Wimbi la Dini Lenye Kuleta Uharibifu Mkubwa—Kutozwa Hesabu Mara ya Mwisho
MIOTO-MIKUBWA, yatoa makelele, cheche zaang’aza, roketi zarushwa juu kuitia anga rangirangi nyekundu, buluu, majano, na chanikiwiti. Viazi katika maganda yazo. Vicheko na makelele ya furaha. Usiku wa Moto-Mkubwa katika Uingereza.
WAFANYA kazi walipata maiti 25 bila kutazamia. Mifupa hiyo mitupu ilikuwa imezikwa kwa uangalifu, mikono ikiwa imekunjwa. Hivyo wanahistoria waligundua bila kutazamia dalili ya fumbo lenye kurudi nyuma kwa miaka yapata 200. Kwibeki, Kanada.
Yaliyo juu ni matokeo mawili yasiyohusiana yaliyo na chanzo kimoja—ule Mgeuzo Mkuu.
MAKALA moja katika toleo letu la Oktoba 1 ilionyesha kwamba Ulaya ilishuhudia msukosuko mkubwa sana wa kidini katika karne ya 16. Matokeo yao yalienea kwenye sehemu nyinginezo za ulimwengu. Pande nyingi za maisha ya kila siku ni mitaro tu iliyoachwa na maji ya ule Mgeuzo Mkuu. Pengine hata yanakuwa na uvutano juu ya kawaida ya kila siku yako. Lililo la maana hata zaidi, sisi tunasimama ukingoni mwa uharibifu mkuu wa kidini wa mwisho ambao kwa hakika utaathiri maisha yako. Je! wewe unajua ni jinsi gani?
Ebu fuatisha mapito ya ule Mgeuzo Mkuu katika nchi zifuatazo:
Ujeremani: Wengine wanasema kwamba uvutano wa Luther juu ya utamaduni wa Kijeremani haulinganiki na wa mtu mwingine ye yote katika ulimwengu unaosema Kiingereza. Tafsiri yake ya Maandiko ni mojapo ya Biblia za Kijeremani zinazokubaliwa mahali pengi zaidi sana. Luther alifanya mengi sana katika kuanzisha matumizi ya maneno bora katika lugha na kuweka msingi kwa mahusiano ya kinyumbani ya Kijeremani. Yeye aliifanya Serikali itambue uhitaji wa elimu kwa wote, akiinua cheo cha kazi ya ualimu.
Kanada: Wakati uliopita wa Kikoloni uliona Uingereza na Ufaransa zikijitia katika msukumano wa kivita ambao uliacha alama yao juu ya mkoa mmoja hasa—Kwibeki. Mwanzoni ukiwa umekaliwa na walowezi-wahamiaji Wakatoliki Wafaransa, Kwibeki ulikuja chini ya Uingereza, na kwa sababu hiyo chini ya uongozi wa Kiprotestanti, katika 1763. Ilikuwa muda mfupi kabla ya hapo kwamba zile maiti zilizotajwa kwenye mwanzo wa makala hii zilizikwa kwa siri karibu na kuta za mji zilizoimarishwa. Kwa sababu gani kwa siri? Kwa sababu zinaelekea kuwa zilikuwa Waprotestanti, ambao katika wakati huo walikuwa wamekatazwa kuzikwa katika maziara ya Kikatoliki. Kwibeki ungali unasimama ukiwa kisiwa cha Ukatoliki wenye kusema Kifaransa, na hilo linazusha harakati za ki-siku-hizi za wanaopendelea utengano.
Ailandi: Bila kuvutiwa na ule Mgeuzo Mkuu, kile Kisiwa Emeraldi kilikaa mbali nao. Baada ya muda kupita, uvutano wa Uprotestanti ulipenya polepole kuvuka Bahari ya Arishi kutoka Uingereza kuingia katika ile mikoa ya kaskazini. Urithi wa hilo ni nchi ya Ailandi iliyogawanyika leo. Miandamano ya kila mwaka wakati wa kiangazi katika Ulster huadhimisha ushindi mbalimbali wa Uprotestanti wa wakati uliopita. Miadhimisho kwa kawaida huacha alama za vizuizi vilivyojengwa, makombora, na risasi za plastiki. Ile Siku ya Mwandamano wa Orange katika Julai 1986 iliacha nyuma watu 160 waliojeruhiwa. Ilikuwa ukumbusho wa ile siku ya miaka yapata 300 iliyopita wakati Mfalme William wa Orange, ambaye alifanya Uprotestanti uimarike katika Uingereza, alipomshinda James wa Pili, mtawala Mkatoliki wa mwisho wa Uingereza.
United States: “[Zile] madhehebu mbali-mbali zenye asili za Ulaya zenye kutofautiana zilikuwa sababu yenye nguvu katika kuleta uhuru wa kidini katika Amerika,” anaandika A. P. Stokes katika kichapo Church and State in the United States. Siku za kikoloni ziliona United States ikiwa imepambwa kwa rangi za Kiprotestanti. Kanuni bora za Calvin zilitoa mwelekezo katika dini, siasa, na uchumi. Ile itikadi ya msingi ilikuwa kwamba kila mtu alisimama katika hali ya kutoa hesabu moja kwa moja kwa Muumba wake bila upatanisho wa kikuhani. Wazo hili lilizaa tabia iliyojitahidi kujifanyia maisha yayo yenyewe, kuvuna thawabu za kazi ngumu yayo yenyewe.
T. H. White anakumbuka katika kitabu chake In Search of History kwamba, mwanzoni mwa karne hii, asilimia 13 ya idadi ya watu wa United States walikuwa Wakatoliki. Uwiano huu ulipanda kufika asilimia zaidi ya 25 kufikia 1960. Hata hivyo, ni Wakatoliki wachache waliofikia vile vyeo vya juu zaidi vya siasa. White anaendelea: “Katika vile viwango vya juu zaidi vya Baraza Kuu, ambapo vita na amani zilifanyizwa, ambapo miafaka na maongozi ya nchi za kigeni yaliamuliwa, ambapo Hukumu za Mahakama Kuu Zaidi zilithibitishwa, bado Waamerika walipendelea Waprotestanti wa ile desturi ya kale wawe walinzi wa mradi wa kitaifa.” Desturi hiyo ilivunjwa wakati John F. Kennedy alipopata kuwa rais Mkatoliki wa kwanza wa United States.
Kwa mifano zaidi ya nchi nyinginezo, tafadhali ona kisanduku.
Mandhari Yaliyotopezwa
Chini ya Uprotestanti, majadiliano ya kitheolojia yaliongezeka na tafsiri za Biblia na vitabu vya maelezo vikaja kuelea juu ya wimbi la uhuru na kujieleza binafsi kwa watu mmoja mmoja. Hata hivyo, wakati ulipoendelea kupita, uhuru ukatokeza juu uchambuzi wa Biblia. Mawazo mapya yakakubaliwa; uamuzi wa kibinafsi wa mambo ukawa ndio kawaida ya maisha. Maendeleo yakawa sasa si ule mpigo mwanana wa mawimbi bali mshindo wa ngurumo za mawimbi ya kuumuka. Lile wimbi lenye nguvu nyingi la mgeuzo mkuu likafagilia mbali misingi yenyewe ya fundisho la Kikristo la kidesturi. Vibadala vya ki-siku-hizi kama vile mageuzi, ukombozi wa wanawake, na ile ‘adili mpya’ vimefagiliwa mbali kama vile miti iliyokauka ifagiliwavyo na maji, vikiwa mashahidi walio kimya kwa dhoruba hiyo. Dini zilizofanywa kuwa za mtu binafsi katika nchi fulani za Kiprotestanti ziliacha watu mmoja mmoja bila kujua la kufanya, wametupwa kila mmoja katika kisiwa chake mwenyewe cha upweke wa imani.
Hali katika maeneo ya Kiprotestanti inafinyangwa na mavutano ya mwelekeo wa akili wenye nguvu wa kutilia shaka kawaida zilizosimamishwa imara. Watu wanalelewa juu ya itikadi ya maendeleo, uhuru, na haki za kibinadamu. Max Weber, mtaalamu wa elimu ya kijamii na uchumi Mjeremani, alichapisha insha moja katika 1904 juu ya Uprotestanti na Ubepari. Yeye alitaarifu kwamba Ubepari haukuwa tu tokeo la ule Mgeuzo Mkuu. Lakini yeye aligundua kwamba katika maeneo yenye ubepari uliofanikiwa ya mazingira yaliyochangamana ya kidini, kwa kutokeza sana Waprotestanti ndio waliokuwa wenyeji, viongozi, wastadi, na wenye elimu. Kulingana na kichapo Der Fischer Weltalmanach, kati ya zile zawadi za Nobeli 540 zilizotolewa kufikia 1985, theluthi mbili zilienda kwa wananchi kutoka tamaduni za Kiprotestanti. Wakaaji wa mazingira ya Kikatoliki walishinda asilimia 20 tu. Kati ya yale mataifa 20 ya kiwango cha juu kwa habari ya jumla ya zao la kitaifa kwa kila mtu, tisa yalikuwa ya Kiprotestanti, mawili ya Kikatoliki. Kwa upande mwingine, kati ya nchi kumi changa zilizoorodheshwa zenye madeni, tano zilikuwa za Kikatoliki, hakuna ya Kiprotestanti.
Gazeti la habari la kila juma la Ujeremani Der Spiegel liliandika kwamba mawazo ya Calvin yalisukuma Uingereza ikawa mamlaka yenye nguvu ya ulimwengu. Tangu karne ya 19, nguvu ya kisiasa iliyoongezeka ya United States, Ujeremani na Uingereza zikawa kani za kufanyiza upya hali za kijamii. Usawa wa nafasi kwa wote ulitiliwa mkazo. Mizingo-mizingo ndani ya mkondo mkubwa wa ule Mgeuzo Mkuu inaonwa na wengine kuwa vitangulizi vya usoshalisti wa ki-siku-hizi. Ufahamu wa kisiasa wa daraka la kijamii ulitayarisha njia kwa serikali zenye kutimiza masilahi ya raia. Hasa katika mazingira ya Kiprotestanti, mamlaka za kiserikali polepole zilichukua maongozi ya mambo ya kisheria ya uzaliwa, kifo, ndoa, talaka, na urithi. Upatikanaji wa talaka na utoaji mimba unaoruhusiwa kisheria sasa mara nyingi unatofautiana sana katika nchi za Kikatoliki na za Kiprotestanti.
Nguzo mbili ambazo zimeutegemeza Uprotestanti, United States na Uingereza, zilikua pamoja zikawa yule mnyama mwenye pembe mbili wa unabii wa Biblia. (Ufunuo 13:11) Jitu kubwa la kisiasa la karne ya 20, lile tengenezo la Umoja wa Mataifa, lililoitwa hapo kwanza Ushirika wa Mataifa, lilisitawi kutokana na mianzo ya Kiprotestanti.
Ile Gharika Itarudi
Wimbi la maji yenye kupwa linaacha nyuma alama ya wimbi la maji juu ya ufuo wa bahari ambalo hukumbusha sisi juu ya kurudi kwalo kunakokuja. Hali moja na hiyo, ule Mgeuzo Mkuu wa karne ya 16 uliacha nyuma alama zenye kuonekana ambazo sisi tunaweza kuona leo. Na kuna ushuhuda wenye nguvu kwamba sisi tunasimama ukingoni mwa wimbi la kukata maneno la badiliko la kidini ambalo litapita mabadiliko yote yaliyotangulia, likifagalia mbali dini isiyo ya kweli kwa umilele, na kuleta mabadiliko katika hali ya kila mmoja anayeisha. Je! wewe utaliokoka? Ulimwenguni pote, kuna hali ya kutotosheka na dini iliyopangwa kitengenezo yenye msingi uliosambaa miongoni mwa watu mmoja mmoja na serikali. Sababu ni nini ya hali hiyo ya kutotosheka?
Dini mara nyingi inapita mamlaka yayo ya kiroho, ikichanganya dini na siasa, ikichukua cheo cha kisiasa na cha kidini, ikitumia mamlaka ya kisiasa na ya kidini. Miaka kadha iliyopita karatasi ya habari ya Jumapili Observer ilizusha swali juu a kama wanasiasa katika Ailandi walikuwa tayari kutwaa mamlaka ya kuongoza nchi kutoka kwa makasisi. Aliyekuwa hapo kwanza kiongozi wa Ujeremani Magharibi Helmut Schmidt alieleza juu ya kujiingiza kwa dini katika siasa kwa kusema, “Mimi siitikadi kwamba hilo linaweza kuruhusiwa kwa muda usiojulikana.” Na Le Figaro la Paris lilishtakia kanisa “kujidukiza katika siasa” sana hivi kwamba “liko katika hatari ya kuona siasa zikijidukiza katika dini.” Kuanzia India mpaka Misri mpaka United States, kuanzia Polandi mpaka Nicaragua, Malesia mpaka Chile, lile shindano lenye kuchosha kati ya siasa na dini linaendelea.
Hili halishangazi, si jambo jipya. Ufunuo sura ya 17 huieleza dini yote nzima isiyo ya kweli kuwa kahaba, Babuloni Mkuu, ambaye hufanya uasherati pamoja na wanasiasa wa dunia. Mstari wa 4 (HNWW) humfananisha zaidi akiwa “amejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu.” Milki ya kidini haitosheki, ikigaagaa katika anasa, ikichuruza utajiri. Katika karne ya 16, ule utajiri wenye kumetameta wa Kanisa Katoliki ulivuta macho yenye kutamani. Ndivyo ilivyo kwa habari ya mali yenye kupambwa kwa almasi ya dini yote katika karne yetu ya 20.
Tayari serikali zinatupa macho yenye kutamani kuelekea utajiri huu. Albania iliona ile misikiti, makanisa, na majengo mengine ya kidini zaidi ya 2,000, na ama ikayataifisha au kuyabomoa. Gazeti Sunday Times liliripoti katika 1984 kwamba serikali ya Malta “ilianza kuukazia macho utajiri wa kanisa,” ikakata misaada ya kifedha inayotolewa na serikali kwa mashule ya kanisa. Alipoulizwa jinsi kanisa lapaswa kulipia hasara hiyo, waziri mmoja wa serikali alijibu hivi: “Ikihitajiwa, wao wanaweza kuyeyusha misalaba yao ya dhahabu na maaltare ya fedha.” Kanisa la Orthodoksi la Kigiriki lilikubali katika 1986 kutoa kwa masharti kwa serikali mashamba lililokuwa nayo (asilimia 10 ya eneo la nchi). Kwa sababu gani ukarimu huu? Kwa sababu ya mwongozo wa serikali wa ‘kutumia mali ya kanisa kwa shughuli za kijamii.’
Ulimwenguni pote, dini ni kitamaushi kikubwa. Badala ya kuunganisha, inapasua. Karatasi ya habari moja ya kila siku ya Kijeremani ilitaja ule “ushindani kati ya Wakatoliki na Waprotestanti ambao unakuwa sawa na chuki.” Frankfurter Allgemeine Zeitung liliandika kwamba hata harakati za ekumeni, zinazokusudiwa kuziba pengo, zilianza kutokana na hali ya “kushukiana, uadui usiopatanika kati ya Wakatoliki na Waprotestanti.” Elie Wiesel, mshindi wa Zawadi ya Nobeli ya Amani ya 1986, alinakiliwa katika gazeti jingine la kila siku la Kijeremani kuwa akisema: “Mimi mara nyingi nafikiri tumeshindwa. Ikiwa mtu fulani angekuwa ametuambia katika 1945 kwamba sisi tungeona tena vita vilivyochochewa kidini vikipiganwa katika karibu kila bara . . . sisi hatungeitikadi hilo.” Dini ambayo huanzisha matata, inayochochea au kukubali vita, ni dini mbaya. Si ya kweli. Na Muumba aliamua muda mrefu uliopita kuifutilia mbali.
Sura ya 17 ya Ufunuo haiachi shaka lo lote kwa habari ya kitakaloipata dini yote mbaya. Katika mstari wa 16 tunasoma hivi: “Na zile pembe kumi [mamlaka za kiserikali ndani ya tengenezo la Umoja wa Mataifa] ulizoziona, na huyo mnyama [Umoja wa Mataifa], hao watamchukia yule kahaba [dini isiyo ya kweli], nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.”
Wewe Wasimama Wapi?
Hata lionekane kuwa jambo la kushangaza namna gani, dini isiyo ya kweli imekwisha. Mazoea, desturi, mapokeo, na mapendeleo yayo yatatoweka karibuni. Huenda hilo likaonekana kwako kuwa jambo lisiloelekea kutukia kama vile kutopezwa kwa Kanisa Katoliki lilivyokuwa kwa watu katika karne ya 16. Lakini yale maji ya Mgeuzo Mkuu yalikuwa yenye kulemea. Utajiri wa kanisa uliwaendea watu, mamlaka yayo ikawaendea watawala. Vivyo hivyo katika siku yetu, mataifa yatasimamia kuangamizwa kwa mwisho kwa dini isiyo ya kweli.
Hilo linamaanisha nini kwako binafsi? Chunguza tengenezo la kidini unaloshirikiana nalo. Je! yale mambo linalofundisha yanapatana na Biblia katika kila njia? Ikiwa sivyo, basi tengenezo lako ni sehemu ya ‘Babuloni Mkuu,’ au ile milki ya dini isiyo ya kweli. Fuata ile amri inayopatikana katika Ufunuo 18:4, ambayo ni: “Tokeni kwake, enyi watu wangu, . . . msipokee mapigo yake.”
Kumbuka, lile wimbi linaloleta uharibifu mkubwa wa kukata maneno kwa dini isiyo ya kweli linakuja. Linaweza kuonekana kwenye upeo wa macho. Wewe utakuwa unasimama wapi litakapoleta uharibifu walo wenye kishindo? Katika bonde la kutojali? Juu ya kilima cha mamlaka fulani ya kilimwengu? Au juu ya mlima wa Yehova? Kuna mahali pamoja tu pa kuwa penye usalama.
[Blabu katika ukurasa wa 27]
Wimbi lenye nguvu nyingi la Mgeuzo lilifagilia mbali ile misingi yenyewe ya fundisho la kidesturi. Vibadala kama vile mageuzi, ukombozi wa wanawake, na ile ‘adili mpya’ vimefagiliwa mbali kama miti iliyokauka ifagiliwavyo na maji
[Blabu katika ukurasa wa 28]
Kuna ushuhuda wenye nguvu kwamba sisi tunasimama ukingoni mwa wimbi la kukata maneno la badiliko la kidini. Je! wewe utaliokoka?
[Blabu katika ukurasa wa 29]
Ikiwa mtu fulani angekuwa ametuambia katika 1945 kwamba sisi tungeona tena vita vilivyochochewa kidini vikipiganwa katika kila bara, sisi hatungeitikadi hilo
[Sanduku katika ukurasa wa 29]
Afrika Kusini: Itikadi ya Ukalvini ya kuandikiwa kimbele mambo yatakayopata mtu iliupa ubaguzi wa rangi msingi wa kitheolojia. Gazeti la kila siku la Kijeremani Frankfurter Allgemeine Zeitung liliwaita wanatheolojia wa—Reformed Church katika Afrika Kusini, “wachoraji ramani wa siasa za ubaguzi wa rangi.”
Switzerland: Ikiwa ndiyo kitovu cha harakati za Ukalvini, Geneva ulivutia maelfu mengi ya wakimbizi, ambao walikuja pamoja na utajiri na ujuzi. Kama tokeo, huu ungali ni mji mkubwa wa biashara ya benki na wa kiwanda chenye kusitawi cha kutengenezea saa-kiwiko na vipima-wakati.
India: Ile Sosaiti ya Yesu (Wayesuiti) ilikua ikiwa sehemu ya Upingaji Mgeuzo Mkuu, harakati ya kufufua Ukatoliki kufuatia mabadiliko ya Mgeuzo Mkuu. Washiriki wa sosaiti walikuja kwenye mkoa Goa katika karne ya 16, muda mfupi baada ya kufanywa kwayo kuwa koloni na Ureno. Uvutano wa kanisa unaonekana katika idadi ya watu leo: Katika Goa, watu 3 kati ya 10 ni Wakatoliki, hali katika India kwa ujumla, mtu 1 tu katika 25 hudai kuwa Mkristo.
Uingereza: Mwaka 1605 uliona James I, Mprotestanti, akikalia kiti cha ufalme. Kadiri uonezi juu ya Wakatoliki katika nchi hiyo ulivyokua, njama ilitungwa ya kulipua Bunge, kutia na Mfalme. Wale wananjama, kikundi cha Wakatoliki walioongozwa na Guy Fawkes, walifunuliwa na kuuawa. Novemba 5 hutia alama ya mwadhimisho wa Usiku wa Moto-mkubwa. Jamaa na marafiki bado hukusanyika kupasha moto jioni yenye unyevu-nyevu kwa milipuko ya baruti na kumchoma “guy,” au mfano, wa yule mfanyiza njama.
[Pichas katika ukurasa wa 26]
Martin Luther na John Calvin—viongozi katika ule Mgeuzo Mkuu