-
Yehova Ni Msaidizi WetuMnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
-
-
20, 21. Mtume Paulo aliimarishwa na ndugu kutoka Roma chini ya hali gani?
20 Masimulizi yenye kugusa moyo hasa ni yale yanayohusu jinsi watumishi wa Yehova walivyojitahidi kuimarishana na kutiana moyo. Fikiria mfano unaomhusu mtume Paulo. Alipokuwa safarini kuelekea Roma akiwa mfungwa, Paulo alipitia barabara kuu ya Roma iliyoitwa Njia ya Apio. Sehemu ya mwisho ya safari hiyo ilikuwa ngumu hasa kwa kuwa iliwabidi wasafiri kupitia eneo tambarare lenye majimaji.a Akina ndugu katika kutaniko la Roma walijua kwamba Paulo alikuwa anakuja. Wangefanya nini? Je, wangeendelea kustarehe katika nyumba zao jijini hadi Paulo afike ndipo waende kumpokea?
21 Luka, mwandikaji wa Biblia, aliyeandamana na Paulo katika safari hiyo, anatuambia yaliyotukia: “Kutoka huko [Roma] akina ndugu, waliposikia habari juu yetu, wakaja kukutana nasi mpaka Soko la Apio na Mikahawa Mitatu.” Je, unaweza kuwazia yaliyotukia? Walipojua kwamba Paulo alikuwa anakuja, kikundi cha akina ndugu walisafiri kutoka Roma ili kukutana naye. Baadhi ya ndugu hao walikuwa wakimngojea katika Soko la Apio, kituo mashuhuri cha kupumzikia kilichokuwa umbali wa kilometa 74 hivi nje ya Roma. Ndugu wale wengine walikuwa wakimngojea kwenye Mikahawa Mitatu, kituo cha kupumzikia kilichokuwa umbali wa kilometa 58 hivi nje ya jiji. Paulo aliitikiaje? Luka anaripoti hivi: “Alipowaona, Paulo akamshukuru Mungu na kujipa moyo.” (Matendo 28:15) Hebu wazia jambo hilo, Paulo aliimarika na kutiwa moyo alipowaona ndugu hao waliojitahidi kufunga safari hiyo ndefu! Naye Paulo alimshukuru nani kwa msaada huo? Alimshukuru yule aliyehusika, Yehova Mungu.
-
-
Yehova Ni Msaidizi WetuMnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
-
-
a Mtunga-mashairi Mroma Horace (65—8 K.W.K.), aliyesafiri katika njia hiyohiyo, alieleza kuhusu magumu ya sehemu ya mwisho ya safari hiyo. Horace alisema kwamba Soko la Apio lilikuwa “limesongamana na wenye mashua na wenye mikahawa wachoyo.” Alilalamika kuhusu “chawa na vyura waliolaaniwa” na maji “mabaya sana.”
-