-
Msamaria Athibitika Kuwa Jirani MwemaMnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
-
-
Walifanya Mapenzi ya Yehova
Msamaria Athibitika Kuwa Jirani Mwema
KATIKA siku ya Yesu, uhasama wenye kuonekana wazi ulikuwako kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi. Baada ya muda, Mishnah ya Kiyahudi hata ilitia ndani sheria iliyowakataza wanawake Waisraeli kuwasaidia wasio Wayahudi wakati wa kuzaa, kwa kuwa jambo hilo lingesaidia tu kuleta mtu mwingine asiye Myahudi duniani.—Abodah Zarah 2:1.
Wasamaria walikuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Wayahudi kidini na pia kijamii, kuliko wale wasio Wayahudi. Hata hivyo, wao pia walionwa kuwa watu waliotengwa na jamii. “Kwa maana Wayahudi hawana shughuli pamoja na Wasamaria,” akaandika mtume Yohana. (Yohana 4:9) Kwa kweli Talmud ilifundisha kwamba “kipande cha mkate ambacho Myahudi alipewa na Msamaria kilikuwa kichafu zaidi kuliko nyama ya nguruwe.” Wayahudi wengine hata walitumia neno “Msamaria” kama usemi wa kudharau na kuaibisha.—Yohana 8:48.
-
-
Msamaria Athibitika Kuwa Jirani MwemaMnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
-
-
Yesu aliendelea kusema hivi: “Msamaria fulani mwenye kusafiri katika ile barabara alikuja akamkuta.” Bila shaka kutajwa kwa Msamaria kuliongeza udadisi wa huyo mwanasheria. Je, Yesu angekubali maoni yasiyofaa ya jamii hiyo? Kinyume cha hilo, huyo Msamaria alipomwona msafiri aliyepatwa na msiba “akasukumwa na sikitiko.” Yesu akasema hivi: “Kwa hiyo akamkaribia akafunga majeraha yake, akimwaga mafuta na divai juu yayo. Kisha akampandisha juu ya hayawani wake mwenyewe akamleta kwenye hoteli ndogo na kumtunza.b Na siku iliyofuata akatoa dinari mbili, akampa hizo mtunza-hoteli, na kusema, ‘Mtunze, na chochote kile utumiacho mbali na hiki, mimi nitakulipa nirudipo hapa.’”—Luka 10:33-35.
-