-
“Ninakata Rufaa kwa Kaisari!”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
5. Festo alishughulikiaje kesi ya Paulo?
5 Siku kadhaa baadaye, Festo “akaketi kwenye kiti cha hukumu” jijini Kaisaria.b Paulo na wanaomshitaki walikuwa wamesimama mbele yake. Akijibu mashtaka yao yasiyo na msingi, Paulo akasema: “Sijatenda dhambi yoyote dhidi ya Sheria ya Wayahudi wala dhidi ya hekalu wala dhidi ya Kaisari.” Mtume huyo hakuwa na hatia na alistahili kuachiliwa huru. Festo atatoa uamuzi gani? Akitamani kukubaliwa na Wayahudi, anamuuliza Paulo: “Je, ungependa kupanda kwenda Yerusalemu ukahukumiwe huko mbele yangu kuhusu mambo haya?” (Mdo. 25:6-9) Pendekezo la kipumbavu sana. Ikiwa Paulo angerudishwa Yerusalemu, watu wanaomshtaki ndio ambao wangemhukumu, na bila shaka angeuawa. Katika kisa hiki, Festo alikuwa akihangaikia manufaa yake ya kisiasa badala ya kuzingatia haki. Pontio Pilato, gavana aliyemtangulia, alitenda vivyo hivyo katika kesi iliyomhusu Yesu. (Yoh. 19:12-16) Leo pia, huenda mahakimu wakatenda isivyo haki ili kuwapendeza wanasiasa. Kwa hiyo, tusishangae mahakama zinapotoa uamuzi usiopatana hata kidogo na ushahidi uliotolewa katika kesi zinazowahusu watu wa Mungu.
-
-
“Ninakata Rufaa kwa Kaisari!”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
b “Kiti cha hukumu” ni kiti kilichokuwa juu ya jukwaa lililoinuliwa. Kwa kuwa kiti hicho kilikuwa juu, basi ilionekana kana kwamba uamuzi wa hakimu unapaswa kuheshimiwa na hauwezi kupingwa. Pilato aliketi juu ya kiti hicho aliposikiliza kesi ya Yesu.
-