-
Maswali Manne Kuhusu Mwisho YajibiwaMnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 1
-
-
Jifunze kutokana na historia. Petro aliandika kwamba Mungu “hakujizuia kuuadhibu ulimwengu wa kale, bali alimlinda Noa, mhubiri wa uadilifu, akiwa salama pamoja na wengine saba alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiomwogopa Mungu.” (2 Petro 2:5) Pia, aliandika hivi kuwahusu wadhihaki: “Kulingana na kupenda kwao, wao hawalioni jambo hili, kwamba mbingu zilikuwapo tangu zamani za kale na dunia ikisimama imara kutoka katika maji na katikati ya maji kwa neno la Mungu; na kwa njia hizo ulimwengu wa wakati huo uliangamia kwa gharika ya maji. Lakini kwa neno hilohilo mbingu na duniab za sasa zimewekwa akiba kwa ajili ya moto nazo zinahifadhiwa mpaka ile siku ya hukumu na ya kuangamizwa kwa watu wasiomwogopa Mungu.”—2 Petro 3:5-7.
-
-
Maswali Manne Kuhusu Mwisho YajibiwaMnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 1
-
-
b Katika andiko hilo Petro anazungumzia dunia ya mfano. Musa, mwandikaji mwingine wa Biblia, alizungumzia pia dunia ya mfano. Aliandika hivi: “Dunia yote iliendelea kuwa na lugha moja.” (Mwanzo 11:1) Dunia halisi haiwezi kuzungumza “lugha moja,” hali kadhalika, si dunia halisi itakayoharibiwa. Lakini kama Petro anavyosema, ni watu wasiomwogopa Mungu watakaoangamizwa.
-