-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
3. Yohana anatuambia ni nini kitakachompata Shetani?
3 Basi, ni nini kilicho akibani kwa ajili ya Shetani mwenyewe na roho waovu wake? Yohana hutuambia: “Na mimi nikaona malaika mmoja akija chini kutoka katika mbingu mwenye ufunguo wa abiso na mnyororo mkubwa katika mkono wake. Na yeye akakamata drakoni, nyoka wa awali kabisa, ambaye ndiye Ibilisi na Shetani, na akamboba yeye kwa miaka elfu moja. Na yeye alimvurumisha ndani ya abiso na akaifunga na akatia kalafati juu yake, ili asipate kuongoza vibaya mataifa tena mpaka miaka elfu ilipokuwa imekwisha. Baada ya vitu hivi ni lazima yeye aachwe legelege kwa kitambo kidogo.”—Ufunuo 20:1-3, NW.
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
5. Malaika wa abiso hushughulikaje na Shetani Ibilisi, na kwa nini?
5 Drakoni mkubwa mwenye rangi-moto alipovurumishwa chini kutoka katika mbingu, alisemwa kuwa ndiye “nyoka wa awali kabisa, mmoja ambaye huitwa Ibilisi na Shetani, ambaye anaongoza vibaya dunia nzima yote inayokaliwa.” (Ufunuo 12:3, 9, NW) Sasa, wakati wa kukamatwa kwake na kutiwa ndani ya abiso, yeye ameelezwa tena kwa ukamili kuwa ndiye “drakoni, nyoka wa awali kabisa, ambaye ndiye Ibilisi na Shetani.” Huyu ambaye ni mmezaji, mdanganyaji, mchongezi, na mpinzani mwenye sifa mbaya sana anafungwa mnyororo na kuvurumishwa “ndani ya abiso,” ambayo inashindikwa ndi ndi ndi na kutiwa kalafati kikiki, “ili asipate kuongoza vibaya mataifa tena.” Huku kutiwa kwa Shetani ndani ya abiso ni kwa muda wa miaka elfu moja, wakati huo uvutano wake juu ya aina ya binadamu utakuwa haupo tena kama wa mfungwa aliye ndani ya gereza la shimo lenye kina kirefu. Malaika wa abiso anamwondolea mbali kabisa Shetani asiwe na mgusano wowote na Ufalme wa uadilifu. Lo! ni kitulizo kama nini kwa aina ya binadamu!
-