Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uadilifu Si kwa Mapokeo ya Mdomo
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Oktoba 1
    • 12. (a) Yesu alifanya badiliko gani la kuiacha njia yake ya kawaida ya kutoa utangulizi wenye kurejezea Maandiko ya Kiebrania katika Mahubiri yake juu ya Mlima, na kwa nini? (b) Twajifunza nini kutokana na utumizi wa sita wa usemi “Imesemwa”?

      12 Yesu aliponukuu kutokana na Maandiko ya Kiebrania hapo kwanza, alisema hivi: “Imeandikwa.” (Mathayo 4:4, 7, 10) Lakini mara sita katika yale Mahubiri juu ya Mlima, alifanya utangulizi wa zile zilizosikika kama taarifa za kutoka kwenye Maandiko ya Kiebrania kwa maneno haya: “Ilisemwa.” (Mathayo 5:21, 27, 31, 33, 38, 43, NW) Kwa nini? Kwa sababu alikuwa akirejezea Maandiko kama yalivyofasiriwa kulingana na mapokeo ya Kifarisayo yaliyopinganisha amri za Mungu. (Kumbukumbu 4:2; Mathayo 15:3) Hilo laonyeshwa wazi katika rejezo la Yesu la sita lililo la mwisho katika mfululizo huu: “Mmesikia [mlisikia, NW] kwamba imenenwa [ilisemwa, NW], Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako.” Lakini hakuna sheria yoyote ya Kimusa iliyosema, “Umchukie adui yako.” Waandishi na Mafarisayo ndio waliosema hivyo. Hiyo ilikuwa ndiyo fasiri yao ya Sheria ya kupenda jirani yako—jirani yako Myahudi, hakuna wengine.

  • Uadilifu Si kwa Mapokeo ya Mdomo
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Oktoba 1
    • 16. Ni zoea gani la Kiyahudi lililofanya kuapa viapo kukose maana, na Yesu alichukua msimamo gani?

      16 Kwa kufuata ukanda ule ule Yesu aliendelea hivi: “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usizuri [usiape bila kufanya, NW] . . . lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa.” Kufikia wakati huu Wayahudi walikuwa wakivunja heshima ya kiapo wakawa wakiapa-apa viapo vingi juu ya vijambo visivyo vya maana bila kuvifanya. Lakini Yesu alisema: “Usiape kabisa . . . Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo.” Kanuni yake ilikuwa sahili: Sema ukweli nyakati zote, bila kulazimika kuhakikisha neno lako kwa kiapo. Acha viapo vibakie kwa mambo yaliyo muhimu.—Mathayo 5:33-37; linganisha 23:16-22.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki