Je! Wewe Hutafuta Hazina Zilizofichika?
“Maarifa sahihi kuhusu Mungu na Yesu Bwana wetu na yaongezee nyinyi fadhili zisizostahiliwa na amani.”—2 PETRO 1:2, NW.
1, 2. Ni mambo gani hufanya dhahabu iwe yenye thamani kubwa na ya bei ghali
KWA nini dhahabu ni ya bei ghali sana? Hiyo ni madini nyororo tu, na hali thamani yayo hufikia mamia ya dola kwa kila wakia. Ni kweli kwamba ina wororo wa kuweza kuundwa-undwa iwe na maumbo tofauti na iwapo ni pete au kikuku huwa ni pambo la kuvutia. (1 Timotheo 2:9; Yakobo 2:2) Hata hivyo, kama ungepotea jangwani, uwe unakufa kwa sababu ya njaa na kiu, hungeweza kuila wala kuinywa. Katika hali hiyo pande la mkate au sahani ya wali pamoja na maji ya kunywa vingeuzidi kwa mbali ustahiki wa dhahabu.
2 Basi, kwa nini dhahabu huthaminiwa sana? Kwanza, ni chache sana tena ni haba. Kwa kielelezo, wakati ule mgodi wa dhahabu uitwao Empire katika Kalifornia ya kaskazini ulipofungwa katika 1957 kwa sababu haukuleta tena faida, wachimba-migodi walikuwa wakichimba kina cha kuteremka chini meta zaidi ya 1,500 bila kwenda kombokombo lakini ikawa lazima washuke kilometa 3 za kwenda kando kimshadhari ili waifikie dhahabu. Kufikia hatua hiyo, bei ghali ya dhahabu ilikuwa imeifanya istahiki kufanyiwa ile jitihada kubwa sana ya kuitafuta.
3. Ni hazina gani ambayo twaweza kutafuta?
3 Ingawa hivyo, sisi twaweza kuchimba tutafute kitu chenye thamani kubwa kuliko dhahabu. Nini hicho? Mfalme Sulemani mwenye hekima alitoa jibu miaka 3,000 hivi iliyopita: “Ikiwa, zaidi ya hilo, wewe wapaaza wito kuomba uelewevu wenyewe na wewe watokeza sauti yako kuomba utambuzi wenyewe, ikiwa wewe unaendelea kuutafuta kama kutafuta fedha, na unaendelea kuutafuta kama kutafuta hazina zilizofichika, hapo wewe utaelewa kuhofu Yehova, na wewe utapata yale maarifa hususa kuhusu Mungu.” Wazia wanadamu duni wakiweza kupata “maarifa hususa kuhusu Mungu”!—Mithali 2:3-5, NWa
Kwa Nini Wote Wahitaji Maarifa Sahihi
4. Ni nini chapasa kuhusishwa ndani ya maarifa sahihi ya Mkristo?
4 Tangu wakati wa Kristo, maarifa hayo yenye kuhitajiwa sana yamepanuka yakahusisha mambo mengi kuliko yale waliyokuwa nayo wanaume na wanawake Waebrania wa zamani. Kama vile Paulo alivyoeleza jambo hilo: “Kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, apate kuwapa nyinyi roho ya hekima na ya ufunuo katika maarifa sahihi ya yeye; macho ya moyo wenu ukiisha kuwa umeangaziwa nuru, kwamba nyinyi mpate kujua ni nini tumaini ambalo yeye aliitia nyinyi, ni nini matajiri matukufu ambayo yeye awatolea watakatifu kama urithi.”—Waefeso 1:17, 18, NW.
5. Kwa nini wapakwa-mafuta wahitaji kutoa uangalifu wa daima kuhusu maarifa yao ya penzi la Mungu?
5 Huko nyuma, hili lilikuwa shauri la moja kwa moja kwa ndugu za Kristo wapakwa-mafuta walio watakatifu, na lingali hivyo leo. Wakiwa sehemu ya pili ya “mbegu” ya ahadi, hao ni shabaha za pekee za kupinduliwa kiroho na Shetani. (Wagalatia 3:2629; Waefeso 6:11, 12) Ni lazima wapakwa-mafuta hasa wahakikishe wito wao kwa kutokosa kujali ile zawadi ya bure ya fadhili zisizostahiliwa za Mungu. Hiyo ndiyo sababu ni lazima wao waimarishe daima maliasili zao za kiroho kwa kutengeneza upya maarifa sahihi waliyo nayo kuhusu penzi na Neno la Mungu.—Waefeso 3:7; Waebrania 6:4-6; 2 Petro 1:912.
6. (a) Kwa nini sisi sote twahitaji maarifa sahihi, bila kujali kama tumaini letu ni la kimbingu au la kidunia? (b) Ni kitu gani chatakiwa ili kupata maarifa sahihi?
6 Namna gani wale ambao tumaini lao ni kupata uhai wa milele duniani? Kwa nini maarifa sahihi ni muhimu kwao? Kwa sababu hakuna vipimo mbalimbali vya uaminifu wa maadili ya Kikristo, kana kwamba kuna kiwango kilicho juu kwa wapakwa-mafuta, ambao wana tumaini la kimbingu, kwa kuzidi kile cha kondoo wengine, ambao wana tumaini la kidunia. (Yohana 10:16; 2 Petro 3:13) Kanuni za Kikristo hutumika kwa wote kwa njia yenye usawa. Kwa sababu hiyo, sisi sote twahitaji kujazia nguvu za betri zetu za kiroho kwa kuzitia maarifa sahihi kwa ukawaida. Lakini wakati na jitihada vyahusika. Ni lazima tujitie katika uchimbaji wa kiroho, kana kwamba ni kwa kutafuta hazina zilizofichika.—Zaburi 105:4, 5.
Kununua Kabisa Wakati wa Kuchimba
7. (a) Kuna magumu gani ambayo yangeweza kuleta kizuizi tusipate maarifa sahihi? (b) Huenda matokeo ya kutojali hali ya kiroho yakawa nini?
7 Watu walio wengi leo huendesha maisha zenye shughuli, na sisi Wakristo twaonekana kuwa wenye shughuli nyingi hata kuliko walio wengi kati yao, tukiwa na ratiba zetu za mikutano ya Biblia, utumishi wa shambani, kazi ya kimwili, kazi ya nyumbani, kazi ya shule, na kadhalika. Hata hivyo, sawa na vile sisi huratibu kila siku wakati wa kula, ndivyo ilivyo lazima tuweke kando wakati wa kulisha akili yetu na hali yetu ya kiroho. Yesu hakutamka upuuzi aliponukuu Kumbukumbu 8:3: “Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu [Yehova, NW].” (Mathayo 4:4) Tukikosa kujali hali yetu ya kiroho, twakosa kujali thamani zetu za maadili ya kiroho na tumaini letu kwa wakati ujao. Hapo ndipo twaweza kuanza kuteleza na kuyumbayumba. Kwa hiyo twaweza kutafutaje wakati wa funzo la kibinafsi la Biblia lililo na ukawaida?
8. Ni mashauri gani ya Kimaandiko hutupa sisi maoni yafaayo kuhusu funzo la kibinafsi?
8 Maneno ya mtume Paulo yafaa sana: “Endelezeni uangalifu wa kujali sana kwamba jinsi nyinyi mwatembea si kama watu wasio na hekima bali kama walio na hekima, mkijinunulia kabisa ule wakati wenye fursa, kwa sababu siku ni zenye uovu. Kwa sababu hii komeni kuwa wasiosababu mambo kiakili, bali endeleeni kuwa na ufahamivu penzi la Yehova ni nini.” Twaweza kuwa na ufahamivu penzi la Yehova ni nini ikiwa tu tutatoa uangalifu kuhusu Neno lake kwa funzo letu la kibinafsi. Na hiyo yamaanisha ni lazima ‘tununue kabisa ule wakati wenye fursa’ au ‘tufanye utumizi bora zaidi wa wakati wetu.’—Waefeso 5:1517, NW; Phillips.
9. Tungeweza kuwa tukipoteza wapi wakati ambao waweza kukombolewa kwa ajili ya funzo la kibinafsi? Toa mambo uliyojionea binafsi.
9 Tukichanganua utendaji wetu mbalimbali wa kila siku ambao hatuuhitaji sana, twapata kwamba sisi hutumiaje mwingi wa wakati ambao sisi huwa huru? Je! sisi huutumia tukiwa mbele ya televisheni? Chombo hicho chenye kuzubaisha akili za watu zikawa ni kama zimelala usingizi chaweza kuibia maisha yetu muda upatao saa mbili hadi tano hivi kila jioni! Wewe binafsi hutumia saa ngapi kwa siku ukiangalia televisheni? Mara nyingi, mambo yenye kuonyeshwa hushusha tabia kwa kukazia jeuri na ngono. Na mara nyingi huwa yamepangwa kwa njia ya kuvutia “tamaa ya mnofu na tamaa ya macho na wonyesho mshaufu wa mali za maisha za mtu.” (1 Yohana 2:1517, NW) Hata hivyo, wengi hawana uthabiti wa nia ili waweze kuifunga televisheni. Ndiyo, kivumbuo hiki cha ki-siku-hizi chaweza kula sehemu kubwa ya kifaidio chetu chenye thamani kubwa zaidi, wakati.
10. Kwa nini ni jambo la maana sana leo tutumie wakati wetu kwa hekima?
10 Tukifuata haki katika kujichunguza wenyewe, tutatambua kwamba kwa kawaida huwa yawezekana kukomboa wakati wa utendaji mbalimbali wenye kuhitajiwa sana, kama funzo la Biblia. Na funzo la kibinafsi la Biblia ambalo huongoza kwenye maarifa sahihi lahitajiwa sana kwa Mkristo katika hizi nyakati zenye hatari. Hata hivyo, kukiwa na watu zaidi ya 41,000 waliotengwa na ushirika mwaka jana, ni wazi kwamba ndugu na dada wengi wamekosa kujali hali yao ya kiroho. Kuvaa na kudumisha “suti kamili ya silaha kutoka kwa Mungu” si jambo la kufanywa vivi hivi tu bila kusudi. Sawa na vile ilivyo kuhusu askari aliyevaa silaha halisi, huu ni wajibu wa kila siku.—Waefeso 6:10-18, NW; Warumi 1:28-32; 2 Timotheo 3:1.
11. Ni kielelezo gani ambacho jamaa ya Betheli huweka katika kujipanga kitengenezo kwa ajili ya funzo la jamaa?
11 Kuzunguka ulimwengu, wale washirika zaidi ya 9,000 wa jamaa za Betheli 95 kwenye ofisi za matawi za Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi huwa na funzo lao la jamaa kila jioni ya Jumatatu. Wao hujifunza Mnara wa Mlinzi kwa kujitayarishia mkutano wa mwisho-juma, na katika pindi nyingi huwa pia na mhadhara wa Biblia au kipindi cha darasa kwa ajili ya washirika wapya zaidi wa jamaa. Naam, Jumatatu ndio usiku wa funzo kwa jamaa ya Betheli ulimwenguni pote. Kipindi chenu nyinyi cha funzo la kibinafsi au la kijamaa huwa lini?—Waebrania 10:24, 25.
Vyombo vya Kazi na Jinsi ya Kuvitumia
12. Ni mambo gani ya kutokeza kuhusiana na funzo yaliyomo katika New World Translation of the Holy Scriptures—With References?
12 Sawa na vile mwana-migodi huwa na vyombo vya kazi yake, ndivyo sisi tulivyo na vyombo vya kazi ya kuchimba mgodi wa dhahabu ya Neno la Mungu. Kwa kielelezo, fikiria New World Translation of the Holy Scriptures—With References. Kwa wakati uliopo imetangazwa kwa chapa katika Kiholanzi, Kiingereza, Kifaransa, Kijeremani, Kiitalia, Kijapani, Kireno, na Kihispania. Kwa hiyo, walio wengi wa Mashahidi wa Yehova wana chombo kizuri sana cha kupatia maarifa sahihi kuhusu yule Mungu wa kweli. Chapa hii ya Biblia iliyohaririwa yahusisha ndani maelfu ya marejezo ya pambizoni na wingi mkubwa wa vielezi vya chini. Pia ina nyongeza yenye kurasa 36 ikiwa na habari zenye maelezo mengi madogo-madogo kuhusu unamna-namna wa maswali ya Biblia yaliyo ya maana.b
13. Ni mambo gani ya kupendeza ambayo yanatokezwa kuhusiana na utumizi wa “maarifa” na “maarifa sahihi” katika Maandiko ya Kiebrania na Maandiko ya Kigiriki?
13 Nyuma, Reference Bible ina orodha ya “Maneno ya Biblia Yaliyofahirishwa” yakiwa ni yale yenye umaana mkubwa zaidi. Twaweza kuyatumiaje? Katika nakala yako ukichunguza ule usemi “maarifa sahihi,” utapata maandiko kumi yakiwa yameorodheshwa. Lakini lolote la hayo halimo katika Maandiko ya Kiebrania. Je! hiyo yamaanisha kwamba Maandiko ya Kiebrania hayakazii uhitaji wa maarifa hayo? Sivyo. Kwa maana chini ya neno “maarifa,” kuna marejezo 24, kutia ndani 18 kutokana na Maandiko ya Kiebrania. Hata hivyo, lugha ya Kiebrania haina neno la pekee la kusema “maarifa sahihi.” Kwa hiyo, kama utakavyoona kutokana na marejezo yale, nyakati fulani lugha hiyo hukazia uhitaji wa kuwa na maarifa yazidiyo yale ya ujumla tu kwa kuunganisha neno “maarifa” na maneno kama vile “utambuzi” na “muono-ndani” au kwa kunena juu ya maarifa yakiwa “mengi sana.”—Danieli 1:4; 12:4; Yeremia 3:15, NW.
14. Ni mambo gani makuu ya kupendeza yaliyo chini ya “maarifa” katika Insight on the Scriptures?
14 Kama vile tumejifunza katika makala iliyotangulia, Kigiriki cha Biblia kilitokeza tofauti nyembamba kati ya kadiri mbili hizo za maarifa. Tuchimbapo, twataka kujua mengi zaidi kuhusu tofauti kati ya semi mbili hizi kama zitumikavyo kwa Wakristo. Kwa nini maarifa, gno·sis, na maarifa sahihi, e·piʹgno·sis, yahitajiwa sana kwa Wakristo? Twaweza kupata jibu wapi? Katika ile ensaiklopedia ya Biblia Insight on the Scriptures. Lo, mabuku haya ni nyumba-hazina iliyoje! Tafuta kichwa “Maarifa.” Humo utapata makala kamili kuhusu mitajo ambayo tunaifikiria na kuhusu zile sifa za hekima, uelewevu, utambuzi, na uwezo wa kufikiri ambazo zahusiana nayo. Nasi tumeipata “dhahabu” yote hii, yaani habari hizi, kwa kutumia tu misaada michache ya kujifunzia Biblia! Lakini kuna mengi zaidi. —Zaburi 19:9, 10.
15. Ni vyombo gani vingine vya kazi ya utafiti tulivyo navyo, na vyaweza kutumiwaje?
15 Kama ungetaka kufuatia funzo lenye upekuzi mwingi zaidi kuhusu neno “maarifa” na mitajo yenye kuhusiana nalo, ungeweza kutumia Fahirisi za vichapo vya Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, ambazo zapatikana katika lugha kadhaa. Na sawa na vile sisi tumefuatilia kichwa hiki cha maarifa, wewe waweza kufuata utaratibu uo huo kwa mamia ya habari nyinginezo. Wazia utajiri wa habari zilizo chini ya jina Yehova! Ni wingi mkubwa kama nini wa maarifa sahihi uliopo kuhusu Bwana Mwenye Enzi Kuu wa ulimwengu wote mzima!—Zaburi 68:19, 20; Matendo 4:24, NW.
16. Maandiko yasema nini kuhusu kutafuta?
16 Tukiwa na misaada hii na mingineyo yenye kutangazwa kwa chapa na Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi Biblia na Trakti, lo! twaweza kupata “hazina zilizofichika” zilizo nzuri kama nini! Je! wewe waitaka “dhahabu”? Je! wafikiri yastahiki uipate? Je! utajifanyizia wakati wa kuichimba?—Mithali 2:15, NW.
Ni Nani Huongoza Katika Uchimbaji Migodi wa Kiroho?
17. Ni lazima tufanye nini ili kupata maarifa kuhusu Mungu na Kristo?
17 Ni nini ufunguo wa kupata maarifa haya yenye thamani kubwa kuhusu Mungu na Kristo? Ni kichocheo—hamu nyingi sana ya kuwa na msimamo wenye kukubalika pamoja na Yehova na Mwana wake na tamaa ya kupokea ile zawadi ya uhai wa milele. Yesu aliliweka hivi wazo hilo: “Endeleeni kuomba, nanyi mtapewa; endeleeni kutafuta, nanyi mtapata; endeleeni kubisha, nanyi mtafunguliwa. Kwa maana kila mmoja anayeomba hupokea, na kila mmoja anayetafuta hupata, na kila mmoja anayebisha atafunguliwa.” Lakini liangalie sharti lililowekwa. Yesu alisema, ‘Endeleeni kuomba, kutafuta, na kubisha.’ Hilo si jambo la kufanywa mara moja tu. Utafutaji wa maarifa ni lazima uwe wenye usisitivu.—Mathayo 5:6; 7:7, 8, NW.
18. Katika jamaa, ni nani apaswa kuongoza katika kutafuta maarifa sahihi, na kwa nini?
18 Katika jamaa ya Kikristo, ni nani ambaye lazima aongoze katika uchimbaji wa kutafuta maarifa sahihi? Paulo ajibu hivi: “Nyinyi, akina baba, msiwe mkiwaudhi watoto wenu, bali endeleeni kuwalea katika nidhamu na rekebisho la akilini la Yehova.” Naam, wazazi, hasa baba, ni lazima waongoze katika kuonyesha uthamini kwa thamani za maadili ya kiroho. Na hiyo yatukumbusha tena juu ya uhitaji wa kuwako mpango wa ukawaida ambao jamaa yaweza kutarajia na kutazamia.—Waefeso 6:4, NW.
19. Vipindi vya funzo la jamaa vyaweza kufanywaje vipendeze? Jamaa yako imejionea nini kuhusu jambo hili?
19 Vipindi vya funzo la jamaa vyaweza kufanywa vipendeze. Kwa kielelezo, ikiwa wewe una watoto, kwa nini usiwaache wao wachague kichwa cha habari fulani kisha uwagawie kufanya utafiti katika vichapo tofauti-tofauti kulingana na umri na uwezo wao. Halafu baada ya muda wa saa moja hivi, mje pamoja na kuona kila mmoja amegundua nini kuhusiana na habari aliyogawiwa. Ikiwa konkodansi ipo, kijana aweza kuhesabu ni mara ngapi neno fulani laonekana katika Maandiko ya Kiebrania na Maandiko ya Kigiriki. Labda mmoja aliye na umri mkubwa zaidi atapata johari fulani-fulani katika mabuku Insight. Wazazi wajua uwezo mbalimbali wa watoto wao na muda ambao wao waweza kudumisha fikira zao katika jambo moja na yawapasa wasitawishe kipindi hicho kwa kutegemea mambo hayo. Mwe wenye kupindikana na wenye uthamini. Tieni jamaa yenu moyo wa kufanya uchimbaji wa kiroho—na mwe na kusudio lifaalo.
Kuchimba kwa Kusudio Lifaalo
20. Ni kusudio gani la kimakosa ambalo twapaswa kuepuka katika funzo letu la kibinafsi?
20 Kiasi cha mtu katika kujikadiria ubora wake ni nguvu ya wema wa Kikristo. (Mithali 11:2; 1 Timotheo 2:9) Basi, je! yatupasa tuwe tukijifunza ili tuwe tukijisifia mambo ambayo tumejifunza? Au yatupasa tujionyeshe mbele ya watu kuhusu maarifa yetu na labda tuonyeshe wengine kuwa wasiojua kitu? Au je! yatupasa tupige mbiu ya fasiri au makisio-kisio yetu wenyewe? Paulo alishauri hivi: “Kutokana na neema [fadhili zisizostahiliwa, NW] aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.”—Warumi 12:3, HNWW.
21, 22. Maarifa sahihi tuliyo nayo yapasa kutuathirije?
21 Jitihada ya moyo wenye bidii na utumizi wa maarifa sahihi yaweza kuongoza kwenye imani, nguvu ya wema, kujidhibiti, uvumilivu, ujitoaji kimungu, shauku ya kidugu, na upendo. Petro alionyesha umaana wa mambo haya alipoandika hivi: “Kwa maana ikiwa mambo haya yamo ndani ya nyinyi na yafurika, hayo yatazuia nyinyi msiwe ama wasiotenda ama wasio na matunda kuhusiana na maarifa sahihi kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo.”—2 Petro 1:2-8, NW.
22 Maarifa yetu yapasa kuathiri moyo. Yapasa kutusukuma tuonyeshe upendo kwa Mungu na kwa jirani na kuwa Wakristo wenye mazao katika mwenendo na huduma yetu. Hiyo itatokeza umoja na uelewevu kamili zaidi wa kielelezo cha Kristo. (Waefeso 4:13) Lo, hiyo itakuwa thawabu nzuri kama nini ya kutafuta hazina zilizofichika!
[Maelezo ya Chini]
a Kwa kupendeza, kwenye Mithali 2:5 usemi “maarifa hususa kuhusu Mungu” waonekana katika Septuagint ya Kigiriki ukiwa e·piʹgno·sis, au “maarifa sahihi,” ambalo ni moja la matumizi manane ya neno hilo la Kigiriki katika Septuagint.
b Ili upate maelezo marefu juu ya jinsi ya kupata manufaa nyingi zaidi kutokana na Reference Bible, ona Mnara wa Mlinzi wa Novemba 1, 1985, kurasa 2730.
Maswali ya Kufikiriwa Sana
◻ Kulingana na Mfalme Sulemani, ni nini chenye thamani kubwa kuliko hazina zilizofichika?
◻ Kwa nini maarifa sahihi ni muhimu kwa wapakwa-mafuta na kwa kondoo wengine?
◻ Twaweza kununuaje wakati wa funzo la kibinafsi?
◻ Ni vyombo gani vya pekee tulivyo navyo kwa kazi ya kuchimba maarifa sahihi?
◻ Nani apaswa kuongoza katika funzo la jamaa, nasi twapaswa kujifunza tukiwa na kusudio gani?