Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Rekebisho la Katoliki Nilifikiri makala yenu juu ya historia ya kidini (Juni 8, 1990) iliandikwa vizuri kwa ujumla. Hata hivyo, naamini mmefanya kosa kubwa kwa kumwondoa Martin Luther katika hatia ya “Katoliki kupinga-Usemiti.” Martin Luther alisema maneno mengi yenye chuki dhidi ya wale walio wa rangi ya Kiyahudi, akiwaita “watu waliofisidika na waliolaaniwa” na hata “maibilisi.”
E. W., United States
Makala hiyo ilikazia mazoea yaliyopotoka ya Kanisa Katoliki, wala si kuhusu makosa ya warekebishaji Waprotestanti. Hapo awali Luther hakukubaliana na Katoliki kupinga-Usemiti. Hata hivyo, kitabu cha Kijerumani “Die Juden und Martin Luther—Martin Luther und die Juden,” (Wayahudi na Martin Luther—Martin Luther na Wayahudi), cha Heinz Kremers, chaeleza hivi: “Hapo kwanza Martin Luther alikuwa mwenye urafiki kuelekea Wayahudi, kwa kuwa alitazamia kwamba wangeongoka kuwa Wakristo mara tu gospeli safi ikiisha kuhubiriwa kwao. Wakati tumaini hilo lilipokosa kutimizwa, yeye akawa adui mkubwa wa Wayahudi.”—ED.
Ibada ya Shetani Nilishtushwa na jalada la toleo la Septemba 8, 1990! Sikuzote nimeyaona magazeti haya kuwa yenye kujenga sana. Lakini toleo hilo lanishtua na kunivuruga. Je! si kosa mtu kuwa na mifano ya umbo lolote la Kishetani katika nyumba yake?
P.W., United States
Ni kweli habari ya ibada ya Shetani inashtua. Hata hivyo, sisi twaona tuna wajibu wa kuwaonya wasomaji juu ya ‘hila za shetani,’ na nyakati nyingine hilo lahusisha kueleza habari ambazo huenda wengine wakaona zaudhi. (2 Wakorintho 2:11, “NW”) Hata hivyo, wala maandishi wala picha—kutia ndani uonyeshaji wa mifano ya ibada ya Shetani—hazikuonyeshwa katika njia ambayo ama yahimiza ibada ya Shetani au kuchochea udadisi katika hiyo. Badala yake, vilitumika kuwasaidia wasomaji, kutia ndani vijana, wachukizwe kabisa na kuepuka mazoea ya ibada ya Shetani.—ED.
Nilisoma kwa tisho kubwa na mshangao ripoti yenu juu ya ibada ya Shetani, nami nashukuru mnajulisha wasomaji wenu dhambi hiyo iliyo mbaya sana. Sijaona ushuhuda wowote wa ibada ya Shetani katika eneo la kwangu, lakini, hata hivyo, nitakuwa chonjo kwa ajili ya uwezekano wowote wa kutokea.
M.V.H., M.D., United States
Chawa wa Kichwani Nikiwa mwuguzi wa shuleni, mwenye kushughulika na habari ya chawa wa kichwani kwa ukawaida, nakubaliana na sehemu kubwa ya makala yenu. (Aprili 8, 1990) Lakini kwa kusikitisha, mnapendekeza kunyoa kichwa kuwa njia yenye matokeo zaidi ya kutibu mtoto. Mimi binafsi naonelea kunyoa kichwa cha mtoto ili kuondoa chawa kuwa ni kutenda kupita kiasi na si jambo la lazima. Mimi pia sipendekezi matumizi ya mafuta ya taa kwenye kichwa. Yana sumu na yaweza kuwaka moto, na kwa hakika mamia ya visa vya chawa wa kichwani ni afadhali kuliko mtoto mmoja aliyechomeka.
C.M., Uingereza
Twathamini maelezo hayo. “Amkeni!” halipendekezi matibabu ya kitiba. Lakini kwa kuwa jarida letu hutawanywa ulimwenguni pote na husomwa na watu ambao huenda wasiweze kupata matibabu ya ki-siku-hizi, sisi tuliripoti tu masuluhisho ya nyumbani ambayo wengine wamedai yalifaulu katika kutibu ambukizo la chawa. Hata hivyo, wataalamu wa tiba wa ki-siku-hizi hawapendekezi kunyoa nywele zilizoambukiwa na chawa, wakiliona hilo kuwa lenye kudhuru kisaikolojia na lisilo la lazima. Kunyoa nywele kwapendekezwa tu wakati nywele ni ndefu mno au zimejiviringa mno hivi kwamba kuchanua hakuwezekani. Kuongezea hayo, wataalamu wa tiba leo hawapendekezi mafuta ya taa yatumiwe kichwani. Kwa kielelezo, Profesa David Taplin wa Chuo Kikuu cha Shule ya Tiba ya Miami aliambia “Amkeni!” kwamba kwa maoni yake zoea hilo ni la kikale.—ED.