Wimbo Na. 94
Kuridhika na Zawadi Nzuri za Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Kila tuzo kamilifu,
Na zawadi njema,
Vyote tunavyovipenda,
Tunavyohitaji,
Hushuka kutoka juu,
Kwake Baba yetu,
Ambaye habadiliki Mungu
wetu Yehova.
2. Hatutahangaishwa na
Mahitaji yetu;
Twajua anatujali,
Huwalisha ndege.
Hatupotezi wakati,
Kwa yanayopita.
Twaridhika na maandalizi
yake Yehova.
3. Twaona mengi ambayo,
Ni ubatili tu.
Tutumie siku zetu,
Kuweka hazina.
Hata tukifa, twajua
Haziharibiki.
Tunaridhika na kudumisha
jicho rahisi.
(Ona pia Yer. 45:5; Mt. 6:25-34; 1 Tim. 6:8; Ebr. 13:5.)