Maisha na Huduma ya Yesu
Yesu Akemea Mafarisayo
IKIWA ni kwa uwezo wa Shetani yeye anafukuza mashetani, Yesu anatoa hoja yake, basi Shetani amegawanyika dhidi yake mwenyewe. “Ama ninyi watu mfanye mti uwe mzuri sana na tunda lao liwe zuri sana,” yeye anaendelea kusema, “au mfanye mti uoze na tunda lao lioze; kwa maana mti unajulikana kwa tunda lao.”
Ni upumbavu kutoa shtaka la kwamba tunda jema la kutupa nje mashetani linatokea kwa sababu Yesu anatumikia Shetani. Ikiwa tunda ni zuri sana, mti hauwezi kuwa umeoza. Kwa upande ule mwingine, tunda lililooza la Mafarisayo la mashtaka ya upuuzi na upinzani usio na msingi kwa Yesu ni uthibitisho wa kwamba wao wenyewe wameoza. “Wazao wa nyoka wenye sumu,” Yesu anapaaza sauti, “mnaweza kunenaje mambo mema, hali ninyi wenyewe ni waovu? Kwa maana kinywa hunena kutokana na utele wa moyo.”
Kwa kuwa maneno yetu yanaonyesha hali ya mioyo yetu, tunayosema yanaandaa msingi wa hukumu. “Mimi nawaambia ninyi,” Yesu anasema, “kwamba kila usemi usioweza kuleta faida ambao wanadamu wananena, wao watatoa hesabu kuuhusu katika Siku ya Hukumu; kwa maana kwa maneno yenu ninyi mtatangazwa kuwa waadilifu, na kwa maneno yenu mtalaaniwa.”
Zijapokuwa kazi zote za ajabu alizofanya Yesu, waandishi na Mafarisayo wanaomba hivi: “Mwalimu, sisi tunataka kuona ishara moja kutoka kwako wewe.” Ingawa huenda watu hawa hasa kutoka Yerusalemu hawajajionea wao wenyewe miujiza yake, upo ushahidi usiopingika wa wale waliojionea kwa macho yao wenyewe miujiza hiyo. Kwa hiyo Yesu anawaambia viongozi hao Wayahudi: “Kizazi kiovu na chenye uzinzi kinaendelea kutafuta ishara, lakini hakuna ishara kitakayopewa isipokuwa ishara ya Yona nabii.”
Akieleza analomaanisha, Yesu anaendelea kusema: “Sawa na vile Yona alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa sana michana mitatu na mausiku matatu, ndivyo Mwana wa mtu atakavyokuwa katika moyo wa dunia michana mitatu na mausiku matatu.” Baada ya kumezwa na samaki huyo, Yona alitoka nje kama kwamba amefufuliwa, na ndivyo Yesu anavyotabiri kwamba yeye atakufa na siku ya tatu ainuliwe akiwa hai. Hata hivyo viongozi hao Wayahudi, hata Yesu anapofufuliwa baadaye wanaikataa “ishara ya Yona.”
Hivyo Yesu anasema kwamba watu wa Ninawi waliotubu kwa kusikia mahubiri ya Yona watainuka katika hukumu kulaani Wayahudi wanaokataa Yesu. Vivyo hivyo, yeye anatokeza ulinganifu pamoja na malkia wa Sheba, aliyekuja kutoka miisho ya dunia asikie hekima ya Sulemani naye akastaajabishwa na aliyoona na kusikia. “Lakini, tazama!” Yesu anasema, “kitu fulani kilicho zaidi ya Sulemani kipo hapa.”
Ndipo Yesu anapotoa mfano wa mwanamume anayetokwa na roho mchafu. Hata hivyo, mwanamume huyo hajazi utupu uliobaki kwa mambo mema na kwa hiyo anapagawa na roho saba waovu zaidi. “Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia na kizazi hiki kiovu,” Yesu anasema. Taifa la Israeli lilikuwa limesafishwa uchafu na likapata maumbo mapya—kama mwondoko wa muda wa roho mchafu. Lakini taifa hilo linapokataa manabii wa Mungu, jambo ambalo linafikia upeo kwa kumpinga Kristo mwenyewe, linafunua hali mbovu lililo nayo kuwa mbaya zaidi ya ilivyokuwa mwanzoni.
Wakati Yesu anapoendelea kunena, mamaye na ndugu zake wanafika na kusimama kwenye ukingo wa kutano la watu. Kwa hiyo mtu fulani anasema: “Tazama! Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wakitafuta kunena na wewe”
“Ni nani mama yangu, na ni nani ndugu zangu?” Yesu anauliza. Akinyosha mkono wake kuelekea wafuasi wake, yeye anasema. “Tazama! Mama na ndugu zangu! Kwa maana mtu ye yote anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu.” Kwa njia hiyo Yesu anaonyesha kwamba hata viwe ni vyenye thamani kama nini vifungo vinavyomfunganisha yeye kwa watu wa ukoo wake, wenye thamani hata zaidi ni uhusiano wake na wafuasi wake. Mathayo 12:33-50, NW; Marko 3:31-35; Luka 8:19-21.
◆ Mafarisayo walishindwaje kufanya mti na tunda lao pia liwe zuri sana?
◆ “Ishara ya Yona” ilikuwa nini, na ilikataliwaje?
◆ Taifa la Israeli lilikuwaje kama mwanamume aliyetokwa na roho mchafu?
◆ Yesu alikaziaje uhusiano wake wa karibu pamoja na wanafunzi wake?