SHERIA
“1. Sheria ni kanuni na masharti yanayotungwa na serikali na yanayopaswa kufuatwa na kikundi fulani cha watu, iwe yametungwa au yametokana na desturi na sera zinazotambuliwa na kuungwa mkono na uamuzi wa kihukumu. 2. Amri yoyote iliyoandikwa au inayofaa, au mkusanyo wa sheria zinazotolewa na mamlaka ya nchi au taifa.” (The American College Dictionary, iliyohaririwa na C. L. Barnhart, 1966) “Amri ya Mungu au kufunuliwa kwa mapenzi ya Mungu . . . amri za Mungu kwa ujumla au ufunuo wake: mapenzi ya Mungu . . . : sheria inayowezesha mtu kuishi kwa njia inayofaa au kuwa na mwenendo mzuri hasa inapopatana na mapenzi ya Mungu, dhamiri au maadili yanayofaa, au haki ya kiasili.”—Webster’s Third New International Dictionary, 1981.
Neno “sheria” katika Maandiko ya Kiebrania limetafsiriwa kutokana na neno toh·rahʹ la Kiebrania, linalohusiana na kitenzi ya·rahʹ, kinachomaanisha “kuelekeza, kufundisha, kuagiza.” Nyakati nyingine linatafsiriwa kutokana na neno dath la Kiaramu. (Da 6:5, 8, 15) Maneno mengine yaliyotafsiriwa kuwa “sheria” katika King James Version ni mish·patʹ (maamuzi ya hukumu, hukumu), na mits·wahʹ (amri). Katika Maandiko ya Kigiriki neno noʹmos, linalotokana na kitenzi neʹmo (kutoa, kugawa), linatafsiriwa kuwa “sheria.”
Yehova Mungu anarejelewa kuwa Chanzo cha sheria, Mpaji-Sheria Mkuu (Isa 33:22), Mwenye Enzi Kuu, anayetoa mamlaka (Zb 73:28; Yer 50:25; Lu 2:29; Mdo 4:24; Ufu 6:10), na hakuna yeyote anayeweza kuwa na mamlaka bila ruhusa au idhini yake. (Ro 13:1; Da 4:35; Mdo 17:24-31) Msingi wa kiti chake cha ufalme ni uadilifu na haki. (Zb 97:1, 2) Mapenzi ya Mungu yanakuwa sheria kwa viumbe wake.—Ona KESI.
Sheria Waliyopewa Malaika. Malaika, ambao ni viumbe wa hali ya juu kuliko wanadamu, wanapaswa kutii sheria na amri za Mungu. (Ebr 1:7, 14; Zb 104:4) Yehova hata alimwamuru na kumzuia Shetani ambaye ni mpinzani wake. (Ayu 1:12; 2:6) Mikaeli yule malaika mkuu alipotofautiana na Ibilisi alitambua na kuheshimu cheo cha Yehova akiwa Hakimu Mkuu aliposema hivi: “Yehova na akukemee.” (Yuda 9; linganisha na Zek 3:2.) Yehova Mungu amempa Yesu Kristo aliyetukuzwa mamlaka ya kusimamia malaika wote. (Ebr 1:6; 1Pe 3:22; Mt 13:41; 25:31; Flp 2:9-11) Kwa hiyo, malaika alitumwa kwa Yohana kwa amri ya Yesu. (Ufu 1:1) Isitoshe, katika 1 Wakorintho 6:3 mtume Paulo anasema kwamba ndugu wa kiroho wa Kristo watawahukumu malaika, kwa sababu watashiriki kwa njia fulani kutekeleza hukumu dhidi ya roho waovu.
Sheria ya Uumbaji wa Mungu. Maana moja ya neno sheria katika kamusi ya Webster’s Third New International Dictionary ni “ukawaida unaoonekana katika uumbaji.” Akiwa Muumba wa vitu vyote mbinguni na duniani (Mdo 4:24; Ufu 4:11), Yehova ameweka sheria zinazoongoza uumbaji wote. Andiko la Ayubu 38:10 linasema kwamba bahari imewekewa “mpaka”; Ayubu 38:12 linataja kuhusu “kuiamuru asubuhi”; na Ayubu 38:31-33 linaelekeza fikira kwa makundi ya nyota na kwa “sheria zinazoongoza mbingu.” Sura hiyohiyo inasema kwamba Mungu anaongoza nuru, theluji, mvua ya mawe, mawingu, mvua, umande, na radi. Sura ya 39 hadi 41 zinaonyesha jinsi Mungu anavyowajali wanyama, na jinsi sheria zake zinavyowaongoza wanyama kuhusiana na kuzaa, maisha yao, na tabia zao, mambo ambayo hayategemei “mabadiliko” yoyote ya mageuzi. Mambo hayo hayangetokea kamwe kwa mageuzi kwa sababu Mungu alipoumba aliweka sheria ya kwamba kila kitu kizae “kulingana na aina zake.” (Mwa 1:11, 12, 21, 24, 25) Mwanadamu pia alizaa wana “kwa mfano wake, kwa sura yake.” (Mwa 5:3) Zaburi 139:13-16 inazungumzia ukuzi wa mtoto ndani ya tumbo la mama yake, inasema kwamba sehemu zake ziliandikwa “katika kitabu [cha Yehova]” kabla sehemu yoyote haijakuwepo. Andiko la Ayubu 26:7 linasema Yehova “ameining’iniza dunia mahali pasipo na kitu.” Leo wanasayansi wanasema kwamba dunia inakaa mahali pake angani hasa kwa sababu ya nguvu za uvutano na nguvu zinazoivuta nje.
Sheria Aliyopewa Adamu. Katika bustani ya Edeni, Mungu aliwapa Adamu na Hawa maagizo kuhusu majukumu yao ya (1) kuijaza dunia, (2) kuitiisha, na (3) kutawala viumbe wengine wote walio hai duniani, baharini, na angani. (Mwa 1:28) Walipewa sheria kuhusu chakula, wangekula mimea yote inayozaa mbegu na matunda. (Mwa 1:29; 2:16) Hata hivyo, Adamu aliamriwa asile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwa 2:17); kisha akamwambia Hawa amri hiyo. (Mwa 3:2, 3) Adamu anaitwa mkosaji kwa sababu alivunja sheria.—Ro 5:14, 17; 4:15.
Sheria Alizopewa Noa; Sheria ya Wazee wa Ukoo. Noa alipewa maagizo kuhusu kujenga safina na kuokoa familia yake. (Mwa 6:22) Baada ya Gharika alipewa sheria zilizowaruhusu kula nyama; zilizoonyesha utakatifu wa uhai na wa damu, kwa kuwa uhai umo ndani yake; zilizokataza kula damu; zilizoshutumu kuua; na kutoa hukumu ya kifo kwa yeyote aliyemuua mwingine.—Mwa 9:3-6.
Mzee wa ukoo alikuwa kichwa cha familia na pia mtawala. Yehova ndiye Kichwa cha Familia aliye mkuu zaidi, au Mzee wa Ukoo, “Baba . . . ambaye kila familia mbinguni na duniani hupata jina kutoka kwake.” (Efe 3:14, 15) Noa, Abrahamu, Isaka, na Yakobo ni wazee wa ukoo walioweka vielelezo bora. Yehova alishughulika nao kwa njia ya pekee sana. Abrahamu aliamriwa awatahiri wanaume wote wa nyumba yake kama ishara ya agano alilofanya na Mungu. (Mwa 17:11, 12) Alitii “amri,” “maagizo,” na “sheria” za Yehova. Alijua jinsi Yehova anavyotenda uadilifu na kuhukumu, naye aliwafundisha watu wa nyumba yake amri hizo.—Mwa 26:4, 5; 18:19.
Kwa ujumla, sheria zilizowaongoza wazee hao wa ukoo zilieleweka na baadhi yake zilifuatwa na mataifa yaliyokuwepo wakati huo, na mataifa hayo yote yalitokana na wana watatu wa mzee wa ukoo, Noa. Kwa mfano, kuhusiana na Sara na Rebeka, Farao wa Misri alijua kwamba ni kosa kumchukua mke wa mtu mwingine, hata wafalme Wafilisti walijua hivyo.—Mwa 12:14-20; 20:2-6; 26:7-11.
Katika siku za Musa, Waisraeli walikuwa watumwa nchini Misri. Walienda Misri kwa hiari katika siku za Yakobo lakini wakafanywa watumwa baada ya kifo cha Yosefu, mwana wa Yakobo aliyekuwa waziri mkuu. Kwa hiyo, waliuzwa utumwani bure. Kupatana na sheria ya wazee wa ukoo kuhusu ukombozi na kuhusu mzaliwa wa kwanza, Yehova alimwambia hivi Farao kupitia Musa na Haruni: “Israeli ni mwanangu, mzaliwa wangu wa kwanza. Ninakwambia, Mruhusu mwanangu aondoke ili anitumikie. Lakini ukikataa kumruhusu aondoke, nitamuua mwana wako, mzaliwa wako wa kwanza.” (Kut 4:22, 23) Hakuna bei ya ukombozi iliyohitajiwa ili kuwaachilia huru, Misri haikulipwa chochote. Waisraeli walipoondoka utumwani, Misri, ‘Yehova aliwafanya watu hao wapate kibali machoni pa Wamisri, hivi kwamba wakawapa walichoomba; nao wakachukua mali za Wamisri.’ (Kut 3:21; 12:36) Farao alikuwa amewaruhusu waingie Misri, si kama mateka wa vita, bali watu huru. Utumwa huo haukuwa wa haki, basi ni wazi kwamba Yehova alihakikisha wanalipwa kwa ajili ya kazi yao ngumu.
Familia ililaumiwa ikiwa mshiriki mmoja aliasi sheria. Kichwa cha familia ndiye aliyekuwa mwakilishi; alilaumiwa kwa sababu ya makosa ya familia yake na alikuwa na wajibu wa kumwadhibu mkosaji katika familia.—Mwa 31:30-32.
Ndoa na haki ya kuzaliwa. Wazazi waliongoza mpango wa ndoa wa wana na binti zao. (Mwa 24:1-4) Kwa kawaida mahari ililipwa. (Mwa 34:11, 12) Waabudu wa Yehova waliofunga ndoa na waabudu sanamu walikosa kutii nao waliiumiza familia yao.—Mwa 26:34, 35; 27:46; 28:1, 6-9.
Haki ya kuzaliwa ilikuwa ya mzaliwa wa kwanza, alirithi haki hiyo. Angerithi sehemu mbili za mali. Hata hivyo, baba, akiwa kichwa cha familia, angeweza kumpa mwingine haki hiyo. (Mwa 48:22; 1Nya 5:1) Kwa kawaida baada ya baba kufa mwana wa kwanza alichukua nafasi yake na kuwa kichwa cha familia. Baada ya kuoa, wana wangeanzisha familia zao wenyewe na kuwa vichwa vya familia hizo badala ya baba yao.
Maadili. Uasherati ulileta aibu na mwasherati aliadhibiwa, hasa ikiwa alikuwa katika uchumba au katika ndoa (uzinzi). (Mwa 38:24-26; 34:7) Ndoa za ndugu mkwe ziliruhusiwa ikiwa mwanamume alikufa bila kupata mwana. Ndugu yake alikuwa na daraka la kumwoa mjane aliyeachwa, na mwana wa kwanza waliyemzaa angerithi mali ya mwanamume aliyekufa na kuendeleza jina lake.—Kum 25:5, 6; Mwa 38:6-26.
Mali. Kwa ujumla, inaonekana mtu binafsi hangemiliki mali yake mwenyewe isipokuwa vitu vichache vya kibinafsi; kwa kuwa mifugo yote, vitu vya nyumbani, na vifaa vingine vilimilikiwa na familia.—Mwa 31:14-16.
Kulingana na uthibitisho wa kihistoria, wasomi fulani wanaamini kwamba, wakati wa kuuza ardhi, mnunuzi angeonyeshwa ardhi kutoka umbali fulani, na kuonyeshwa mipaka yake. Ikiwa mnunuzi angesema “Nimeona,” ingemaanisha amekubali kisheria. Yehova alipomwahidi Abrahamu kwamba atampa nchi ya Kanaani, Abrahamu aliambiwa kwanza aangalie pande zote nne. Abrahamu hakusema, “Nimeona,” huenda kwa sababu Mungu alimwambia kwamba angeupa uzao wa Abrahamu Nchi ya Ahadi baadaye. (Mwa 13:14, 15) Ikiwa maoni yaliyotolewa hapo juu ni sahihi, basi Musa, akiwa mwakilishi wa kisheria wa taifa la Israeli, aliambiwa ‘aone’ nchi, jambo ambalo lingemaanisha kwamba nchi hiyo sasa ilikuwa mali ya Israeli kisheria, na wangeimiliki chini ya uongozi wa Yoshua. (Kum 3:27, 28; 34:4; ona pia maneno ambayo Shetani alimwambia Yesu katika Mt 4:8.) Tendo lingine ambalo inaonekana lilikuwa na maana hiyohiyo ya kisheria ni: kutembea katika nchi na kuivuka au kuingia ndani yake ili kuimiliki. (Mwa 13:17; 28:13) Kwenye hati fulani za kale, idadi ya miti katika shamba ilitajwa kwenye hati ya ununuzi.—Linganisha na Mwa 23:17, 18.
Utunzaji. Mtu aliyeahidi kutunza au ‘kulinda’ mtu, mnyama, au kitu fulani alikuwa na wajibu wa kisheria. (Mwa 30:31) Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo aliwajibika Yosefu alipopotea. (Mwa 37:21, 22, 29, 30) Mtunzaji alipaswa kukitunza vizuri kitu kilichokuwa chini ya ulinzi wake. Alipaswa kulipia wanyama walioibwa, lakini si wanyama waliokufa wenyewe au waliopotea kwa sababu ya hali zisizoepukika, kwa mfano wanyama walioibwa na waporaji wenye silaha. Ikiwa mnyama wa mwituni alimuua mnyama wa kufugwa, mchungaji alipaswa kutoa uthibitisho ili kujiondolea lawama.—Mwa 37:12-30, 32, 33; Kut 22:10-13.
Utumwa. Watumwa wangenunuliwa au kuzaliwa na wazazi waliokuwa watumwa. (Mwa 17:12, 27) Watumwa wangepewa cheo chenye kuheshimiwa sana katika nyumba ya ukoo, kama alichopewa Eliezeri, mtumishi wa Abrahamu.—Mwa 15:2; 24:1-4.
Sheria Ambayo Mungu Aliwapa Waisraeli—Sheria ya Musa. Mwaka wa 1513 K.W.K., Yehova aliwapa Waisraeli Sheria katika Nyika ya Sinai kupitia Musa akiwa mpatanishi wao. Sheria ilipoanzishwa rasmi kwenye Mlima Horebu, Yehova alidhihirisha nguvu zake kwa njia ya kustaajabisha. (Kut 19:16-19; 20:18-21; Ebr 12:18-21, 25, 26) Agano hilo lilihalalishwa kwa damu ya ng’ombe dume na mbuzi. Watu walitoa dhabihu za ushirika, wakasikiliza kitabu cha agano kikisomwa, kisha wakakubali kutii maneno yote ambayo Yehova alisema. Sheria aliyopewa Musa ilitia ndani sheria nyingi ambazo wazee wa ukoo walipewa.—Kut 24:3-8; Ebr 9:15-21; ona AGANO.
Kwa kawaida vitabu vitano vya kwanza vya Biblia (Mwanzo hadi Kumbukumbu la Torati) huitwa Sheria. Nyakati nyingine neno hilo hutumiwa kurejelea Maandiko yote ya Kiebrania yaliyoongozwa na roho takatifu. Hata hivyo, kwa ujumla Wayahudi waligawanya Maandiko yote ya Kiebrania katika sehemu tatu, “Sheria ya Musa,” “Manabii,” na “Zaburi.” (Lu 24:44) Waisraeli walikuwa na wajibu wa kutii amri zote zilizotolewa na manabii.
Sheria ilimtambulisha Yehova kwa njia ya pekee kuwa Mwenye Enzi Kuu aliye na mamlaka kamili na pia Mfalme. Kwa kuwa Yehova alikuwa Mungu na Mfalme wa Israeli, kuvunja Sheria kulikuwa kosa la kidini na la uhaini pia, kosa dhidi ya Kiongozi wa Taifa, ambaye katika kisa hiki alikuwa Mfalme Yehova. Maandiko yalisema kwamba Daudi, Sulemani, na wafalme wengine wa Yuda waliotawala baada yao waliketi kwenye “kiti cha ufalme cha Yehova.” (1Nya 29:23) Wafalme wa kibinadamu na watawala wa Israeli walipaswa kutii Sheria, na walipotawala kimabavu, waliasi sheria na kuwajibika mbele za Mungu. (1Sa 15:22, 23) Ufalme na ukuhani ulitenganishwa, jambo ambalo lilisawazisha mamlaka na kuzuia ukandamizaji. Liliwakumbusha daima Waisraeli kwamba Yehova ndiye Mungu wao na Mfalme wao. Sheria ilitoa maagizo kuhusu uhusiano ambao kila mtu alipaswa kuwa nao pamoja na Mungu na pamoja na mwanadamu mwenzake, na kila mtu angeweza kumfikia Mungu kupitia mpango wa ukuhani.
Sheria iliwapa Waisraeli fursa ya kuwa “ufalme wa makuhani na taifa takatifu.” (Kut 19:5, 6) Matakwa ya Sheria yaliyotia ndani kumwabudu Yehova peke yake, kutoshirikiana kamwe na dini nyingine, na masharti kuhusu usafi wa ibada na vyakula, yalikuwa “ukuta” uliofanya taifa hilo liwe tofauti kabisa na mataifa mengine. (Efe 2:14) Myahudi aliyeingia katika hema la Mtu Asiye Myahudi au nyumba yake au kula chakula pamoja na watu hao alikuwa najisi kiroho. Hata Yesu alipokuwa duniani, Myahudi aliyeingia katika nyumba ya Mtu Asiye Myahudi alionwa kuwa najisi. (Yoh 18:28; Mdo 10:28) Sheria ililinda utakatifu wa uhai na heshima katika familia, ndoa, na mtu mmoja-mmoja. Mbali na faida za kiroho walizopata kwa kutii agano la Sheria na kujitenga kidini, Waisraeli walipata pia faida nyingine kutia ndani faida za kiafya na kulindwa kutokana na magonjwa yaliyoenea katika mataifa jirani. Bila shaka walinufaika sana walipotii sheria zilizohusu usafi wa maadili, usafi wa kimwili, na vyakula.
Lakini kama mtume Paulo alivyosema, Sheria ilikusudiwa hasa “kufanya makosa yawe wazi, mpaka ufike ule uzao.” Ilikuwa ‘mtunzaji ikiongoza kwa Kristo.’ Ilielekeza kwa Kristo (“Kristo ndiye mwisho wa Sheria”). Ilifunua kwamba wanadamu wote, kutia ndani Wayahudi, walikuwa chini ya dhambi na kwamba mtu hawezi kupata uzima kupitia “matendo ya sheria.” (Ga 3:19-24; Ro 3:20; 10:4) Ilikuwa ya “kiroho,” kutoka kwa Mungu, na “takatifu.” (Ro 7:12, 14) Katika Waefeso 2:15 inaitwa “ile Sheria iliyokuwa na amri na maagizo.” Ilikuwa kiwango cha ukamilifu, na yeyote aliyeweza kuishika angeonwa kuwa mkamilifu, anayestahili uzima. (Law 18:5; Ga 3:12) Kwa kuwa wanadamu wasio wakamilifu walishindwa kushika Sheria, ni wazi kwamba “wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Ro 3:23) Yesu Kristo peke yake ndiye aliyeishika bila lawama.—Yoh 8:46; Ebr 7:26.
Pia, Sheria ilikuwa “kivuli cha mambo mema yatakayokuja,” na mambo yaliyohusiana nayo yalikuwa “mifano ya uhalisi,” ndiyo sababu Yesu na mitume waliirejelea mara nyingi walipofafanua vitu na mambo ya mbinguni yanayohusu mafundisho na mwenendo wa Mkristo. Basi, ni muhimu sana kwa Mkristo kujifunza kuihusu.—Ebr 10:1; 9:23.
Yesu alisema kwamba Sheria yote ilitegemea amri mbili, kumpenda Mungu na kumpenda jirani. (Mt 22:35-40) Ni jambo la pekee kwamba maneno ya Kiebrania yanayotafsiriwa kuwa “upendo,” “kupendwa,” na mengine, yametumiwa zaidi ya mara 20 katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati (ambapo Sheria ilirekebishwa kidogo ili kuwaongoza Waisraeli waliokuwa na maisha mapya baada ya kuingia katika Nchi ya Ahadi).
Yale Maneno Kumi (Kut 34:28), au Amri Kumi, yalikuwa sehemu ya msingi ya Sheria lakini sheria nyingine 600 ziliongezwa, na Waisraeli walipaswa kuzitii zote. (Yak 2:10) Amri nne za kwanza kati ya zile Amri Kumi zilifafanua uhusiano wa mtu na Mungu; ya tano, uhusiano na Mungu na uhusiano na wazazi; na zile tano za mwisho, zilifafanua uhusiano kati ya mtu na jirani yake. Amri tano za mwisho ziliorodheshwa kulingana na ukubwa wa madhara kwa mtu mwingine: kuua, uzinzi, kuiba, kutoa ushahidi wa uwongo, na kutamani au tamaa zenye ubinafsi. Amri ya kumi inafanya Sheria hiyo iwe ya kipekee ikilinganishwa na sheria za mataifa mengine yote kwa sababu ilikataza tamaa zenye ubinafsi, amri ambayo ni Mungu tu angeweza kujua ikiwa mtu ameivunja. Ililenga hasa chanzo cha uvunjaji wa amri nyingine zote.—Kut 20:2-17; Kum 5:6-21; linganisha na Efe 5:5; Kol 3:5; Yak 1:14, 15; 1Yo 2:15-17.
Sheria ilikuwa na kanuni na maagizo mengi. Waamuzi waliruhusiwa kufanya uchunguzi na kuelewa nia na mitazamo ya wakosaji, na pia hali zilizowachochea kuvunja sheria. Ikiwa mtu angevunja sheria kimakusudi, kwa dharau, au kukosa kutubu, angeuawa. (Hes 15:30, 31) Katika visa vingine hukumu haikuwa kali sana. Kwa mfano, muuaji wa kukusudia aliuawa, lakini mtu aliyeua bila kukusudia alionyeshwa rehema. (Hes 35:15, 16) Mwenye ng’ombe dume aliyezoea kuwapiga watu pembe na aliyeua mtu, angeuawa; au waamuzi wangemdai fidia. (Kut 21:29-32) Mwizi aliyeiba kimakusudia na mkosaji aliyetubu kwa hiari walipata adhabu tofauti kama inavyoonyeshwa katika Kutoka 22:7 na Mambo ya Walawi 6:1-7.
Sheria ya Dhamiri. Biblia inaonyesha watu wana dhamiri kwa sababu ‘sheria imeandikwa ndani ya mioyo yao.’ Wale ambao hawako chini ya sheria iliyotoka kwa Mungu moja kwa moja, kama Sheria aliyopewa Musa, “wao ni sheria kwao wenyewe,” kwa sababu dhamiri zao ‘zinawashtaki au kuwatetea’ katika fikira zao wenyewe. (Ro 2:14, 15) Sheria nyingi zenye haki katika jamii za kipagani zinaonyesha walikuwa na dhamiri, ambayo iliwekwa mwanzoni ndani ya babu yao Adamu na kurithiwa kupitia Noa.—Ona DHAMIRI.
Katika 1 Wakorintho 8:7, mtume Paulo anasema kwamba mtu asipokuwa na ujuzi sahihi wa Kikristo dhamiri yake inaweza kuwa dhaifu. Dhamiri inaweza kumwongoza mtu vizuri au vibaya ikitegemea ujuzi na mazoezi. (1Ti 1:5; Ebr 5:14) Dhamiri inaweza kuchafuliwa na hivyo kumwongoza mtu vibaya. (Tit 1:15) Wengine wamepuuza dhamiri zao tena na tena hivi kwamba zimekufa ganzi kama kovu, kwa hiyo haziwaongozi inavyofaa.—1Ti 4:1, 2.
“Sheria ya Kristo.” Paulo aliandika hivi: “Endeleeni kubebeana mizigo mizito, na hivyo mtaitimiza sheria ya Kristo.” (Gal 6:2) Agano la Sheria lilikomeshwa Pentekoste mwaka wa 33 W.K., (“kwa kuwa ukuhani unabadilishwa, inakuwa muhimu kubadilisha Sheria pia”; Ebr 7:12), sasa Wakristo wako “chini ya sheria kwa Kristo.” (1Ko 9:21) Sheria hiyo inaitwa “sheria kamilifu ambayo ni ya uhuru,” “sheria ya watu huru,” “sheria ya imani.” (Yak 1:25; 2:12; Ro 3:27) Mungu alikuwa ametabiri kuhusu sheria hiyo mpya kupitia nabii Yeremia alipozungumzia agano jipya na kusema kwamba sheria yake ingeandikwa katika mioyo ya watu wake.—Yer 31:31-34; Ebr 8:6-13.
Musa alikuwa mpatanishi wa agano la Sheria, naye Yesu Kristo ndiye Mpatanishi wa agano jipya. Musa aliandika orodha ya Sheria, lakini Yesu hakuandika kihalisi sheria. Alipozungumza alitia sheria yake katika akili na mioyo ya wanafunzi wake. Pia wanafunzi wake hawakuwaandikia Wakristo orodha ya sheria zilizopangwa katika makundi na vichwa vikuu. Hata hivyo, Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo yamejaa sheria, maagizo, na amri ambazo Mkristo anapaswa kufuata.—Ufu 14:12; 1Yoh 5:2, 3; 4:21; 3:22-24; 2Yo 4-6; Yoh 13:34, 35; 14:15; 15:14.
Yesu aliwaamuru wanafunzi wake wahubiri ‘habari njema ya ufalme.’ Amri hiyo inapatikana katika Mathayo 10:1-42; Luka 9:1-6; 10:1-12. Katika Mathayo 28:18-20 wanafunzi wa Yesu walipewa amri mpya ya kwenda, si kwa Wayahudi tu, bali kwa mataifa yote, ili kufanya wanafunzi na kuwabatiza kwa ubatizo mpya, ‘katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu, na kuwafundisha kushika mambo yote aliyowaamuru.’ Kwa hiyo, akiwa na mamlaka aliyopewa na Mungu, Yesu alifundisha na kutoa amri alipokuwa duniani (Mdo 1:1, 2) na pia baada ya kurudi mbinguni. (Mdo 9:5, 6; Ufu 1:1-3) Kitabu chote cha Ufunuo kimejaa unabii, amri, maonyo, na maagizo kwa ajili ya kutaniko la Kikristo.
“Sheria ya Kristo” inahusu sehemu zote za maisha na kazi ya Mkristo. Kwa msaada wa roho ya Mungu Mkristo anaweza kutii amri hizo ili apate hukumu ifaayo kwa msingi wa sheria hiyo, kwa sababu ni “sheria ya roho ambayo hutokeza uzima katika muungano na Kristo Yesu.”—Ro 8:2, 4.
“Sheria ya Mungu.” Mtume Paulo anasema kwamba kuna mambo mawili yanayohusika katika vita vya Mkristo, kuna “sheria ya Mungu,” au “sheria ya roho ambayo hutokeza uzima” na pia kuna “sheria ya dhambi,” au “sheria ya dhambi na kifo.” Paulo anafafanua pigano hilo anaposema kwamba mwili wenye dhambi ni mtumwa wa “sheria ya dhambi.” “Kukaza akili kwenye mwili humaanisha kifo,” lakini ‘Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe akiwa katika mfano wa mwili wenye dhambi na kuhusu dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.’ Kwa msaada wa roho ya Mungu, Mkristo anaweza kushinda pigano hilo—kwa kumwamini Kristo, kuua mazoea ya mwili, na kuishi kupatana na mwongozo wa roho—na kisha kupata uzima.—Ro 7:21-8:13.
Sheria ya Dhambi na Kifo. Mtume Paulo anasema kwamba, kwa sababu ya dhambi ya baba wa wanadamu wote Adamu, “kifo kilitawala kama mfalme” tangu wakati wa Adamu mpaka siku za Musa (walipopewa Sheria) na kwamba Sheria ilifanya makosa yawe wazi, na kuwafanya wanadamu wawe na hatia ya dhambi. (Ro 5:12-14; Ga 3:19) Amri hiyo, au sheria hiyo ya dhambi, inapofanya kazi ndani ya mwili usio mkamilifu inakuwa na nguvu sana, hivi kwamba inauelekeza uvunje sheria ya Mungu. (Ro 7:23; Mwa 8:21) Dhambi husababisha kifo. (Ro 6:23; 1Ko 15:56) Sheria ya Musa haingeweza kushinda utawala wa mfalme dhambi na mfalme kifo, lakini uhuru na ushindi unapatikana kwa fadhili zisizostahiliwa za Mungu kupitia Yesu Kristo.—Ro 5:20, 21; 6:14; 7:8, 9, 24, 25.
“Sheria ya Imani.” “Sheria ya imani” inatofautiana na “ile ya matendo.” Mtu hawezi kuwa mwadilifu kwa kazi zake mwenyewe au matendo ya Sheria ya Musa, kana kwamba anapata uadilifu kwa sababu ya kazi zake, lakini mtu huwa mwadilifu kupitia imani katika Yesu Kristo. (Ro 3:27, 28; 4:4, 5; 9:30-32) Hata hivyo, Yakobo anasema kwamba imani hiyo huonyeshwa kwa matendo yanayotokana na imani na yanayopatana nayo.—Yak 2:17-26.
Sheria ya Mume. Mwanamke aliyeolewa yuko chini ya “sheria ya mume wake.” (Ro 7:2; 1Ko 7:39) Kanuni ya ukichwa wa mume inatumika katika tengenezo lote la Mungu, nayo imekuwa ikifuatwa na wote wanaomwabudu Mungu na pia watu wengine wengi. Mungu ni kama mume wa “mwanamke” wake, “Yerusalemu la juu.” (Ga 4:26, 31; Ufu 12:1, 4-6, 13-17) Taifa la Wayahudi lilikuwa kama mke na Yehova alikuwa mume wake.—Isa 54:5, 6; Yer 31:32.
Sheria ya wazee wa ukoo ilionyesha wazi kwamba mume ndiye kichwa cha familia, mke alijitiisha chini yake, ingawa angeweza kutoa mapendekezo ambayo mume angeyaidhinisha. (Mwa 21:8-14) Sara alimwita Abrahamu “bwana.” (Mwa 18:12; 1Pe 3:5, 6) Mwanamke alijifunika kitambaa kichwani kama ishara ya kujitiisha chini ya ukichwa wa mume wake.—Mwa 24:65; 1Ko 11:5.
Katika Sheria waliyopewa Waisraeli, mke alijitiisha chini ya mume wake. Mume wake angeweza kuidhinisha au kufuta nadhiri alizoweka. (Hes 30:6-16) Hakurithi ardhi, badala yake alichukuliwa pamoja na ardhi ya urithi, na ikiwa urithi ungekombolewa na mtu wa karibu wa ukoo, yeye pia alichukuliwa. (Ru 4:5, 9-11) Hangeweza kumtaliki mume wake, lakini mume alikuwa na haki ya kumtaliki mke wake.—Kum 24:1-4.
Katika mpango wa Kikristo, mwanamke anapaswa kutambua cheo cha mwanamume, naye asijaribu kukinyakua. Mtume Paulo anasema kwamba mwanamke aliyeolewa yuko chini ya sheria ya mume wake maadamu mume wake yuko hai, lakini mwanamke anakuwa huru mume wake akifa, hivi kwamba akiolewa tena yeye si mzinzi.—Ro 7:2, 3; 1Ko 7:39.
“Sheria ya Kifalme.” Kama vile mfalme alivyo mkuu kati ya watu, “sheria ya kifalme” ni muhimu kuliko sheria nyingine zinazoongoza mahusiano ya wanadamu. (Yak 2:8) Jambo kuu katika agano la Sheria lilikuwa upendo; “lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe” (sheria ya kifalme) ilikuwa amri ya pili kati ya amri ambazo Sheria yote na Manabii hutegemea. (Mt 22:37-40) Ingawa Wakristo hawako chini ya agano la Sheria, wako chini ya sheria ya Mfalme Yehova na Mwanaye, Mfalme Yesu Kristo, kuhusiana na agano jipya.
[Sanduku kwenye ukurasa wa 214-220]
BAADHI YA MAMBO YALIYOKUWA KATIKA AGANO LA SHERIA
SERIKALI YA KITHEOKRASI
Yehova Mungu ndiye Mwenye Enzi Kuu (Kut 19:5; 1Sa 12:12; Isa 33:22)
Mfalme aliketi kwenye “kiti cha ufalme cha Yehova,” akimwakilisha (1Nya 29:23; Kum 17:14, 15)
Maofisa wengine (viongozi wa makabila; wakuu wa maelfu, wa mamia, wa hamsini, na wa makumi) walichaguliwa kwa msingi wa kumwogopa Mungu, kutegemeka, na kuchukia faida isiyo ya haki (Kut 18:21, 25; Hes 1:44)
Wote waliopewa mamlaka na Mungu walipaswa kuheshimiwa: maofisa, makuhani, waamuzi, wazazi (Kut 20:12; 22:28; Kum 17:8-13)
WAJIBU WA KIDINI
(Wajibu huo ulitajwa katika amri kuu zaidi katika Sheria—kumpenda Yehova kwa moyo wote, akili yote, nafsi yote, na nguvu zote; Kum 6:5; 10:12; Mk 12:30)
Yehova peke yake ndiye aliyepaswa kuabudiwa (Kut 20:3; 22:20; Kum 5:7)
Upendo ndio unaopaswa kumchochea mtu awe na uhusiano pamoja na Mungu (Kum 6:5, 6; 10:12; 30:16)
Wote walipaswa kumwogopa Mungu ili wasikose kumtii (Kut 20:20; Kum 5:29)
Jina la Mungu halikupaswa kutumiwa kwa njia isiyofaa (Kut 20:7; Kum 5:11)
Wangewasiliana naye kwa njia aliyokubali tu (Hes 3:10; Law 10:1-3; 16:1)
Wote walipaswa kushika Sabato (Kut 20:8-11; 31:12-17)
Walikutana ili kuabudu (Kum 31:10-13)
Wanaume wote walipaswa kukusanyika mara tatu kwa mwaka: Pasaka na Sherehe ya Mikate Isiyo na Chachu, Sherehe ya Majuma, na Sherehe ya Vibanda (Kum 16:16; Law 23:1-43)
Mwanamume aliyepuuza kimakusudi kusherehekea Pasaka ‘aliuawa’ (Hes 9:13)
Kuunga mkono ukuhani
Walawi walipokea sehemu ya kumi ya mazao yote ya nchi kutoka kwa makabila mengine (Hes 18:21-24)
Walawi walipaswa kuwapa makuhani sehemu ya kumi ya vitu bora zaidi walivyopokea (Hes 18:25-29)
Kutoa dhabihu (Ebr 8:3-5; 10:5-10)
Dhabihu mbalimbali zilizotajwa katika Sheria: dhabihu za kuteketezwa zilizotolewa kwa ukawaida (Law sura ya 1; Hes sura ya 28), dhabihu za ushirika (Law sura ya 3; 19:5), dhabihu za dhambi (Law sura ya 4; Hes 15:22-29), dhabihu za hatia (Law 5:1–6:7), matoleo ya nafaka (Law sura ya 2), matoleo ya kinywaji (Hes 15:5, 10), matoleo ya kutikiswa (Law 23:10, 11, 15-17)
Mazoea ya dini ya uwongo yalikatazwa
Ibada ya sanamu (Kut 20:4-6; Kum 5:8-10)
Kuukata mwili kwa ajili ya mtu aliyekufa au kujitia alama ya chanjo (Law 19:28)
Kupanda mti ili uwe mti mtakatifu (Kum 16:21)
Kuleta nyumbani vitu vinavyochukiza, vilivyopaswa kuharibiwa (Kum 7:26)
Kuwachochea wengine wamwasi Yehova (Kum 13:5)
Kuunga mkono ibada ya uwongo (Kum 13:6-10; 17:2-7)
Kujiunga na ibada ya uwongo (Kum 13:12-16)
Kumtoa dhabihu mtoto kwa miungu ya uwongo (Law 18:21, 29)
Kuwasiliana na roho, uchawi (Kut 22:18; Law 20:27; Kum 18:9-14)
MAJUKUMU YA KUHANI
(Walawi waliwasaidia makuhani kutimiza majukumu yao; Hes 3:5-10)
Kufundisha Sheria ya Mungu (Kum 33:8, 10; Mal 2:7)
Kutumikia wakiwa waamuzi, wakiongozwa na sheria ya Mungu (Kum 17:8, 9; 19:16, 17)
Kutoa dhabihu kwa niaba ya watu (Law sura ya 1-7)
Kutumia Urimu na Thumimu kupata ushauri wa Mungu (Kut 28:30; Hes 27:18-21)
KUWA MSHIRIKI WA KUTANIKO LA ISRAELI
Washiriki wa kutaniko la Israeli hawakuwa tu wale waliozaliwa katika taifa hilo
Watu wa mataifa mengine wangejiunga nao katika ibada baada ya kutahiriwa
Wageni hao walipaswa kufuata masharti yote ya agano la Sheria (Law 24:22)
Masharti yaliyowazuia wengine kujiunga na kutaniko la Israeli
Mwanamume yeyote aliyehasiwa kwa kuminywa mapumbu au kukatwa uume hakuruhusiwa (Kum 23:1)
Mwanaharamu au mzao wake kufikia “kizazi cha kumi” hakuruhusiwa kujiunga na kutaniko (Kum 23:2)
Mwamoni au Mmoabu (inaonekana ni wanaume) hakuruhusiwa kamwe kujiunga na kutaniko, kwa kuwa hawakuwasaidia Waisraeli walipokuwa wakitoka Misri, waliwapinga (Kum 23:3-6)
Watoto wa “kizazi cha tatu” waliozaliwa na Wamisri wangejiunga na kutaniko (Kum 23:7, 8)
MFUMO WA KIHUKUMU [MAHAKAMA]
(Sheria kuhusu kesi zilikazia haki na rehema ya Yehova. Waamuzi waliruhusiwa kuonyesha rehema, ikitegemea hali. Pia, sheria hizo zilizuia taifa hilo lisichafuliwe na zililinda masilahi ya kila Mwisraeli)
Waamuzi
Makuhani, wafalme, na wanaume wengine waliwekwa kuwa waamuzi (Kut 18:25, 26; Kum 16:18; 17:8, 9; 1Fa 3:6, 9-12; 2Nya 19:5)
Kusimama mbele ya waamuzi kulikuwa sawa na kusimama mbele za Yehova (Kum 1:17; 19:16, 17)
Kusikiliza kesi
Kesi za kawaida ziliwasilishwa kwa waamuzi (Kut 18:21, 22; Kum 25:1, 2; 2Nya 19:8-10)
Ikiwa mahakama ya chini ingeshindwa kufanya uamuzi, kesi hiyo ilipelekwa kwenye mahakama za juu zaidi (Kut 18:25, 26; 1Fa 3:16, 28)
Kesi za pekee au ngumu zilizopelekwa kwa makuhani:
Kesi zinazohusu wivu au mke kutokuwa mwaminifu (Hes 5:12-15)
Ikiwa shahidi alimshtaki mwingine kwa kosa fulani (Kum 19:16, 17)
Ikiwa mtu alimtendea mwingine kikatili au kumuua, au ilipokuwa vigumu kufanya uamuzi au kufikia makubaliano (Kum 17:8, 9; 21:5)
Mtu alipopatikana ameuawa uwanjani na haijulikani ni nani aliyemuua (Kum 21:1-9)
Mashahidi
Angalau mashahidi wawili walihitajiwa ili kuthibitisha ukweli (Kum 17:6; 19:15; linganisha na Yoh 8:17; 1Ti 5:19)
Mikono ya mashahidi ndio iliyopaswa kuwa ya kwanza kumuua mtu mwenye hatia. Hilo liliwazuia watu kutoa ushahidi wa uwongo, haraka-haraka, au bila msingi wowote (Kum 17:7)
Kutoa ushahidi wa uwongo
Ushahidi wa uwongo ulikatazwa kabisa (Kut 20:16; 23:1; Kum 5:20)
Ikiwa mtu angeshtakiwa kwa uwongo, shahidi wa uwongo angepokea adhabu ambayo alimpangia ndugu yake kwa hila (Kum 19:16-19)
Rushwa, upendeleo katika hukumu
Rushwa ilikatazwa (Kut 23:8; Kum 27:25)
Kupotosha haki kulikatazwa (Kut 23:1, 2, 6, 7; Law 19:15, 35; Kum 16:19)
Mtu alitiwa kifungoni ikiwa tu kesi ilikuwa gumu na ilihitaji kuamuliwa na Yehova (Law 24:11-16, 23; Hes 15:32-36)
Adhabu
Viboko—mtu angepigwa viboko visivyozidi 40, ili asiaibishwe (Kum 25:1-3; linganisha na 2Ko 11:24)
Kuua kwa kupiga mawe—kisha mwili ungetundikwa mtini kwa sababu alikuwa amelaaniwa (Kum 13:10; 21:22, 23)
Kulipiza kisasi—malipo, adhabu inayolingana (Law 24:19, 20)
Hasara: Ikiwa mnyama wa mtu angeharibu shamba la mwingine (Kut 22:5; 21:35, 36); ikiwa mtu angewasha moto na kuteketeza mali ya mwingine (Kut 22:6); ikiwa mtu angemuua mnyama wa kufugwa wa mtu mwingine (Law 24:18, 21; Kut 21:33, 34); ikiwa mtu angetumia bila kukusudia vitu “vitakatifu,” kama vile sehemu za kumi au dhabihu (Law 5:15, 16); ikiwa mtu angemdanganya mwenzake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa atunze au alichoachiwa kwa dhamana au kumnyang’anya au kuchukua kitu kilichopatikana, na kuapa kwa uwongo kuhusu vitu hivyo (Law 6:2-7; Hes 5:6-8)
Majiji ya makimbilio
Mtu aliyeua bila kukusudia angekimbilia katika jiji lililo karibu (Hes 35:12-15; Kum 19:4, 5; Yos 20:2-4)
Kisha kesi ilifanyiwa mahali mauaji yalipotokea
Mtu aliyeua bila kukusudia alipaswa kuishi katika jiji la makimbilio mpaka kifo cha kuhani mkuu (Hes 35:22-25; Yos 20:5, 6)
Mtu aliyeua kimakusudi aliuawa (Hes 35:30, 31)
NDOA, MAHUSIANO YA FAMILIA, MAADILI YA NGONO
(Sheria iliwalinda Waisraeli kwa kulinda utakatifu wa ndoa na maisha ya familia)
Ndoa ya kwanza ilianzishwa na Yehova (Mwa 2:18, 21-24)
Mume alimmiliki mke wake lakini aliwajibika mbele za Mungu kwa jinsi alivyomtendea mkewe (Kum 22:22; Mal 2:13-16)
Ndoa za wake wengi ziliruhusiwa lakini zilidhibitiwa ili kumlinda mke na wazao wake (Kum 21:15-17; Kut 21:10)
Baada ya mwanamume kumtongoza bikira ilikuwa lazima amwoe (ila ikiwa tu baba ya msichana alikataa) (Kut 22:16, 17; Kum 22:28, 29)
Ndoa ya ndugu mkwe ilipangwa ili mwanamume amwoe mjane aliyeachwa na ndugu yake aliyekufa bila mwana; ikiwa mwanamume angekataa kufanya hivyo angeshutumiwa (Kum 25:5-10)
Hawakuruhusiwa kuoa wageni (Kut 34:12-16; Kum 7:1-4), lakini waliruhusiwa kuoa wanawake waliokuwa mateka (Kum 21:10-14)
Wanawake waliorithi ardhi waliolewa na wanaume wa kabila lao tu (Hes 36:6-9)
Talaka
Mume tu ndiye aliyeruhusiwa kutaliki (ikiwa angeona jambo lisilofaa katika mke wake); alipaswa kumwandikia mke cheti cha talaka (Kum 24:1-4)
Hakuruhusiwa kumtaliki ikiwa alimwoa baada ya kumtongoza (Kum 22:28, 29)
Mwanamume hangemwoa tena mwanamke aliyemtaliki akaolewa tena na kutalikiwa na mume wa pili au baada ya mume huyo wa pili kufa (Kum 24:1-4)
Mwanamume na mwanamke waliofanya uzinzi walipata adhabu ya kifo (Kut 20:14; Kum 22:22)
Ngono kati ya watu wa ukoo
Mwanamume Mwisraeli hangeoa wafuatao: Mama yake, mama wa kambo, au mke wa pili wa baba yake (Law 18:7, 8; 20:11; Kum 22:30; 27:20); dada yake au binti ya baba au ya mama yake (Law 18:9, 11; 20:17; Kum 27:22); binti ya mwana au binti ya binti yake (Law 18:10); dada ya baba au mama yake (Law 18:12, 13; 20:19); shangazi yake (mke wa ndugu ya baba yake au ndugu ya mama yake) (Law 18:14; 20:20); binti mkwe wake (Law 18:15; 20:12); binti yake, binti ya mke wake, binti ya binti ya mke wake, binti ya mwana wa mke wake, mama mkwe wake (Law 18:17; 20:14; Kum 27:23); mke wa ndugu yake (Law 18:16; 20:21), isipokuwa katika ndoa ya ndugu mkwe (Kum 25:5, 6); dada ya mke wake ikiwa mke wake angali hai (Law 18:18)
Mwanamke Mwisraeli hangeolewa na wafuatao: Mwana wake au mwana wa mume wake (Law 18:7, 8; 20:11; Kum 22:30; 27:20); ndugu yake au ndugu ya baba au mama yake (Law 18:9, 11; 20:17; Kum 27:22); babu yake (Law 18:10); mpwa wake (mwana wa ndugu au dada yake) (Law 18:12, 13; 20:19); mwana wa ndugu au dada ya mume wake (Law 18:14; 20:20); baba mkwe wake (Law 18:15; 20:12); baba yake, mume wa mama yake, baba wa kambo wa mama yake, baba wa kambo wa baba yake, mwana mkwe wake (Law 18:7, 17; 20:14; Kum 27:23); ndugu ya mume wake (Law 18:16; 20:21), isipokuwa katika ndoa ya ndugu mkwe (Kum 25:5, 6); mume wa dada yake ikiwa dada yake angali hai (Law 18:18)
Adhabu ya ngono kati ya watu wa ukoo: kifo (Law 18:29; 20:11, 12, 14, 17, 20, 21)
Ngono wakati wa hedhi
Mwanamume na mwanamke waliofanya ngono kimakusudi wakati wa hedhi, waliuawa (Law 18:19; 20:18)
Mume aliyefanya ngono na mke wakati wa hedhi (labda hedhi ilianza bila kutazamiwa) hangekuwa safi kwa siku saba (Law 15:19-24)
Uhusiano wa wazazi na watoto
Wazazi (hasa akina baba) waliamriwa wawafundishe watoto wao Sheria ya Mungu (Kum 6:6-9, 20-25; 11:18-21; Isa 38:19)
Watoto walipaswa kuwaheshimu wazazi (Kut 20:12; 21:15, 17; Law 19:3; Kum 5:16; 21:18-21; 27:16)
Hawakupaswa kuvaa mavazi ya watu wa jinsia tofauti (kwa kusudi la kuvutia kingono) (Kum 22:5)
Wanaume waliolala na wanaume waliuawa wote wawili (Law 18:22; 20:13)
Mtu aliyefanya ngono na mnyama aliuawa pamoja na mnyama huyo (Kut 22:19; Law 18:23, 29; 20:15, 16; Kum 27:21)
Mwanamke aliyemshambulia mwanamume kwa njia isiyofaa (mwanamke aliyeingilia vita na kukamata sehemu za siri za mwanamume aliyepigana na mume wake) aliadhibiwa kwa kukatwa mkono, badala ya kupata adhabu inayolingana, kwa sababu Yehova aliheshimu uwezo wake wa kuzaa na haki ya mume wake ya kupata watoto kupitia kwake (Kum 25:11, 12)
SHUGHULI ZA BIASHARA
(Sheria ilisisitiza watu wawe wanyoofu katika shughuli za biashara na kuheshimu nyumba na mali ya wengine)
Kumiliki ardhi
Familia ziligawiwa ardhi (Hes 33:54; 36:2)
Ardhi haikuuzwa milele bali ilirudishwa kwa mwenyewe kwenye Mwadhimisho wa Miaka 50; thamani yake ilitegemea idadi ya mazao yaliyobaki kufikia Mwadhimisho wa Miaka 50 (Law 25:15, 16, 23-28)
Ikiwa shamba liliuzwa, mtu wa karibu wa ukoo alikuwa na haki ya kulinunua (Yer 32:7-12)
Serikali haikuwa na haki ya kuchukua ardhi ya mtu ya urithi na kuilipia fidia ili itumiwe na umma (1Fa 21:2-4)
Walawi waligawiwa majiji na malisho yake
Kati ya majiji 48 waliyogawiwa, 13 yalikuwa majiji ya makuhani (Hes 35:2-5; Yos 21:3-42)
Malisho ya jiji la Walawi hayangeuzwa; yalikuwa mali ya jiji hilo, si ya watu binafsi (Law 25:34)
Ikiwa mtu alitakasa (aliweka kando au kutolima) sehemu fulani ya shamba lake ili iwe ya Yehova (itumiwe kwa ajili ya patakatifu, ukuhani), thamani yake ilikadiriwa kulingana na kiasi cha mbegu zilizohitaji kupandwa, homeri moja ya mbegu za shayiri ilikuwa shekeli 50 za fedha; thamani yake ilipungua kulingana na miaka iliyobaki kufikia Mwadhimisho wa Miaka 50 (Law 27:16-18)
Ikiwa mtakasaji alitaka kulinunua tena, alipaswa kulipa thamani yake pamoja na asilimia 20 ya thamani iliyokadiriwa (Law 27:19)
Ikiwa hakulinunua lakini akamuuzia mwingine, wakati wa Mwadhimisho wa Miaka 50 lingekuwa mali ya makuhani, kitu kitakatifu kwa Yehova (Law 27:20, 21)
Ikiwa mtu alitakasa sehemu ya shamba alilonunua kutoka kwa mwingine ili iwe ya Yehova, wakati wa Mwadhimisho wa Miaka 50 ilirudishwa kwa mmiliki wa shamba hilo (Law 27:22-24)
Ikiwa mtu ‘aliweka wakfu’ kitu chochote kati ya vitu vyake (vitu ‘vilivyowekwa wakfu’ vilitumiwa tu mahali patakatifu au viliharibiwa; Yos 6:17; 7:1, 15; Eze 44:29), hakingeuzwa au kununuliwa tena; kilibaki mali ya Yehova (Law 27:21, 28, 29)
Kukomboa mali
Ardhi yote ilirudishwa kwa mmiliki wake wa awali wakati wa Mwadhimisho wa Miaka 50 (isipokuwa katika hali zilizotajwa awali) (Law 25:8-10, 15, 16, 24-28)
Walawi wangekomboa nyumba zao katika majiji ya Walawi wakati wowote (Law 25:32, 33)
Mwaka wa Mwadhimisho wa Miaka 50: ulianza Siku ya Kufunika Dhambi, katika mwaka wa 50; kuhesabu kulianzia mwaka ambao Waisraeli waliingia nchini (Law 25:2, 8-19)
Urithi
Mzaliwa wa kwanza alirithi mali maradufu (Kum 21:15-17)
Ikiwa mtu alikufa bila mwana, urithi ulichukuliwa na binti zake. (Hes 27:6-8) Ikiwa mtu hakuwa na wana au mabinti, ndugu zake, ndugu za baba yake, au mtu wake wa karibu wa ukoo alichukua urithi wake (Hes 27:9-11)
Mizani na vipimo
Yehova aliwaamuru wawe wanyoofu na watumie vipimo sahihi (Law 19:35, 36; Kum 25:13-15)
Mizani ya uwongo ilimchukiza (Met 11:1)
Madeni
Mwishoni mwa kila miaka saba walipaswa kufuta madeni ya ndugu zao Waebrania (Kum 15:1, 2)
Wangeweza kumdai mgeni alipe deni (Kum 15:3)
Dhamana ya mkopo
Ikiwa mtu alichukua vazi la nje la mwenzake kuwa dhamana ya mkopo, hakupaswa kukaa nalo usiku kucha (Kwa kawaida maskini walitumia mavazi hayo usiku kwa sababu hawakuwa na nguo za kulala) (Kut 22:26, 27; Kum 24:12, 13)
Mtu hangeingia katika nyumba ya mwenzake ili kuchukua kitu kuwa rehani au dhamana ya mkopo. Alipaswa kusimama nje ya nyumba na kumruhusu mkopaji amletee nje (Hilo lilidumisha usalama wa nyumba ya mtu huyo) (Kum 24:10, 11)
Mtu hakupaswa kuchukua jiwe la chini la kusagia au jiwe la juu la kusagia kuwa dhamana (Hangeweza kusaga nafaka ambayo yeye na familia yake wangekula) (Kum 24:6)
SHERIA ZA JESHI
(Sheria hizo zilidhibiti vita vya Waisraeli vilivyokubaliwa na Mungu katika Nchi ya Ahadi. Mungu alikataza kabisa vita vilivyoongozwa na ubinafsi au vilivyopita mipaka aliyoweka)
Vita
Vilipaswa kuwa tu vita vya Yehova (Hes 21:14; 2Nya 20:15)
Wanajeshi walitakaswa kabla ya kwenda vitani (1Sa 21:1-6; linganisha na Law 15:16, 18)
Umri wa wanajeshi
Miaka ishirini na zaidi (Hes 1:2, 3; 26:1-4)
Kitabu Jewish Antiquities, III, 288 (xii, 4), cha Josephus, kinasema walitumikia jeshini hadi walipofikia umri wa miaka 50
Waliokatazwa kuwa wanajeshi:
Walawi, wakiwa wahudumu wa Yehova (Hes 1:47-49; 2:33)
Mwanamume ambaye hakuwa ameizindua nyumba yake mpya au hajaanza kuvuna matunda ya shamba lake la mizabibu (Kum 20:5, 6; linganisha na Mhu 2:24; 3:12, 13)
Mwanamume aliyemchumbia mwanamke lakini bado hajamwoa. Mwanamume aliyeoa karibuni hakuruhusiwa kutumikia jeshini kwa mwaka mmoja (Alikuwa na haki ya kupata mrithi na kumwona mrithi huyo) (Kum 20:7; 24:5)
Mtu mwoga (Angewavunja moyo wanajeshi wenzake) (Kum 20:8; Amu 7:3)
Walipaswa kudumisha usafi katika kambi za kivita (kwa sababu wanajeshi walitakaswa kwa ajili ya vita) (Kum 23:9-14)
Wanawake hawakuruhusiwa kuja kambini kwa ajili ya mahusiano ya kingono; mahusiano hayo yaliepukwa muda wote wa vita. Hilo lilihakikisha kuna usafi wa kidini na wa kimwili (Law 15:16; 1Sa 21:5; 2Sa 11:6-11)
Hawakuruhusiwa kuwabaka wanawake wa maadui, kwa sababu huo ungekuwa uasherati; na hawakuruhusiwa kufunga ndoa nao wakati wa vita. Kwa njia hiyo walidumisha usafi wa kidini na kuwashawishi maadui wajisalimishe, kwa sababu wangekuwa na uhakika kwamba wanawake wao hawatatendewa vibaya (Kum 21:10-13)
Mipango ya kushambulia majiji ya maadui
Ikiwa jiji lililoshambuliwa lilikuwa kati ya yale mataifa saba ya nchi ya Kanaani (yaliyotajwa katika Kum 7:1), wakaaji wote walipaswa kuangamizwa. (Kum 20:15-17; Yos 11:11-14; Kum 2:32-34; 3:1-7) Ikiwa wangebaki nchini, wangehatarisha uhusiano wa Waisraeli pamoja na Yehova Mungu. Aliwaacha waendelee kuishi hadi uovu wao uwe kamili (Mwa 15:13-21)
Masharti ya amani yalitangazwa kwanza katika majiji ambayo hayakuwa kati ya yale mataifa saba. (Kum 20:10, 15) Ikiwa jiji lingejisalimisha, wakaaji wake wangefanya kazi za utumwa. Ikiwa halingejisalimisha, wanaume wote na wanawake wote ambao si mabikira wangeuawa. Wengine wangechukuliwa mateka. (Kum 20:11-14; linganisha na Hes 31:7, 17, 18.) Kuwaua wanaume wote kuliondoa hatari ya jiji hilo kuasi baadaye na pia kuwazuia wanaume hao wasioe wanawake Waisraeli. Hatua hizo zilisaidia pia kuzuia ibada ya sanamu za uume na magonjwa kati ya Waisraeli
Miti ya chakula haingekatwa na kutumiwa kulizingira jiji (Kum 20:19, 20)
Magari ya vita yalichomwa moto; farasi walikatwa mishipa ya miguu ili wasiweze kutumiwa vitani, na baadaye waliuawa (Yos 11:6)
SHERIA KUHUSU VYAKULA NA USAFI
(Sheria hizo ziliwatenga Waisraeli na mataifa ya kipagani, ziliwasaidia kudumisha usafi na afya, na ziliwakumbusha umuhimu wa kuwa watakatifu machoni pa Mungu; Law 19:2)
Matumizi ya damu
Walikatazwa kabisa kula damu. (Mwa 9:4; Law 7:26; 17:12; Kum 12:23-25) Aliyekula damu alipata adhabu ya kifo (Law 7:27; 17:10)
Uhai (nafsi) uko katika damu (Law 17:11, 14)
Damu ya mnyama aliyechinjwa ilipaswa kumwagwa ardhini kama maji na kufunikwa kwa udongo (Law 17:13; Kum 12:16)
Mnyama aliyekufa mwenyewe au aliyepatikana amekufa hakupaswa kuliwa (kwa sababu hakuwa safi na damu yake haikuwa imemwagwa ifaavyo) (Kum 14:21)
Damu ilitumiwa tu kwa makusudi ya kisheria: ilitiwa kwenye madhabahu ili kufunika dhambi; ilitumiwa katika kutakasa (Law 17:11, 12; Kum 12:27; Hes 19:1-9)
Jinsi mafuta yalivyotumiwa
Mafuta yoyote hayakuliwa; yalikuwa ya Yehova (Law 3:16, 17; 7:23, 24)
Yeyote aliyekula mafuta ya dhabihu alipata adhabu ya kifo (Law 7:25)
Wanyama waliochinjwa
Wanyama wowote wa kufugwa waliochinjwa nyikani waliletwa katika hema la ibada. Waliliwa wakiwa dhabihu za ushirika (Law 17:3-6)
Aliyekosa kufanya hivyo alipata adhabu ya kifo (Law 17:4, 8, 9)
Wanyama wa mwituni walio safi ambao walikamatwa waliuawa papo hapo; damu yao ilipaswa kumwagwa ardhini (Law 17:13, 14)
Baada ya kuingia katika Nchi ya Ahadi, mtu aliyeishi mbali na mahali patakatifu aliruhusiwa kumchinjia mnyama safi nyumbani kwa ajili ya chakula, lakini alipaswa kumwaga damu ardhini (Kum 12:20-25)
Wanyama, samaki, na wadudu wafuatao waliliwa:
Mnyama yeyote mwenye kwato zilizopasuka na kugawanyika, na anayecheua (Law 11:2, 3; Kum 14:6)
Kiumbe yeyote mwenye mapezi na magamba anayeishi ndani ya maji (Law 11:9-12; Kum 14:9, 10)
Wadudu na viumbe wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa ambao wanatambaa kwa miguu minne na kuruka: nzige wanaohama, nzige wanaoliwa, chenene, na panzi (wote kulingana na aina zao) (Law 11:21, 22)
Wanyama, samaki, ndege, na wanyama wanaoishi katika makundi makubwa ambao hawakupaswa kuliwa:
Wanyama: ngamia, wibari, sungura, nguruwe (Law 11:4-8; Kum 14:7, 8)
Samaki na viumbe wengine wasio na mapezi wala magamba wanaoishi katika makundi makubwa ndani ya maji (Law 11:10)
Ndege na viumbe wanaoruka: tai, furukombe, tumbusi mweusi, mwewe mwekundu, mwewe mweusi, ndege mbua, kunguru, mbuni, bundi, shakwe, kipanga, bundi mdogo, bundi mwenye masikio marefu, batamaji, mwari, tumbusi, mnandi, korongo, kulastara, hudihudi, popo, kila kiumbe anayeishi katika makundi makubwa anayetembea kwa miguu minne (yaani, anayetembea kama wanyama wenye miguu minne). Biblia haitaji moja kwa moja mambo yaliyoamua ikiwa viumbe wanaoruka si “safi” kidesturi. Ingawa ndege wengi wanaokula nyama au mizoga walikuwa “si safi,” si wote walioonwa hivyo (Kum 14:12-19; Law 11:13-20; ona NDEGE na makala nyingine kuhusu ndege hususa)
Viumbe wanaoishi katika makundi makubwa duniani: fuko, panya, mjusi, mjusi kafiri, mjusi mkubwa, mjusi wa majini, mjusi wa mchangani, kinyonga, kiumbe yeyote anayetambaa kwa tumbo, anayetembea kwa miguu yote minne, au aliye na miguu mingi (Law 11:29, 30, 42)
Mnyama aliyekufa mwenyewe au aliyepatikana amekufa au aliyeraruliwa na mnyama wa mwituni (Law 17:15, 16; Kum 14:21; Kut 22:31)
Ikiwa wanyama walitolewa kwa ajili ya nadhiri au toleo la hiari, dhabihu ya ushirika ililiwa siku iliyotolewa na kesho yake lakini si siku ya tatu; mtu aliyekula siku ya tatu alipata adhabu ya kifo. Dhabihu ya shukrani ililiwa siku iliyotolewa; hawakupaswa kuhifadhi sehemu yoyote mpaka asubuhi (siku ya pili). Dhabihu ya Pasaka haikupaswa kuachwa mpaka asubuhi; sehemu ambayo haikuliwa iliteketezwa (Law 7:16-18; 19:5-8; 22:29, 30; Kut 12:10)
Mambo yaliyomfanya mtu asiwe safi:
Kutokwa na shahawa
Mtu alipaswa kuoga na hakuwa safi mpaka jioni (Law 15:16; Kum 23:10, 11)
Vazi lililomwagikiwa na shahawa lilifuliwa, na halikuwa safi mpaka jioni (Law 15:17)
Mume na mke, baada ya kufanya ngono, walipaswa kuoga na hawakuwa safi mpaka jioni (Law 15:18)
Kuzaa mtoto
Mwanamke hakuwa safi kwa siku 7 baada ya kuzaa mtoto wa kiume, na siku 33 zaidi (siku 7 za kwanza, hangegusa chochote, kama wakati wa hedhi; kwa siku 33 hakuwa safi na hivyo hakugusa vitu vitakatifu kama vile vyakula vya dhabihu au kuingia mahali patakatifu) (Law 12:2-4)
Ikiwa mtoto ni wa kike, mwanamke hakuwa safi kwa siku 14, na siku 66 zaidi (Law 12:5)
Hedhi ya mwanamke (Law 12:2)
Mwanamke hakuwa safi kwa siku saba za hedhi ya kawaida; na pia kwa kipindi chote alichotokwa na damu isivyo kawaida au kwa muda unaozidi kipindi cha hedhi, na siku saba zaidi (Law 15:19, 25, 28)
Kitu chochote alichokalia au kulalia muda wote ambao hakuwa safi hakikuwa safi (Law 15:20)
Mtu aliyemgusa au kugusa kitanda chake au kugusa chochote alichokalia alipaswa kufua mavazi yake na kuoga, na hakuwa safi mpaka jioni (Law 15:21-23)
Ikiwa damu yake ya hedhi ilimgusa mwanamume, hangekuwa safi kwa siku saba, na kitanda chochote alicholalia mwanamume huyo hakikuwa safi (Law 15:24)
Wakati wowote mwanamke alipotokwa na damu hakuwa safi (Law 15:25
Kujilinda na magonjwa
Ukoma na magonjwa mengine hatari
Kuhani aliamua ikiwa mtu alikuwa na ukoma au la (Law 13:2)
Mtu alitengwa kwa siku saba na kisha kuchunguzwa; ikiwa ugonjwa haukuenea, alitengwa kwa siku nyingine saba (Law 13:4, 5, 21, 26); ikiwa haukuenea basi alitangazwa kuwa safi (Law 13:6); ikiwa ulienea, ulikuwa ukoma (Law 13:7, 8)
Mtu mwenye ukoma alivaa mavazi yaliyoraruka, hakutunza nywele zake, naye alifunika masharubu yake (au mdomo wa juu), na kusema hivi kwa sauti: “Mimi si safi, mimi si safi!” Alitengwa na kuishi nje ya kambi. (Law 13:45, 46; Hes 5:2-4)
Kutokwa na umajimaji kwenye kiungo cha uzazi (kwa sababu ya ugonjwa fulani) (Law 15:2, 3)
Kitanda au kitu chochote alichokalia au kulalia hakikuwa safi (Law 15:4)
Yeyote aliyemgusa mtu huyo, kitanda chake, au chochote alichokalia, hakuwa safi, au ikiwa mtu huyo alimtemea mate mtu mwingine, mtu huyo hakuwa safi (Law 15:5-11)
Vyombo vya udongo vilivyoguswa na mtu aliyetokwa na umajimaji vilivunjwa, na vyombo vya mbao vilisafishwa kwa maji (Law 15:12)
Baada ya umajimaji kuacha kutoka, mtu huyo hakuwa safi kwa siku saba (Law 15:13)
Usafi wa kambi ya majeshi ulidumishwa kwa kufuata sheria ya kuwa na mahali pa kujisaidia nje ya kambi na kufunika kinyesi (Kum 23:12, 13)
Sheria kuhusu maiti
Mtu aliyegusa maiti au mfupa wa mtu aliyekufa, au kaburi la mwanadamu hakuwa safi kwa siku saba (hata kama ni uwanjani). (Hes 19:11, 16) Aliyekataa kujitakasa aliuawa (Hes 19:12, 13) (Angalia utaratibu wa kujitakasa katika Hes 19:17-19)
Wote waliokuwa ndani au walioingia ndani ya hema lililokuwa na maiti hawakuwa safi na pia chombo chochote kilichofunuliwa ambacho kifuniko chake hakikuwa kimefungwa kwa kamba (Hes 19:14, 15)
Sheria kuhusu mizoga ya wanyama
Mtu aliyebeba, aliyegusa, au aliyekula mzoga wa mnyama safi aliyekufa mwenyewe hakuwa safi; aliyegusa mzoga wa mnyama yeyote asiye safi hakuwa safi. Alipaswa kujitakasa (Law 11:8, 11, 24-31, 36, 39, 40; 17:15, 16)
Vyombo, majiko, nguo, ngozi, na magunia yaliyoguswa na mzoga wa mnyama asiye safi hayakuwa safi (Law 11:32-35)
Nyara zilizochukuliwa kutoka katika jiji
Kila kitu ambacho kilistahimili moto kilipitishwa motoni (vyuma), kisha kilitakaswa kwa kutumia maji ya kutakasa; vitu vingine vilipaswa kusafishwa (Hes 31:20, 22, 23)
MAAGIZO KUHUSU VIUMBE WENGINE
(Sheria ilisema kwamba lazima “umpende mwenzako kama unavyojipenda mwenyewe”; Law 19:18. Yesu alisema kwamba hiyo ndiyo amri ya pili iliyo kuu zaidi katika Sheria; Mt 22:37-40)
Kuwaelekea Waisraeli wenzao
Walipaswa kupendana; walikatazwa kuuana (Kut 20:13; Ro 13:9, 10)
Hawakupaswa kulipiza kisasi au kuweka kinyongo dhidi ya wenzao (Law 19:18)
Kuwatunza maskini (Kut 23:6; Law 25:35, 39-43)
Kuwatunza wajane na mayatima (Kut 22:22-24; Kum 24:17-21; 27:19)
Kuheshimu mali
Walikatazwa kuiba; aliyeiba alilipa fidia (Kut 20:15; 22:1-4, 7)
Walikatazwa kutamani mali na vitu vya mtu mwingine (Kut 20:17)
Kuwajali walemavu
Hawakupaswa kumdhihaki au kumtukana kiziwi; hangeweza kujitetea kwa sababu hasikii (Law 19:14)
Aliyeweka kizuizi mbele ya kipofu au kumfanya apotee njia alilaaniwa (Law 19:14; Kum 27:18)
Kuwaelekea wakaaji wageni: hawakupaswa kuteswa (Kut 22:21; 23:9; Law 19:33, 34; Kum 10:17-19; 24:14, 15, 17; 27:19)
Kuwaelekea watumwa
Mtumwa Mwebrania aliwekwa huru katika mwaka wake wa saba wa utumwa au mwaka wa Mwadhimisho wa Miaka 50. Alitendewa vizuri kama mfanyakazi aliyeajiriwa muda wote aliokuwa mtumwa (Kut 21:2; Kum 15:12; Law 25:10)
Ikiwa mwanamume alikuja na mke wake, mke aliondoka naye au aliwekwa huru pamoja naye (Kut 21:3)
Ikiwa bwana wake alimpa mke (wa kigeni) akiwa utumwani, mtumwa huyo aliwekwa huru peke yake; ikiwa mke alimzalia watoto, mke pamoja na watoto wake walibaki kuwa mali ya bwana wake (Kut 21:4)
Mtumwa Mwebrania alipowekwa huru, bwana wake alimpa zawadi kulingana na vitu alivyokuwa navyo (Kum 15:13-15)
Mtumwa angeweza kupigwa kwa fimbo na bwana wake. (Kut 21:20, 21) Ikiwa alilemaa, aliwekwa huru. (Kut 21:26, 27) Ikiwa bwana alimpiga mtumwa na kumuua, bwana huyo angepata adhabu ya kifo; waamuzi waliamua adhabu (Kut 21:20; Law 24:17)
Kuwaelekea wanyama
Ikiwa mtu alikutana na mnyama wa kufugwa akiteseka, alipaswa kumsaidia, hata kama alikuwa wa adui yake (Kut 23:4, 5; Kum 22:4)
Wanyama waliobeba mizigo hawakupaswa kuteswa au kufanya kazi kupita kiasi (Kum 22:10; linganisha na Met 12:10)
Ng’ombe dume hakufungwa kinywa alipopura, ili aweze kula nafaka alizokuwa akipura (Kum 25:4; linganisha na 1Ko 9:7-10)
Mtu hakupaswa kuchukua ndege pamoja na mayai yake, na hivyo kuangamiza familia yote (Kum 22:6, 7)
Mtu hakupaswa kumchinja ng’ombe dume au kondoo pamoja na mtoto wake siku ileile (Law 22:28)
KUSUDI LA SHERIA
Ilifanya makosa yawe wazi; ilionyesha kwamba Waisraeli walihitaji kusamehewa dhambi zao na kwamba walihitaji dhabihu kubwa zaidi ambayo ingeweza kufunika dhambi zao kikweli (Ga 3:19)
Ilikuwa mtunzaji, iliwaongoza na kuwatia nidhamu Waisraeli, ili kuwatayarisha kwa ajili ya Masihi ikiwa mfundishaji wao (Ga 3:24)
Mambo mbalimbali ya Sheria yalikuwa vivuli vya mambo makubwa ambayo yangekuja; vivuli hivyo viliwasaidia Waisraeli wenye moyo mnyoofu kumtambua Masihi, kwa kuwa wangeona jinsi unabii huo ulivyotimia kumhusu (Ebr 10:1; Kol 2:17)