Kahaba na “Wafalme wa Dunia”
HISTORIA ya Jumuiya ya Wakristo imejaa vielelezo vya kueneza uvutano na kujiingiza-ingiza katika nafasi za mamlaka. Acheni tufikirie vichache. Charlemagne (742-814 W.K.) alikuwa mtawala aliyeona manufaa za kuwa mwenzi mwenye kuoana na dini na kubarikiwa na makasisi wa Kanisa Katoliki.
The New Encyclopcedia Britannica inaeleza kwamba papa alimpaka mafuta Charlemagne, baba yake, na ndugu yake, katika kuweka msingi wa ukoo mpya wa kifalme baada ya ile jamaa iliyokuwa ikitawala ‘kusukumwa kando.’ Halafu inaongezea hivi: “Mapatano ya kisiasa kati ya akina Frank [watu wa Charlemagne] na Papa dhidi ya akina Lombard yalihakikishwa katika pindi hiyo. . . . Charles [ambaye akawa Charlemagne] alikiri mapema kwamba ulikuwako uhusiano wa karibu kati ya mamlaka ya kidunia na kanisa.”
Katika mwaka 800 W.K., Papa Leo 3, “alipiga moyo konde kumfanya Charles awe mmaliki” wa Milki ya Magharibi ya Kiroma, akamvika taji kwenye Misa ya Krismasi katika St. Peter’s, Roma.
Kahaba Mwenye Pupa
Lakini kahaba hutaka malipo. Charlemagne angeweza kumlipa nini mwakilishi wa Babuloni, Roma? “Charles . . . alitaja tena, katika St. Peter’s Basilica, ahadi ya baba yake kuhamisha sehemu kubwa za Italia ziwe za utawala wa papa.” Chanzo icho hicho kinaongezea hivi: “Katika uanadini wake uliowekewa masharti ya kidini, milki na kanisa zilikua zikawa muungano mmoja katika muundo na hali ya kiroho.”
Kielelezo kingine cha uvutano mwingi ambao dini imekuwa nao katika utawala ni Kardinali Wolsey wa Uingereza (1475-1530). Britannica inataarifu kwamba yeye alikuwa “kardinali na mwanaserikali aliyetawala serikali ya Mfalme Henry 8 wa Uingereza. . . . Katika Desemba 1515 Wolsey akawa chansela mheshimiwa wa Uingereza. . . . Wolsey alitumia mamlaka yake kubwa katika mambo ya kilimwengu na ya kidini kujikusanyia utajiri ambao wingi wao ulikuwa wa pili kwa ule wa Mfalme tu.” Kwa kutumia usemi wa Ufunuo ulio wa ufananisho, umalaya wa daraja la juu hudai malipo ya daraja ya juu.
Kielelezo kingine chenye sifa mbaya cha uvutano wa kidini katika mambo ya Serikali kilikuwa kardinali na dyuki wa Richelieu (1585-1642), aliyetumia mamlaka kubwa katika Ufaransa na pia akakusanya utajiri “uliozidi mno hata kwa kupimwa kulingana na viwango vya muda huo,” inataarifu Britannica.
Aliyemfuata Richelieu katika cheo alikuwa kardinali mwingine pia, Jules Mazarin (1602-61), ambaye akawa waziri wa kwanza wa Ufaransa wakati wa utawala wa Mfalme Louis 14. Ingawa hakuwa padri aliyeagizwa rasmi, alifanywa kardinali katika 1641 na Papa Urban 8. Kardinali Mazarin pia alitamani sana utajiri. Ensaiklopedia hiyo inataarifu hivi: “Adui za Mazarin walimsuta kwa pupa yake. Yeye alikuwa amejikusanyia ofisi nyingi na majengo yenye kuleta mapato, na nyakati fulani akachanganya mapato ya mfalme na yake mwenyewe.”
Nyakati za ki-siku-hizi dini bandia ingali ikirundika utajiri na kujaribu kuwatolea wanasiasa uvutano na, ikiwezekana, kuwaongoza. Kielelezo kimoja cha kutokeza ni lile tengenezo la siri la Kikatoliki Opus Dei (kwa Kilatini, Kazi ya Mungu), ambalo kwa sasa lina shangwe ya kupendelewa na papa na, kulingana na mtungaji Lawrence Lader, “limejitoa kabisa kufuata siasa za kupinga ukomunisti na zisizopendelea mabadiliko mengi.” Lina mwongozo wa kuwapitisha vijana Wakatoliki wenye akili bora zaidi katika shule za sekondari na vyuo vikuu kisha kuwaweka wanaume wao katika vyeo vya uvutano na maongozi katika serikali, uchumi, na vyombo vya habari. Katika Hispania walipata ufanisi mkubwa chini ya Franco mtawala mtumia-nguvu wa Kifashisti aliye Mkatoliki wakati ambapo, katika kipindi kimoja, 10 kati ya washiriki 19 wa baraza lake la mawaziri walikuwa washirika wa Opus Dei ya walio bora zaidi.a
Katika United States, waevanjeli wa televisheni wanajulikana kwa utajiri wao mwingi na mitindo-maisha ya anasa. Makasisi fulani Waprotestanti wameingia siasani na hata wakagombea urais. Hakuna shaka kwamba kahaba wa zamani, akiwa chini ya kisingizio cha namna fulani, angali ana shangwe ya kuwa na mapambo na wingi wa mamlaka na hujaribu kutawala akiwa ndiye bwana-mkubwa, ingawa yu katika hali ya kuanguka.—Ufunuo 17:4.
Lakini namna gani jina lile la kahaba, Babuloni Mkubwa? Linasaidiaje kuhakikisha utambulisho wa mwanamke anayefananishwa katika Ufunuo?
[Maelezo ya Chini]
a Ili kupata habari zaidi kuhusu Opus Dei na kujihusisha kwa kanisa katika siasa, ona vitabu Hot Money and the Politics of Debt, cha R. T. Naylor, na Politics, Power, and the Church, cha L. Lader.
[Picha katika ukurasa wa 6]
Makardinali Wolsey, Mazarin, na Richelieu walijirundikia mali nyingi sana walipokuwa wakitumikia Serikali
[Hisani]
Photos: Culver Pictures