-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1986 | Februari 15
-
-
Katika Yohana sura ya 12 chakula kilicholiwa nyumbani kwa Simoni kinatajwa katika hali tofauti. Andiko la Yohana 12:1 (NW) linaripoti kwamba Yesu alifika Bethania karibu na Yerusalemu “siku sita kabla ya sikukuu ya Kupitwa,” na hiyo ingekuwa ni Nisani 8. Halafu mistari 2-8 inaeleza chakula cha jioni katika Bethania, na mistari 9-11 inatuambia kwamba Wayahudi waliosikia kwamba Yesu alikuwa karibu walikuja kumwona. Mistari 12-15 inasema kwamba “siku iliyofuata” Kristo aliingia Yerusalemu kwa ushindi. (Linganisha Matendo 20:7-11.) Kwa hiyo, andiko la Yohana 12:1-15 linaonyesha kwamba kile chakula kilicholiwa nyumbani kwa Simoni kilitukia Nisani 9 jioni, ambayo kulingana na kalenda ya Kiyahudi ingekuwa ndio mwanzo wa siku mpya, kisha ikafuatwa na kupanda kwa Yesu kuingia Yerusalemu katika kipindi chenye mwangaza cha siku hiyo (Nisani 9).
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1986 | Februari 15
-
-
Ingawa hivyo, Yohana anatoa tarehe ya waziwazi juu ya wakati karamu ilipofanyika, kuonyesha kwamba yeye aliitaja kulingana na mahali ilipopasa kuwa kulingana na utaratibu wa orodha za matukio. Jambo hilo linaunga mkono kukata shauri kwamba chakula cha jioni kwenye nyumba ya Simoni kilitukia baada ya Yesu kufika Bethania Nisani 8, 33 W.K. Zaidi ya hilo, kumbuka habari zinazoelezwa na Yohana kwamba Wayahudi ‘waliopata kujua kwamba Yesu sasa alikuwa katika Bethania’ walikuja kutoka Yerusalemu ili wamwone yeye na Lazaro, ambaye pia aliishi katika Bethania na ambaye dada zake walikuwa karamuni. Ziara hiyo ya Wayahudi ambao walikuwa wametoka tu ‘kupata kujua’ kwamba Yesu alikuwa Bethania ingeelekea zaidi kuwa ilitokea kabla ya yeye kuingia Yerusalemu, na inaweza i kuwa ilisaidia kufanya Kristo apokewe kwa shauku wakati alipopanda kuuingia mji huo “siku iliyofuata, mchana wa Nisani 9.
-