WIMBO NA. 132
Sasa Tumekuwa Mwili Mmoja
Makala Iliyochapishwa
1. Huyu ndiye, mfupa wangu
Mwili wangu, nina mwenzangu.
Mungu amenipa mwenzi,
Ninayempenda.
Tumekuwa mwili mmoja,
Tupate baraka za Mungu.
Mume na mke pamoja,
Familia moja.
Daima tumtumikie.
Atuongoze,
Tupendane kikweli.
Tuapavyo, iwe hivyo
Tupate shangwe na furaha.
Tumheshimu Yehova,
Sikuzote uwe wangu.
(Ona pia Mwa. 29:18; Mhu. 4:9, 10; 1 Kor. 13:8.)