Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • tr sura 13 kur. 114-121
  • Kanisa La Kweli na Msingi Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kanisa La Kweli na Msingi Wake
  • Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MSINGI WA KANISA LA KWELI
  • “JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU”
  • KANISA LA UMOJA
  • KUTHAMINI KWA KANISA LA KWELI NA MSINGI WAKE
  • Je, Petro alikuwa Papa wa Kwanza?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Urithi wa Upapa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Je, Tuhudhurie Mikutano ya Kikristo?
    Amkeni!—2001
  • Kanisa—Mabadiliko na Mvurugo
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
tr sura 13 kur. 114-121

Sura ya 13

Kanisa La Kweli na Msingi Wake

1. Kwa nini ni jambo la muhimu kuweza kutambua kanisa la kweli na msingi wake?

IKIWA tunataka kuishi milele katika taratibu mpya ya Mungu lazima tukubali kanisa la kweli na msingi wake. Kwa habari yake, Yesu alisema: “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” (Mathayo 16:18) Kanisa hili ni nini na mwamba ambao juu yake limejengwa ni nini? Biblia hutupa sisi majibu ya kweli.

2. (a) Je! Biblia inatumia neno “kanisa” wakati wo wote kwa kumaanisha jengo? (b) Ni nini maana ya neno la Kigiriki?

2 Ijapokuwa watu wengi husema juu ya majengo ambayo katika hayo watu hukutana kwa ibada kama “makanisa,” je! wewe ulijua kwamba Biblia haisemi hivyo kamwe? Katika Biblia neno “kanisa” sikuzote huwa na maana ya watu, hasa kusanyiko au kundi la watu. (Filemoni 2) Neno la Kigiriki ek-kle-siʹa, lililotafsiriwa “kanisa” au “kundi,” maana yake halisi ni “kile kilichoitwa.” Humaanisha kikundi cha watu walioitwa kutoka miongoni mwa wengine kwa kusudi la pekee; lakini hutumiwa kama neno linalofanana na neno la Kiebrania la qahalʹ, likimaanisha “kundi” au “kusanyiko.”

3. Kwa nini kanisa la kweli linafananishwa na (a) mwili wa kibinadamu? (b) msichana bikira aliyeposwa?

3 Kanisa au kundi la kweli hufananishwa na mwili wa kibinadamu, kwa sababu lina washiriki wengi la-kini kichwa kimoja tu, kama vile mwili wa kibinadamu unavyo. Maandiko yaliyoongozwa na roho ya Mungu, katika Waefeso 1:22, 23, hutuambia kwamba Mungu amemfanya Kristo “kichwa juu ya . . . kanisa; ambalo ndilo mwili wake.” Kanisa hili hufananishwa pia na msichana bikira aliyeposwa kwa Kristo, kwa sababu kama kikundi washiriki wa kanisa la kweli wataungana karibu na Kristo, kama vile mke kwa mumewe. Akiandika kwa washiriki fulani wa kanisa, mtume Paulo alisema: “Naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” (2 Wakorintho 11:2; tazama pia Ufunuo 21:2, 9, 10.) Kwa hiyo ni kundi safi, lisilo na uchafu wa kilimwengu na lililojitoa kwa Kichwa chake, Yesu Kristo.

4. (a) Je! mtu ye yote anaweza “kujiunga” na kanisa la kweli kwa kuandikisha jina lake katika kitabu fulani cha kidunia chenye majina ya washiriki? Kwa nini? (b) Ni wangapi waliomo katika kanisa la kweli watakaokuwa pamoja na Kristo mbinguni?

4 Je! mtu ye yote wa kwetu angeweza kuamua “kujiunga” na kanisa hili kwa kuandikisha jina lake katika kitabu fulani chenye majina ya washiriki hapa duniani? La; kama Waebrania 12:23 ielezavyo, hili ni “kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni.” Mungu ndiye mwenye kuchagua washiriki. Yeye huwaweka katika kundi kama yeye apendavyo. (1 Wakorintho 12:18) Hawa ndio watakaokuwa pamoja na Kristo mbinguni. Na Yesu alifunua kwamba, kuliko kutia wote ambao hujidai kuwa Wakristo, wao wana kikomo cha hesabu ya 144,000. —Ufunuo 14:1-3; Luka 12:32.

5. Ni kwa kusudi gani la pekee washiriki wa kanisa la kweli wameitwa?

5 Kweli, wao ni kikundi cha watu walioitwa kutoka katika giza la kiroho kwa kusudi la pekee. Wakati bado wapo duniani wao kwa ujasiri ‘hutangaza fadhili’ za Mungu Aliye Juu sana, aliyewaita kutoka katika giza kuingia katika nuru yake ya ajabu. (1 Petro 2:9) Na, baada ya kufufuka kwao, watakuwa na pendeleo la ajabu la kutawala pamoja na Kristo katika ufalme wake wa kimbinguni.—Luka 22:28-30.

6. (a) Ni nani waliokuwa washiriki wa kwanza wa kanisa la kweli, na jinsi gani ushuhuda ulitolewa kwao kwamba walikuwa wana wa kiroho wa Mungu? (b) Hali ya kuwa mshiriki ilifunguliwa lini kwa wasio Wayahudi?

6 Washiriki wa kwanza wa kanisa hili la kweli wa-likuwa wote Wayahudi (kama vile Yesu na mitume wake walivyokuwa) au waongofu wa Kiyahudi waliotahiriwa. Siku ya Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E. —siku kumi tu baada ya kupaa kwa Yesu mbinguni na kufungua njia kwa wengine wamfuate katika wakati uliowekwa—Yehova alionyesha uchaguzi wake wa washiriki hawa kupitia kwa kumiminwa kwa roho takatifu. Kupokea kwao kwa roho wakati huo kuliwashuhudia kwamba sasa walikuwa wana wa kiroho wa Mungu na warithi wa ufalme pamoja na Kristo. (Matendo 2:1-4, 16-21, 33; Warumi 8:16, 17) Lakini hali ya kuwa mshiriki wa kanisa la kweli haikudumu kuwa ya Wayahudi peke yao. Miaka mitatu na nusu baada ya kufa kwa Yesu njia ilifunguliwa kwa Mataifa au wasio Wayahudi kutiwa ndani. (Matendo 10: 30-33, 44; Warumi 9:23, 24) Hivyo, baadaye, kanisa la kweli lilikuja kuwa na washiriki kutoka mataifa yote.

MSINGI WA KANISA LA KWELI

7. Jinsi gani Yesu na mtume Paulo hutambulisha jiwe la pembeni la msingi la kanisa la kweli?

7 Ni nani aliye msingi wa kanisa la kweli? Yesu Kristo alionyesha wazi kwamba yeye mwenyewe ndiye msingi huo. Yeye alitumia unabii wa Zaburi 118:22 kuwa ukimhusu yeye mwenyewe, akisema: “Jiwe walilolikataa hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.” (Mathayo 21:42-44) Mtume Paulo huongeza ushuhuda wake kwamba Yesu ndiye “jiwe kuu la pembeni,” akiwaandikia Wakristo katika Efeso: “Ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” (Waefeso 2:19, 20) Mtume alisema dhahiri sana juu yake, akisema tena: “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.”—1 Wakorintho 3:11.

8. (a) Kwa nini kusingeweza kuwa na msingi ulio bora zaidi kwa kanisa la kweli kuliko Kristo Yesu? (b) Kunazuka swali gani sasa?

8 Kusingeweza kuwa na msingi ulio bora zaidi na ulio hakika zaidi kwa kanisa la kweli kuliko Kristo Yesu, sivyo? Ni uhai wake mwenyewe mkamilifu wa kibinadamu uliotolewa kama ukombozi ambao huwezesha mpango huu wa kimungu. Lakini, jinsi gani twaweza kupatanisha ushuhuda huu wa Yesu na wa mtume Paulo kwa yale ambayo Yesu alisema kwa Petro katika Mathayo 16:18? Twaweza kuwa hakika kwamba hapana kutopatana.

“JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU”

9. (a) Jinsi gani watu wengine huelewa maneno ya Yesu katika Mathayo 16:18? (b) Je! wingi wa “mababa” wa kwanza wa kanisa walielewa mtajo wa Yesu wa “mwamba” kama ukimhusu Petro?

9 Petro alikuwa ndiyo kwanza amkiri Yesu kuwa Kristo (au, Masihi), Mwana wa Mungu aliye hai. Ndipo Yesu akasema: “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” Wengine huelewa maneno haya kuwa na maana ya kwamba kanisa la Yesu limejengwa juu ya Petro kama msingi. Hii ndiyo hali rasmi ya Kanisa la Kirumi la Katoliki. Lakini inapendeza kuangalia kwamba Askofu mkuu Kenrick, katika kitabu An Inside View of the Vatican Council (cha mwaka wa 1870), huonyesha kwamba kati ya “mababa” wa kanisa wa kwanza wasiopungua themanini na sita, kumi na saba peke yao ndio walioelewa mtajo wa Yesu wa “mwamba” kama ukihusu Petro. Je! wewe ulijua jambo hili?

10. Jinsi gani Augustino alielewa mtajo wa Yesu wa “mwamba”?

10 Kwa mfano, angalia maoni ya Augustino (wa miaka ya 354-430 C.E.), kwa kawaida hutajwa kama “Mtakatifu Augustino.” Ijapokuwa hapo kwanza alikuwa na maoni juu ya Petro kama “mwamba,” baadaye Augustino alibadili nia yake, akisema katika kitabu shake Retractationes: “Tangu wakati huo nimeeleza maneno ya Bwana wetu mara kwa mara: ‘We-we ndiwe Petro na juu ya mwamba huu mimi nitalijenga Kanisa langu,’ kwa kusudi la kwamba yapate kueleweka kama yakimhusu yeye ambaye Petro alimkiri wakati aliposema: ‘Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai,’ . . . Kwa maana yaliyosemwa kwa [Petro] hayakuwa ‘Wewe ndiwe mwamba,’ bali ‘Wewe ndiwe Petro.’ Lakini mwamba alikuwa ni Kristo.”

11. Ni nani ambaye Petro mwenyewe alielewa kuwa ndiye “mwamba”?

11 Lakini jambo la muhimu zaidi sana—Petro mwenyewe alielewaje maneno ya Yesu? Kuhusu Bwana Yesu, Petro alisema: “Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya [kiroho] , ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, na kila amwaminiye hatatahayarika. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. Tena, jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini.” (1 Petro 2:4-8) Maneno haya ya Petro yanaonyesha kwamba yeye, kama mtume Paulo, alielewa Yesu kuwa ndiye “jiwe kuu la pembeni,” “mwamba” ambao juu yake kanisa limejengwa. Petro ni mmoja tu wa 144,000 “mawe yaliyo hai” yaliyomo katika kanisa la kweli.

12. (a) Twajuaje kama Petro alionwa kama kichwa cha kanisa la kwanza “asiyeweza kukosa”? (b) Ni nani ambaye sikuzote hudumu kuwa ndiye kichwa cha kanisa la kweli?

12 Ni kweli kwamba, Petro alifurahia mapendeleo bora kama mtume wa Yesu Kristo. Lakini hakuna mahali ambapo yeye huonyesha kwamba alijiona kuwa mkubwa wa mitume. Wala hatusomi mahali po pote kwamba mitume wengine na wanafunzi walimtambua Petro kama “papa” na wakampa heshima kama hivyo. Pindi moja mtume Paulo aliona lazima kumkaripia Petro (Kefa) waziwazi kwa kuchukua mwendo ulio kinyume cha imani ya kweli ya Kikristo. Jambo la hakika la kwamba Petro alikosa juu ya jambo hili lenye kuhusu imani na maadili na pia kwamba Paulo aliona huru kumrudi waziwazi huonyesha kwamba Petro hakutazamiwa kuwa kichwa “asiyeweza kukosa” cha mitume au cha kanisa la kwanza. (Wagalatia 2:11-14) Katika kanisa la kweli kuna Kichwa kimoja tu, Yesu Kristo, ambaye, tangu kufufuka kwake, yu “akaa milele,” na hivyo hana haja ya wamfuatao nyuma.—Waebrania 7:23-25.

KANISA LA UMOJA

13. (a) Ni maneno gani ya Yesu yaonyeshayo kwamba hapakupaswa pawe na farakano la kundi katika watu ambao ni mapadre na wasio mapadre? (b) Jinsi gani iliwapasa wenye kuongoza katika kundi kuenenda wenyewe?

13 Yesu, Kichwa, haugawanyi mwili wa kundi lake katika jamii ya mapadre na jamii ya watu wasio ma-padre ya “watu wa kawaida.” Yeye husema kwa wafuasi wake: “Ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.” (Mathayo 23:8-10) Ilivyo Yesu anaonyesha kwamba hapana farakano miongoni mwa wale waliomo katika kanisa la kweli. Walakini, alifanya mpango kwa wanaume kuongoza katika kundi la Kikristo, kutumikia mahitaji ya kiroho ya ndugu zao na kutengeneza kazi ya kuhubiri habari njema. Yesu alisema watu wa namna hiyo haikuwapasa ‘kuwatawala kwa nguvu’ ndugu zao bali iliwapasa wawe kama watumwa au watumishi kwao. (Mathayo 20:25-28) Je! jambo hili ni kweli juu ya mapadre ambao unawajua?

14. Kwa nini lazima wale waliomo katika kanisa la kweli wakusanywe katika tengenezo moja tu kwa ibada?

14 I1i kupatana na masimulizi ya Biblia ya kanisa la kweli, wale waliomo lazima wawe na umoja katika ibada yao. Mtume Paulo aliandika kwa habari hii: “Nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu fa-raka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.” (1 Wakorintho 1:10) Hivyo kupatana na Maandiko hatuwezi tukatarajia kuwaona wametawanyika miongoni mwa dini zote zenye kupingana za Kristendomu. Lazima wakusanywe pamoja katika tengenezo moja tu. Kama Waefeso 4:4, 5 husema kwa habari yao: “Mwili mmoja, . . . Bwana mmoja, imani moja.” Ni jambo la muhimu kwetu kujua “imani moja” hiyo ni nini.

KUTHAMINI KWA KANISA LA KWELI NA MSINGI WAKE

15. (a) Jinsi gani Kristo na kundi lake huwafaidi wanadamu watiifu wengine wote? (b) Ni daraka gani ambalo Yesu alisema angetoa kwa kanisa lake la kweli wakati wa kuja kwake katika mamlaka ya Ufalme?

15 Washiriki wa kanisa la kweli chini ya Kristo kichwa chao wanasemekana kuwa “uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.” (Wagalatia 3:29) Ahadi hii ni ya kwamba wengine wote wa wanadamu watiifu watajibariki wenyewe kupitia kwa Kristo na kundi lake. (Mwanzo 22:18) Biblia ilitabiri kwamba, wakati wa kusimamishwa kwa ufalme wa Kristo, kungekuwapo mabaki tu ya watoto hawa wa “Yerusalemu wa juu,” tengenezo la Mungu la kimbinguni, libakilo duniani. (Wagalatia 4:26; Ufunuo 12:10, 17) Yesu alisimulia juu ya washiriki hawa wa kanisa lake duniani kama “mtumwa mwaminifu mwenye akili.” Naye akasema kwamba watu wa namna hiyo waliokutwa wakitumikia kwa uaminifu wakati wa kuja kwake kwenye kazi ya hukumu wangewekwa “juu ya nyumba yake” yaani, juu ya mambo yote ya kidunia yanayohusu ufalme wa Kristo. Wao wangeongoza katika kuhubiri kwa habari njema za Ufalme uliosimamishwa kwa mataifa yote katika “wakati wa mwisho.” —Mathayo 24:14, 45-47; 25:19-23.

16. Ni baraka gani ziwajiao wale ambao huonyesha ukubali unaofaa wa mpango huu?

16 Wale wote ambao leo wanatumaini kupata uzima wa milele katika taratibu mpya ya Mungu lazima wakubali mpango huu. Kwa maana Yesu alisema kwamba, katika huu “wakati wa mwisho,” yeye huwatenga kwenye upande wa kibali wale watendao mema kwa mabaki duniani wa “ndugu” zake, warithi washirika wake waliomo katika kundi la Kikristo. (Mathayo 25:31-40) Hawa ndio mabaki ya “mawe yaliyo hai” ambayo hujengwa katika nyumba au hekalu la kiroho, “mahali pa Mungu pa kukaa kwa roho.” (1 Petro 2:5; Waefeso 2:20-22, NW) Hao ‘watendao mema’ kwa washiriki wa jamii hii ya hekalu husimuliwa katika kitabu cha Ufunuo kama “mkutano mkubwa” wa watu ambao huja chini ya ulinzi wa Mungu. Angalia, pia, kwamba wao kwa furaha humtumikia Mungu “mchana na usiku katika hekalu lake,” yaani, katika ushirika na mabaki ya jamii ya kiroho ya hekalu, kundi la Kikristo.—Ufunuo 7:9, 10, 15.

17. Ni nini ambalo kweli watu walio mfano wa kondoo, husema kwa mabaki ya kanisa la kweli?

17 Kwa kweli, watu hawa walio mfano wa kondoo husema kwa warithi wa ahadi iliyofanywa na Ibrahimu: “Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.” (Zekaria 8:23) Hata kama vile wale wa kanisa la kweli au kundi watembeavyo kwa uaminifu katika nyayo za Kristo na kutangaza ujumbe wa Ufalme, vivyo hivyo watu hawa walio mfano wa kondoo ‘huenda pamoja nao,’ wakimtumikia Mungu pamoja nao. Je! wewe unafanya jambo hilo? Ikiwa ndivyo, unalo taraja la kupokea uzima wa milele duniani, na baraka zote nyingine zitakazotiririka kutoka kwa Kristo na kundi lake lililotukuzwa katika mbingu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki