahari yake.” (Mathayo 4:8) Kisha Shetani akamwambia Yesu hivi: “Nitakupa mamlaka yote hii na utukufu wazo, kwa sababu nimekabidhiwa, na yeyote nimtakaye mimi humpa hiyo. Kwa hiyo, wewe ukifanya tendo la ibada mbele yangu, yote itakuwa yako.”—Luka 4:6, 7, NW.
Shetani alidai kuwa na mamlaka juu ya falme zote, au serikali, za ulimwengu huu. Je, Yesu alikataa dai hili? La. Kwa kweli, alilithibitisha kwenye tukio jingine kwa kurejezea Shetani kuwa “mkuu (“mtawala,” NW) wa ulimwengu.”—Yohana 14:30.
Kulingana na Biblia, Shetani ni malaika mwovu aliye na uwezo mkubwa. Mtume Mkristo Paulo anamhusianisha Shetani na “majeshi ya roho waovu” naye anazungumza juu yao kuwa “watawala wa ulimwengu wa giza hili.” (Waefeso 6:11, 12, NW) Zaidi ya hayo, mtume Yohana alisema kwamba “dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.” (1 Yohana 5:19) Kitabu cha Biblia cha Ufunuo husema kwamba Shetani ‘huudanganya ulimwengu wote.’ (Ufunuo 12:9) Kwa maneno ya ufananisho, Ufunuo pia humfafanua Shetani kuwa joka ambalo linaupa mfumo wa kisiasa wa ulimwengu “nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.”—Ufunuo 13:2.
Matukio ya ulimwengu pia hushuhudia kwamba kuna uwezo mwovu unaotenda kazi, unaochochea binadamu wajiumize. Ni kwa sababu gani nyingine ambayo serikali za binadamu hushindwa kuendeleza amani? Nini kingine kingeweza kufanya watu wachukiane na kuchinjana? Akifadhaishwa na machinjo na kifo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, shahidi mmoja aliyejionea kwa macho alisema: “Mimi sijui jinsi haya yangeweza kutokea. Ni zaidi ya chuki. Ni roho mwovu ambaye anatumia binadamu hawa kumalizana.”
-
-
Watawala Katika Makao ya RohoMnara wa Mlinzi—1995 | Julai 15
-
-
Kwa Nini Shetani Ameruhusiwa Kutawala
Je, unakumbuka yale Shetani alimwambia Yesu kuhusu utawala juu ya dunia? “Nitakupa mamlaka yote hii . . . kwa sababu nimekabidhiwa,” Shetani akasema. (Luka 4:6, NW) Taarifa hiyo inaonyesha kwamba Shetani Ibilisi yuna mamlaka kwa ruhusa ya Mungu tu. Lakini kwa nini Mungu amvumilie Shetani?
-