-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
9. Ni maagizo gani ya pigano waliyopokea hao nzige?
9 Ni maagizo gani ya pigano waliyopokea hao nzige? Yohana anaripoti: “Na wao waliambiwa wasidhuru mmea wowote wa dunia wala kitu chochote cha chanikiwiti wala mti wowote, ila wale watu tu ambao hawana muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao. Na hao nzige walipewa ruhusa, si kuua wao, bali kwamba hawa wapaswe kuteswa kwa miezi mitano, na mateso yaliyokuwa juu yao yalikuwa kama mateso ya nge wakati anapopiga mtu. Na katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatapata hicho, na wao watatamani kufa lakini kifo hufuliza kukimbia kutoka kwao.”—Ufunuo 9:4-6, NW.
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
11. (a) Nzige wanapewa mamlaka watese adui za Mungu kwa muda gani, na ni kwa nini kwa kweli huo si muda mfupi? (b) Mateso hayo ni makali kadiri gani?
11 Mateso huendelea kwa muda wa miezi mitano. Je! huo ni wakati mfupi kadiri hiyo? Si hivyo kwa maoni yanayohusu nzige halisi. Miezi mitano hueleza habari ya muda wa kawaida wa maisha halisi ya mmoja wa wadudu hawa. Kwa sababu hiyo, ingekuwa ni kadiri ya muda wa kuishi kwao kwamba nzige wa ki-siku-hizi wangeendelea kuchoma kwa uchungu adui za Mungu. Zaidi ya hilo, mateso ni makali sana hivi kwamba watu hutafuta kufa. Kweli, sisi hatuna rekodi kuonyesha kwamba wowote wa hao waliochomwa kwa uchungu na nzige kwa kweli walijaribu kujiua wenyewe. Lakini huo usemi husaidia sisi kupata picha ya ukali wa mateso—kana kwamba kwa shambulio lisilokoma la nge. Yako kama yale mateso yaliyotangulia kuonwa na Yeremia kwa Waisraeli wasioaminika ambao wangetawanywa na Wababuloni washindi na ambao kwao kifo kingependelewa kuliko uhai.—Yeremia 8:3; ona pia Mhubiri 4:2, 3.
-