-
Yehova Hupendezwa Sana na Utumishi Wako wa Nafsi YoteMnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
-
-
5. Kielelezo cha mitume chaonyeshaje kwamba si lazima wote wafanye yaleyale katika huduma?
5 Je, kuwa wenye nafsi yote kwamaanisha kwamba lazima sisi sote tufanye kiwango kilekile katika huduma? Hilo lisingewezekana hata kidogo, kwa kuwa hali na uwezo hutofautiana kati ya nafsi moja na ile nyingine. Wafikirie mitume waaminifu wa Yesu. Wote hawakuweza kufanya kiwango kilekile. Mathalani, twajua machache sana kuhusu baadhi ya mitume hao, kama vile Simoni Mkananayo na Yakobo mwana wa Alfayo. Labda utendaji wao wakiwa mitume ulikuwa kidogo. (Mathayo 10:2-4) Kwa kutofautisha, Petro aliweza kukubali madaraka mengi mazito kwani, hata Yesu alimpa “funguo za ufalme wa mbingu”! (Mathayo 16:19) Hata hivyo, Petro hakuinuliwa kuliko wale wengine. Yohana alipopokea ile njozi ya Yerusalemu Jipya katika Ufunuo (wapata mwaka wa 96 W.K.), aliona mawe 12 ya msingi na “majina kumi na mawili ya mitume kumi na wawili” yaliandikwa juu yake.a (Ufunuo 21:14) Yehova alithamini utumishi wa hao mitume wote, hata ingawa baadhi yao kwa wazi waliweza kufanya mengi zaidi kuliko wengine.
-
-
Yehova Hupendezwa Sana na Utumishi Wako wa Nafsi YoteMnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
-
-
a Kwa kuwa Mathiasi alichukua mahali pa Yudasi akiwa mtume, jina lake—wala si jina la Paulo—lingeonekana miongoni mwa yale mawe 12 ya msingi. Ijapokuwa Paulo alikuwa mtume, hakuwa mmoja wa wale 12.
-