“Mahali Pamoja Baada ya Pengine Magonjwa ya Kuambukiza”
KWA maneno hayo yaliyo juu, yapatikanayo kwenye Luka 21:11, ongezeko la magonjwa ya kuambukiza lapewa kuwa moja ya sehemu kuu za ile ishara ya siku za mwisho. Kwenye Ufunuo 6:8, magonjwa hayo ya kuambukiza yafananishwa mapema na mwendesho wa farasi wa kijivujivu, yule farasi wa nne wa Ufunuo sura 6. Mwandika-safu Lawrence Hall alitokeza mambo makuu kutoka kitabu kipya cha Andrew Nikiforuk chenye kichwa The Fourth Horseman: A Short History of Epidemics, Plagues, Famine and Other Scourges. Yalitokea katika safu ya Hall katika Newark, New Jersey, Star-Ledger, Februari 25, 1994. Madondoo kutoka safu hiyo ni haya yafuatayo.
“Mpanda-farasi Wa Nne wa Apokalipsi anapiga shoti kwelikweli nyakati hizi za uhitaji mkubwa. Wanadamu wamo hatarini kwa zaidi ya njia moja—hata kujapokuwa na tekinolojia na maendeleo yote mapya kabisa ya kustaajabisha katika sayansi za kitiba. Viuavijasumu vingi, ambavyo wakati mmoja vilishangiliwa kuwa dawa za maajabu, hazifui dafu mbele ya viini hodari zaidi vya leo. . . .
“‘Ingawa . . . dawa na chanjo huenda zikaonekana tu ni kama zaweza mambo, magonjwa ya kuambukiza yataendelea kukumbusha halaiki za watu kwamba ile sayansi kifaranga (ya kitiba) ingali imefungwa nepi, na labda iliyo chafu’ . . . Sina madhumuni ya kukuogopesha, lakini lile tatanisho la Mpanda-farasi Wa Nne ni halisi sana. Kifua kikuu chaongezeka tena. Virusi ya UKIMWI yaendelea kuua maelfu kwa maelfu kila mwaka tufeni pote . . . Magonjwa mengine kama homa ya matumbo, diftheria, kipindupindu, anthraksi na malaria yaongezeka kwa kutisha—kuhangaisha sana wataalamu wa afya na umma kwa jumla. . . .
“Kila kipindi cha kihistoria katika wanadamu kimezalisha magonjwa mapya. . . . Kile kipindi cha Mwerevuko kilikuwa na kaswende, ndui iliandamana na Columbus kwenye mabara ya Amerika, na sasa UKIMWI watutisha tena. . . . Na bado, kuna mapigo mapya na maambukizo makubwa yenye kufoka kadiri wanadamu waonekanavyo wakishindwa kudhibiti viini vidogo. . . . Idadi ya watu wenye mifumo ya kinga iliyokandamizwa inaongezeka.” Nikiforuk pia asema kwamba “‘mmojapo uongo mkubwa wa karne ya 20 [ni] kwamba viuavijasumu, chanjo na madaktari wametuokoa na magonjwa ya kuambukiza. . . .
“‘Hata tujaribu kadiri gani, hatuwezi kushinda vile viini hodari, kuhonga yule Mpanda-farasi wala kupuuza kuwapo kusikobadilika kwa magonjwa ya kuambukiza katika historia.’”