Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 3, 1992
MKUTANO WA KILA MWAKA wa washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania utafanywa siku ya Oktoba 3, 1992, kwenye Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova, 2932 Kennedy Boulevard, Jersey City, New Jersey. Mkutano wa utangulizi wa washirika peke yao utafanywa saa 3:30 asubuhi, ukifuatwa na ule mkutano wa ujumla wa kila mwaka saa 4:00 asubuhi.
Washirika wa Shirika hilo wanapaswa kuijulisha Ofisi ya Mwandishi sasa juu ya badiliko lolote lililotokea mwaka uliopita katika anwani zao za barua ili barua zile za kawaida za ujulisho na uwakilishaji ziweze kuwafikia muda mfupi baada ya Agosti 1.
Barua za uwakilishaji, watakazopelekewa washiriki pamoja na ujulisho wa mkutano wa kila mwaka, zinapasa kurudishwa ili ziifikie Ofisi ya Mwandishi wa Sosaiti si baada ya Agosti 15. Inampasa kila mshiriki ajaze mambo yote yaliyo katika barua ya uwakilishaji na kuirudisha haraka, akitaarifu kama atakuwapo ama hatakuwapo mkutanoni yeye binafsi. Habari zenye kutajwa katika kila barua ya uwakilishaji zinapasa kusema jambo hilo waziwazi, kwa kuwa ndizo zitakazotegemewa katika kujua ni akina nani watakaokuwapo binafsi.
Inatarajiwa kwamba kipindi kizima, kutia ndani mkutano ule rasmi wa kishughuli na ripoti mbalimbali, kitamalizwa ifikapo saa 7.00 alasiri au muda mfupi baada ya hapo. Hakutakuwa na kipindi cha alasiri. Kwa sababu nafasi ni ndogo, itawezekana kuingia kwa kuwa na tikiti tu. Hakutakuwa na mipango ya kuunganisha mahali pengine-pengine kwa kamba za simu ili kuusikia mkutano wa kila mwaka.