Maswali ya Funzo Katika Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Hadithi ya 1
Mungu Anaanza Kuumba Vitu
Vitu vyote vizuri vimetoka wapi, unaweza kutaja kitu kimoja kizuri?
Mungu alimwumba nani kwanza?
Kwa nini malaika wa kwanza alikuwa wa pekee?
Elezea jinsi dunia ilivyoonekana mwanzoni?
Mungu alifanya nini kwanza ili kutayarisha dunia kwa ajili ya wanyama na wanadamu?
Maswali ya ziada:
Soma Yeremia 10:12.
Ni sifa gani za Mungu zinazoonekana katika uumbaji wake? (Isa. 40:26; Rom. 11:33)
Soma Wakolosai 1:15-17.
Yesu alihusikaje katika kuumba, na kwa hiyo, tunapaswa kumwonaje? (Kol. 1:15-17)
Soma Mwanzo 1:1-10.
Dunia ilitoka wapi? (Mwa. 1:1)
Ni jambo gani lililotokea katika siku ya kwanza ya uumbaji? (Mwa. 1:3-5)
Eleza mambo yaliyotokea katika siku ya pili ya uumbaji. (Mwa. 1:7, 8)
Hadithi ya 2
Bustani Nzuri
Mungu alitayarishaje dunia kuwa makao yetu?
Mungu aliwaumba wanyama gani mbalimbali? (Ona picha.)
Kwa nini bustani ya Edeni ilikuwa ya kipekee?
Mungu alitaka dunia nzima iwe nini hatimaye?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 1:11-25.
Mungu aliumba nini katika siku ya tatu ya uumbaji? (Mwa. 1:12)
Ni jambo gani lililotokea katika siku ya nne ya uumbaji? (Mwa. 1:16)
Mungu aliwaumba wanyama wa aina gani katika siku ya tano na siku ya sita? (Mwa. 1:20, 21, 25)
Soma Mwanzo 2:8, 9.
Mungu aliweka miti miwili gani ya kipekee katika bustani, nayo iliwakilisha nini?
Hadithi ya 3
Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza
Kuna tofauti gani kati ya picha ya Hadithi ya 3 na picha ya Hadithi ya 2?
Ni nani aliyemwumba mtu wa kwanza, na mtu huyo aliitwa nani?
Mungu alimpa Adamu kazi gani ya kufanya?
Kwa nini Mungu alimfanya Adamu alale usingizi mzito?
Adamu na Hawa wangaliweza kuishi kwa muda gani, na Yehova alitaka wafanye kazi gani?
Maswali ya ziada:
Soma Zaburi 83:18.
Jina la Mungu ni nani, na ana cheo gani cha pekee juu ya dunia? (Yer. 16:21; Dan. 4:17)
Soma Mwanzo 1:26-31.
Soma Mwanzo 2:7-25.
Adamu alihitaji kufanya nini ili awape wanyama majina yaliyofaa? (Mwa. 2:19)
Andiko la Mwanzo 2:24 linatusaidiaje kuelewa maoni ya Yehova kuhusu ndoa, kutengana, na talaka? (Mt. 19:4-6, 9)
Hadithi ya 4
Sababu Walipoteza Makao Yao
Ni nini kinachowapata Adamu na Hawa kama unavyoona katika picha hii?
Kwa nini Yehova aliwaadhibu?
Nyoka alimwambia Hawa nini?
Ni nani aliyemfanya nyoka aseme na Hawa?
Kwa nini Adamu na Hawa hawakuruhusiwa kuendelea kuishi katika Paradiso?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 2:16, 17 na 3:1-13, 24.
Swali ambalo nyoka alimwuliza Hawa lilitoa wazo gani baya kumhusu Yehova? (Mwa. 3:1-5; 1 Yoh. 5:3)
Mwenendo wa Hawa ni onyo kwetu kwa njia gani? (Flp. 4:8; Yak. 1:14, 15; 1 Yoh. 2:16)
Adamu na Hawa walisema nini kuonyesha kwamba hawakukubali kwamba walifanya makosa? (Mwa. 3:12, 13)
Makerubi waliowekwa upande wa mashariki wa bustani ya Edeni waliungaje mkono enzi kuu ya Yehova? (Mwa. 3:24)
Soma Ufunuo 12:9.
Shetani amefaulu kwa kadiri gani kuwafanya watu wapinge utawala wa Mungu? (1 Yoh. 5:19)
Hadithi ya 5
Maisha ya Taabu Yanaanza
Maisha ya Adamu na Hawa yalikuwaje nje ya bustani ya Edeni?
Ni nini kilichowapata Adamu na Hawa, na kwa sababu gani?
Kwa nini watoto wa Adamu na Hawa wangezeeka na kufa?
Ikiwa Adamu na Hawa wangalimtii Yehova, maisha yao na ya watoto wao yangalikuwaje?
Hawa alipatwa na maumivu gani kwa sababu hakumtii Mungu?
Wana wawili wa kwanza wa Adamu na Hawa waliitwa nani?
Wale watoto wengine katika picha ni nani?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 3:16-23 na 4:1, 2.
Maisha ya Adamu yaliathiriwaje kwa sababu udongo ulilaaniwa? (Mwa. 3:17-19; Rom. 8:20, 22)
Kwa nini jina la Hawa, linalomaanisha “Anayeishi,” lilimfaa? (Mwa. 3:20)
Hata baada ya Adamu na Hawa kufanya dhambi, Yehova aliwaonyeshaje fadhili? (Mwa. 3:7, 21)
Soma Ufunuo 21:3, 4.
Ni ‘mambo gani ya zamani’ ambayo unatazamia kwa hamu kuyaona yakiondolewa?
Hadithi ya 6
Mwana Mzuri, na Mbaya
Kaini na Habili wanafanya kazi gani?
Kaini na Habili wanamletea Yehova zawadi gani?
Kwa nini Yehova anapendezwa na zawadi ya Habili, na kwa nini hapendezwi na zawadi ya Kaini?
Kaini ana sifa gani, na Yehova anajaribu kumsahihisha kwa njia gani?
Kaini anafanya nini yeye na ndugu yake wanapokuwa shambani?
Eleza mambo yaliyompata Kaini baada ya kumwua ndugu yake.
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 4:2-26.
Yehova alifafanuaje hali hatari iliyomkabili Kaini? (Mwa. 4:7)
Kaini alionyeshaje kilichokuwa moyoni mwake? (Mwa. 4:9)
Maoni ya Yehova ni nini kuhusu umwagaji wa damu isiyo na hatia? (Mwa. 4:10; Isa. 26:21)
Soma 1 Yohana 3:11, 12.
Kwa nini Kaini alkasirika sana, na jambo hilo ni onyo kwetu kwa njia gani? (Mwa. 4:4, 5; Met. 14:30; 28:22)
Biblia inaonyeshaje kwamba tunaweza kuendelea kuwa washikamanifu hata ikiwa watu wote wa familia yetu wanampinga Yehova? (Zab. 27:10; Mt. 10:21, 22)
Soma Yohana 11:25.
Yehova anaahidi nini kuwahusu wote wanaokufa kwa ajili ya uadilifu? (Yoh. 5:24)
Hadithi ya 7
Mtu Hodari
Henoko alikuwa tofauti na watu wengine kwa njia gani?
Kwa nini watu walioishi siku za Henoko walifanya mambo mengi mabaya?
Watu walifanya mambo gani mabaya? (Ona picha.)
Kwa nini Henoko alihitaji kuwa hodari?
Watu waliishi kwa muda gani siku hizo, lakini Henoko aliishi miaka mingapi?
Watu walizidi kufanya nini baada ya kifo cha Henoko?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 5:21-24, 27.
Soma Mwanzo 6:5.
Hali ikawa mbaya kadiri gani duniani baada ya Henoko kufa, na hali hiyo inafananaje na siku zetu? (2 Tim. 3:13)
Soma Yuda 14, 15.
Wakristo leo wanawezaje kuiga uhodari wa Henoko wanapowaonya watu kuhusu vita vya Har–Magedoni vinavyokaribia? (2 Tim. 4:2; Ebr. 13:6)
3. Soma Waebrania 11:5.
Ni sifa gani ya Henoko ‘iliyompendeza Mungu vema,’ na Mungu alifanya nini? (Mwa. 5:22)
Hadithi ya 8
Watu Wakubwa Mno Duniani
Matokeo yalikuwa nini malaika fulani wa Mungu walipomsikiliza Shetani?
Kwa nini malaika fulani waliacha kazi yao mbinguni ili waje duniani?
Kwa nini malaika walifanya makosa kuja duniani na kujifanyia miili ya wanadamu?
Watoto wa malaika hao walikuwa tofauti na watoto wengine kwa njia gani?
Kama unavyoona katika picha, watoto wa malaika walifanya nini baada ya kuwa wakubwa sana?
Ni mtu yupi mwema aliyeishi duniani baada ya kifo cha Henoko, na kwa nini Mungu alimpenda?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 6:1-8.
Mwanzo 6:6 inaonyesha nini kuhusu jinsi Yehova anavyouona mwenendo wetu? (Zab. 78:40, 41; Met. 27:11)
Soma Yuda 6.
Malaika ambao “hawakubaki mahali pao pa kwanza” katika siku za Nuhu wanatukumbusha nini leo? (1 Kor. 3:5-9; 2 Pet. 2:4, 9, 10)
Hadithi ya 9
Nuhu Anajenga Safina
Familia ya Nuhu ilikuwa na watu wangapi, na wanawe watatu waliitwa nani?
Mungu alimwagiza Nuhu afanye jambo gani lisilo la kawaida, na kwa nini?
Majirani wa Nuhu walifanya nini alipowaambia kuhusu safina?
Mungu alimwambia Nuhu afanye nini na wanyama?
Baada ya Mungu kufunga mlango wa safina, ilimbidi Nuhu na familia yake kufanya nini?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 6:9-22.
Kwa nini Nuhu alikuwa mwabudu wa kipekee sana wa Mungu wa kweli? (Mwa. 6:9, 22)
Yehova anaonaje jeuri, na jambo hilo linatusaidiaje kuchagua burundani zinazofaa? (Mwa. 6:11, 12; Zab. 11:5)
Tunawezaje kumwiga Nuhu tunapopata mwelekezo kutoka tengenezo la Yehova? (Mwa. 6:22; 1 Yoh. 5:3)
Soma Mwanzo 7:1-9.
Tunatiwaje moyo kwa kujua kwamba Mungu alimwona Nuhu kuwa mwadilifu, ingawa alikuwa mtu asiye mkamilifu? (Mwa. 7:1; Met. 10:16; Isa. 26:7)
Hadithi ya 10
Gharika Kuu
Kwa nini hakuna mtu yeyote aliyeweza kuingia ndani ya safina baada ya mvua kuanza kunyesha?
Yehova alifanya mvua inyeshe kwa siku na usiku ngapi, na maji yalifika mpaka wapi?
Ilikuwaje na safina maji yalipoanza kujaa duniani?
Je, wale watu wakubwa mno waliokoka Gharika, na vipi baba zao?
Safina ilikuwa wapi baada ya miezi mitano?
Kwa nini Nuhu alimwachilia kunguru kutoka katika safina?
Nuhu alijuaje kwamba maji yalikuwa yamepungua duniani?
Mungu alimwambia Nuhu nini baada ya yeye na familia yake kukaa katika safina kwa zaidi ya mwaka mmoja?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 7:10-24.
Viumbe wa dunia waliangamizwa kwa kadiri gani? (Mwa. 7:23)
Ilichukua muda gani tangu maji yalipoanza kupunguka hadi dunia ilikuwa imekauka? (Mwa. 7:11; 8:1, 14)
Soma Mwanzo 8:1-17.
Andiko la Mwanzo 8:17 linaonyeshaje kwamba kusudi la awali la Mungu kwa dunia halikubadilika? (Mwa. 1:22)
Soma 1 Petro 3:19, 20.
Malaika walioasi walipata adhabu gani waliporudi mbinguni? (Yuda 6)
Masimulizi kumhusu Nuhu na familia yake yanaimarishaje imani yetu katika uwezo wa Yehova wa kuwaokoa watu wake? (2 Pet. 2:9)
Hadithi ya 11
Upinde wa Kwanza wa Mvua
Kama picha inavyoonyesha Nuhu alifanya nini mara alipotoka katika safina?
Mungu alimpa Nuhu na familia yake amri gani baada ya Gharika?
Mungu alitoa ahadi gani?
Tunapouona upinde wa mvua, tunapaswa kukumbuka nini?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 8:18-22.
Tunawezaje kumtolea Yehova “harufu ya kutuliza” leo? (Mwa. 8:21; Ebr. 13:15, 16)
Yehova alisema nini juu ya moyo wa wanadamu, kwa hiyo tunapaswa kujihadhari kuhusu nini? (Mwa. 8:21; Mt. 15:18, 19)
Soma Mwanzo 9:9-17.
Yehova alifanya agano gani pamoja na viumbe wote duniani? (Mwa. 9:10, 11)
Agano linalohusu upinde wa mvua litaendelea kuwapo mpaka lini? (Mwa. 9:16)
Hadithi ya 12
Watu Wanajenga Mnara Mkubwa
Nimrodi alikuwa nani, na Mungu alimwonaje?
Kwa nini watu walikuwa wakitengeneza matofali, kama unavyoona katika picha?
Kwa nini Yehova hakupendezwa na ujenzi huo?
Yehova alisimamishaje ujenzi huo wa mnara?
Mji huo uliitwaje, na jina hilo linamaanisha nini?
Watu walifanya nini baada ya Yehova kuvuruga lugha zao?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 10:1, 8-10.
Nimrod alikuwa na sifa zipi, na jambo hilo linatupa onyo gani? (Mwa. 3:31)
Soma Mwanzo 11:1-9.
Kusudi la kujenga mnara lilikuwa nini, na kwa nini ujenzi huo haukufaulu? (Mwa. 11:4; Met. 16:18; Yoh. 5:44)
Hadithi ya 13
Ibrahimu—Rafiki ya Mungu
Wakazi wa mji wa Uru walikuwa watu wa aina gani?
Mtu unayemwona katika picha ni nani, alizaliwa lini, na alikaa wapi?
Yehova alimwambia Ibrahimu afanye nini?
Kwa nini Ibrahimu aliitwa rafiki ya Mungu?
Akina nani waliambatana na Ibrahimu alipohama Uru?
Yehova alimwambia Ibrahimu nini alipofika Kanaani?
Yehova alimwahidi Ibrahimu nini alipokuwa na umri wa miaka 99?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 11:27-32.
Ibrahimu na Lutu walikuwa na uhusiano upi wa ukoo? (Mwa. 11:27)
Ijapokuwa Biblia inasema kwamba Tera ndiye aliyechukua hatua ya kwenda Kanaani pamoja na jamaa yake, tunajuaje kwamba kwa kweli ni Ibrahimu aliyechukua hatua ya kwanza ya kuhama, na kwa nini alichukua hatua hiyo? (Mwa. 11:31; Mdo. 7:2-4)
Soma Mwanzo 12:1-7.
Yehova aliongeza ahadi gani katika agano alilofanya pamoja na Ibrahimu baada ya Ibrahimu kufika Kanaani? (Mwa. 12:7)
Soma Mwanzo 17:1-8, 15-17.
Abramu alipewa jina gani alipokuwa na umri wa miaka 99, na kwa nini? (Mwa. 17:5)
Yehova alimwahidi Sara baraka zipi za wakati ujao? (Mwa. 17:15, 16)
Soma Mwanzo 18:9-19.
Ni madaraka gani ya akina baba yanayotajwa katika Mwanzo 18:19? (Kum. 6:6, 7; Efe. 6:4)
Sara alifanya jambo gani linaloonyesha kwamba hatuwezi kumfichia Yehova jambo lolote? (Mwa. 18:12, 15; Zab. 44:21)
Hadithi ya 14
Mungu Anajaribu Imani ya Ibrahimu
Mungu alimwahidi Ibrahimu nini, na alitimizaje ahadi hiyo?
Mungu alijaribu imani ya Ibrahimu jinsi gani, kama picha inavyoonyesha?
Ibrahimu alifanya nini, ijapokuwa hakuelewa kwa nini Mungu alimwamuru kufanya jambo hilo?
Ni nini kilichotukia Ibrahimu alipochomoa kisu ili amwue mwanawe?
Imani ya Ibrahimu ilikuwa yenye nguvu kadiri gani?
Mungu alimwandalia Ibrahimu nini ili atoe dhabihu, na vipi?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 21:1-7.
Kwa nini Ibrahimu alimtahiri mwanawe katika siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake? (Mwa. 17:10-12; 21:4)
Soma Mwanzo 22:1-18.
Isaka alionyeshaje kwamba alimtii babake Ibrahimu, na jambo hilo lilionyesha kimbele tukio gani lililo muhimu zaidi? (Mwa. 22:7-9; 1 Kor. 5:7; Flp. 2:8, 9)
Hadithi ya 15
Mke wa Lutu Alitazama Nyuma
Kwa nini Ibrahimu na Lutu walitengana?
Kwa nini Lutu alichagua kuishi Sodoma?
Watu wa Sodoma walikuwa wenye sifa zipi?
Malaika wawili walimwonya Lutu juu ya jambo gani?
Kwa nini mke wa Lutu akawa nguzo ya chumvi?
Tunawea kujifunza somo gani kutokana na kisa cha mke wa Lutu?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 13:5-13.
Ibrahimu anatufundisha somo gani kuhusu jinsi ya kusuluhisha migogoro kati ya watu? (Mwa. 13:8, 9; Rom. 12:10; Flp. 2:3, 4)
Soma Mwanzo 18:20-33.
Kwa kujua jinsi Yehova alivyomtendea Ibrahimu, tunahakikishwaje kwamba Yehova na Yesu watahukumu kwa haki? (Mwa. 18:25, 26; Mt. 25:31-33)
Soma Mwanzo 19:1-29.
Masimulizi hayo ya Biblia yanaonyesha nini kuhusu maoni ya Yehova juu ya wanaume wanaolala na wanaume? (Mwa. 19:5, 13; Law. 20:13)
Tunaona tofauti gani kati ya jinsi Lutu na Ibrahimu walivyoitikia mwelekezo wa Yehova, na maitikio yao yanatufundisha nini? (Mwa. 19:15, 16, 19, 20; 22:3)
Soma Luka 17:28-32.
Mke wa Lutu alivionaje vitu vya kimwili, na jambo hilo ni onyo kwetu kwa njia gani? (Luka 12:15; 17:31, 32; Mt. 6:19-21, 25)
Soma 2 Petro 2:6-8.
Kwa kumwiga Lutu, tunapaswa kuwaonaje watu wasiomcha Mungu? (Eze. 9:4; 1 Yoh. 2:15-17)
Hadithi ya 16
Isaka Anapata Mke Mzuri
Mwanamume na mwanamke katika picha ni nani?
Ibrahimu alifanya nini ili kumtafutia mwanawe mke, na kwa nini?
Sala ya mtumishi wa Ibrahimu ilijibiwa jinsi gani?
Rebeka alijibuje alipoulizwa iwapo alitaka kuolewa na Isaka?
Ni nini kilichomfanya Isaka kuwa mwenye furaha tena?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 24:1-67.
Rebeka alionyesha sifa zipi nzuri alipokutana na mtumishi wa Ibrahimu kwenye kisima? (Mwa. 24:17-20; Met. 31:17, 31)
Mipango ambayo Ibrahimu alifanya kwa niaba ya Isaka ni mfano mzuri kwa Wakristo leo kwa njia gani? (Mwa. 24:37, 38; 1 Kor. 7:39; 2 Kor. 6:14)
Kama Isaka, kwa nini tunapaswa kutenga wakati ili kutafakari? (Mwa. 24:63; Zab. 77:12; Flp. 4:8)
Hadithi ya 17
Mapacha Waliokuwa Tofauti
Esau na Yakobo walikuwa nani, na walitofautiana kwa njia gani?
Esau na Yakobo walikuwa na umri gani wakati babu yao Ibrahimu alipokufa?
Esau alifanya nini kilichowahuzunisha sana wazazi wake?
Kwa nini Esau alimkasirikia sana ndugu yake Yakobo?
Isaka alimpa mwanawe Yakobo maagizo gani?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 25:5-11, 20-34.
Yehova alitabiri nini kuwahusu wana wawili wa Rebeka? (Mwa. 25:23)
Maoni ya Yakobo na Esau kuhusu haki ya mzaliwa wa kwanza yalitofautianaje? (Mwa. 25:31-34)
Soma Mwanzo 26:34, 35; 27:1-46; na 28:1-5.
Esau alionyeshaje wazi kwamba hakuthamini mambo ya kiroho? (Mwa. 26:34, 35; 27:46)
Isaka alimwambia Yakobo afanye nini ili apate baraka ya Yehova? (Mwa. 28:1-4)
Soma Waebrania 12:16, 17.
Kisa cha Esau kinaonyesha nini kuhusu kile ambacho huwapata wale wanaopuuza mambo matakatifu?
Hadithi ya 18
Yakobo Anakwenda Harani
Mwanamke ambaye unamwona katika picha ni nani, na Yakobo alimsaidiaje?
Yakobo alikuwa tayari kufanya nini ili kumwoa Raheli?
Wakati wa Yakobo kumwoa Raheli ulipowadia, Labani alifanya nini?
Yakobo alikubali kufanya nini ili Raheli awe mkewe?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 29:1-30.
Hata Labani alipomdanganya, Yakobo alitendaje kwa uaminifu, na tunajifunza nini kutokana na jambo hilo? (Mwa. 25:27; 29:26-28; Mt. 5:37)
Kisa cha Yakobo kinaonyeshaje tofauti kati ya upendo wa kweli na kupumbazwa tu na mtu? (Mwa. 29:18, 20, 30; Wim. 8:6)
Wanawake wanne wa familia ya Yakobo waliomzalia wana, walikuwa nani? (Mwa. 29:23, 24, 28, 29)
Hadithi ya 19
Yakobo Ana Jamaa Kubwa
Wana sita ambao mkewe wa kwanza Lea alimzalia Yakobo, waliitwa nani?
Wana wawili ambao Zilpa, mjakazi wa Lea, alimzalia Yakobo, walikuwa nani?
Wana wawili ambao Bilha, mjakazi wa Raheli, alimzalia Yakobo, waliitwa nani?
Wana wawili wa Raheli waliitwa nani, lakini jambo gani lilitukia alipojifungua mwana wa pili?
Yakobo alikuwa na wana wangapi kulingana na picha, na taifa gani lilitokana nao?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 29:32-35; 30:1-26 na 35:16-19.
Kama inavyoonyeshwa na wana 12 wa Yakobo, wavulana Waebrania walipewa majina kupatana na nini?
Soma Mwanzo 35:16-19 na 37:35.
Ijapokuwa Dina pekee anatajwa katika Biblia, tunajuaje kwamba Yakobo alikuwa na binti wengine pia? (Mwa. 37:34, 35)
Hadithi ya 20
Dina Anaingia Katika Taabu
Kwa nini Ibrahimu na Isaka hawakutaka watoto wao waoe au waolewe na Wakanaani?
Je, Yakobo alifurahia kwamba binti yake alifanya urafiki na wasichana Wakanaani?
Yule mtu anayemtazama Dina katika picha ni nani, na alifanya tendo gani baya sana?
Ndugu za Dina, Simeoni na Lawi, walifanya nini waliposikia jambo hilo?
Yakobo alikubali walichofanya Simeoni na Lawi?
Matatizo yote ya familia yao yalianzaje?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 34:1-31.
Je, Dina alishirikiana na wasichana Wakanaani tu mara moja moja? Eleza. (Mwa. 34:1)
) Kwa nini Dina anaweza kulaumiwa kwa kadiri fulani kwa kunajisiwa kwake? (Gal. 6:7)
Vijana leo wanawezaje kuonyesha kwamba wanachukua kwa uzito onyo la kisa cha Dina? (Met. 13:20; 1 Kor. 15:33; 1 Yoh. 5:19)
Hadithi ya 21
Yusufu Anachukiwa na Ndugu Zake
Kwa nini ndugu za Yusufu walimwonea wivu, na walifanya nini?
. Ndugu za Yusufu wanataka kumtenda nini, lakini Rubeni anasema nini?
Wanafanya nini wanabiashara Waishmaeli wanapopita?
Ndugu za Yusufu wanafanya nini ili kumdanganya baba yao kwamba Yusufu ameuawa?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 37:1-35.
Wakristo wanawezaje kumwiga Yusufu kwa kuwaeleza wazee kuhusu makosa ambayo wamewaona wengine wakifanya? (Mwa. 37:2; Law. 5:1; 1 Kor. 1:11)
Kwa nini ndugu za Yusufu walimtenda kwa hila? (Mwa. 37:11, 18; Met. 27:4; Yak. 3:14-16)
Yakobo alifanya nini, ambayo ni jambo la kawaida mtu anapokuwa na huzuni? (Mwa. 37:35)
Hadithi ya 22
Yusufu Anawekwa Katika Gereza
Yusufu ana umri gani anapopelekwa Misri, na ni jambo gani linalotukia anapofika huko?
Kwa nini Yusufu anafungwa gerezani?
Yusufu anapewa daraka gani gerezani?
Anapokuwa gerezani Yusufu anamsaidiaje mnyweshaji na mwokaji wa Farao?
Ni jambo gani linalotukia baada ya mnyeshwaji kuachiliwa kutoka gerezani?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 39:1-23.
Kwa nini Yusufu alimtoroka mke wa Potifa ingawa katika siku zake hakukuwa na sheria iliyoandikwa kutoka kwa Mungu iliyokataza uzinzi? (Mwa. 2:24; 20:3; 39:9)
Soma Mwanzo 40:1-23.
Eleza kifupi ndoto ya mnyweshaji na ufafanuzi ambao Mungu alimpa Yusufu. (Mwa. 40:9-13)
Mwokaji alikuwa na ndoto gani, na ilimaanisha nini? (Mwa. 40:16-19)
Jamii ya mtumwa mwaminifu na mwenye busara leo imeiga mtazamo wa Yusufu jinsi gani? (Mwa. 40:8; Zab. 36:9; Yoh. 17:17; Mdo. 17:2, 3)
Andiko la Mwanzo 40:20 linatusaidiaje kujua jinsi Wakristo wanavyopaswa kuziona sherehe za siku ya kuzaliwa? (Mhu. 7:1; Marko 6:21-28)
Hadithi ya 23
Ndoto za Farao
Ni jambo gani linalompata Farao usiku mmoja?
Kwa nini yule mnyweshaji anamkumbuka Yusufu hatimaye?
Kama picha inavyoonyesha, Farao anaota ndoto mbili zipi?
Yusufu anasema ndoto hizo zinamaanisha nini?
Yusufu anapataje kuwa mtu wa pili kwa cheo, yule anayemfuata Farao, nchini Misri?
Kwa nini ndugu za Yusufu wanakuja Misri, na kwa nini hawamtambui?
Yusufu anakumbuka ndoto gani, na jambo hilo linamsaidia kuelewa nini?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 41:1-57.
Yusufu alimwelekezaje Yehova fikira, na Wakristo wanaweza kuiga mfano wake kwa njia gani leo? (Mwa. 41:16, 25, 28; Mt. 5:16; 1 Pet. 2:12)
Miaka ya wingi iliyofuata miaka ya njaa nchini Misri inaonyeshaje kwa usahihi jinsi hali ya kiroho ya watu wa Yehova ni tofauti na hali ya dini zinazojidai kuwa za Kikristo? (Mwa. 41:29, 30; Amo. 8:11, 12)
Soma Mwanzo 42:1-8 na 50:20.
Je, ni makosa kwa waabudu wa Yehova kumwinamia binadamu ili kuonyesha heshima kwa cheo chake, ikiwa jambo hilo ni la kawaida katika nchi yake? (Mwa. 42:6)
Hadithi ya 24
Yusufu Anawajaribu Ndugu Zake
. Kwa nini Yusufu anawashtaki ndugu zake kwa kuwa wapelelezi?
Kwa nini Yakobo anamwacha mwanawe mdogo Benyamini aende Misri?
Kikombe cha fedha cha Yusufu kinaingiaje katika mfuko wa Benyamini?
Yuda anajitolea kufanya nini ili Benyamini aachiliwe?
Ndugu za Yusufu wamebadilika kwa njia gani?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 42:9-38.
Maneno ya Yusufu ambayo yanapatikana katika Mwanzo 42:18, yanawakumbusha wale walio na madaraka katika tengenezo la Yehova nini? (Neh. 5:15; 2 Kor. 7:1, 2)
Soma Mwanzo 43:1-34.
Ijapokuwa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza, ni nini kinachoonyesha kwamba Yuda ndiye msemaji kwa niaba ya ndugu zake? (Mwa. 43:3, 8, 9; 44:14, 18; 1 Nya. 5:2)
Yaelekea Yusufu aliwajaribu ndugu zake kwa njia gani, na kwa nini? (Mwa. 43:33, 34)
Soma Mwanzo 44:1-34.
Yusufu alijifanya kuwa mtu wa aina gani ili ndugu zake wasimtambue? (Mwa. 44:5, 15; Law. 19:26)
Ndugu za Yusufu walionyeshaje kwamba hawakuwa tena wenye wivu kama zamani? (Mwa. 44:13, 33, 34)
Hadithi ya 25
Jamaa Inahama Kwenda Misri
Inakuwaje Yusufu anapowaambia ndugu zake kwamba yeye ndiye Yusufu?
Yusufu anawaeleza ndugu zake nini kwa fadhili?
Farao anasema nini anapopata habari kuwahusu ndugu za Yusufu?
Watu wa jamaa ya Yakobo walikuwa wangapi walipohamia Misri?
Jamaa ya Yakobo ilikuja kuitwa nini, na kwa nini?
Maswali ya ziada:
Soma Mwanzo 45:1-28.
Masimulizi ya Biblia kumhusu Yusufu yanaonyeshaje kwamba Yehova anaweza kugeuza mambo yanayokusudiwa kuwadhuru watumishi wake yawe na matokeo mazuri? (Mwa. 45:5-8; Isa. 8:10; Flp. 1:12-14)
. Soma Mwanzo 46:1-27.
Yehova alimhakikishia Yakobo nini alipokuwa njiani kwenda Misri? (Mwa. 46:1-4)
Hadithi ya 26
Ayubu Ni Mwaminifu kwa Mungu
Ayubu ni nani?
Shetani alijaribu kufanya nini, lakini je, alifaulu?
Yehova alimpa Shetani ruhusa ya kufanya nini, na kwa nini?
Kwa nini mke wa Ayubu alimwambia ‘amlaani Mungu afe’? (Ona picha.)
Kama unavyoweza kuona katika picha ya pili, Yehova alimbarikije Ayubu, na kwa nini?
Ikiwa sisi, kama Ayubu, ni waaminifu kwa Yehova, tutapokea baraka zipi?
Maswali ya ziada:
Soma Ayubu 1:1-22.
Wakristo leo wanawezaje kumwiga Ayubu? (Ayu. 1:1; Flp. 2:15; 2 Pet. 3:14)
Soma Ayubu 2:1-13.
Ayubu alifanya nini alipoteswa na Shetani, na mkewe alifanya nini? (Ayu. 2:9, 10; Met. 19:3; Mika 7:7; Mal. 3:14)
Soma Ayubu 42:10-17.
Thawabu ambayo Ayubu alipata kwa sababu ya uaminifu wake inalinganaje na kile ambacho Yesu alipata kwa sababu ya uaminifu wake alipoishi duniani? (Ayu. 42:12; Flp. 2:9-11)
Baraka ambazo Ayubu alipokea kwa sababu ya ushikamanifu wake kwa Mungu zinatutia moyo kwa njia gani? (Ayu. 42:10, 12; Ebr. 6:10; Yak. 1:2-4, 12; 5:11)
Hadithi ya 27
Mfalme Mbaya Anatawala Misri
Mtu mwenye kiboko katika picha ni nani, na anampiga nani?
Baada ya Yusufu kufa, Waisraeli walipatwa na magumu gani?
Kwa nini Wamisri waliwaogopa Waisraeli?
Farao aliwapa wanawake waliowasaidia wanawake Waisraeli kujifungua amri gani?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 1:6-22.
Yehova alianza kutimiza ahadi aliyompa Ibrahimu kwa njia gani? (Kut. 1:7; Mwa. 12:2; Mdo. 7:17)
Wanawake Waebrania waliowasaidia wanawake wenzao kujifungua walionyeshaje kwamba waliheshimu utakatifu wa uhai? (Kut. 1:17; Mwa. 9:6)
Wanawake waliowasaidia wanawake Waisraeli kujifungua walipata thawabu gani kwa sababu ya uaminifu wao kwa Yehova? (Kut. 1:20, 21; Met. 19:17)
Shetani alijaribuje kulizuia kusudi la Yehova kuhusiana na Mbegu ya Ibrahimu iliyoahidiwa? (Kut. 1:22; Mt. 2:16)
Hadithi ya 28
Jinsi Mtoto Musa Alivyookolewa
Mtoto katika picha ni nani, na anashikilia kidole cha nani?
Mama ya Musa alifanya nini ili kumwokoa Musa asiuawe?
Ni nani yule msichana mdogo katika picha, naye alifanya nini?
Binti ya Farao alipompata mtoto huyo mchanga, Miriamu alipendekeza nini?
Binti ya Mfalme alimwambia mama ya Musa nini?
Swali la ziada:
Soma Kutoka 2:1-10.
Musa alipokuwa mchanga, mamake alikuwa na nafasi gani ya kumzoeza na kumfundisha, na wazazi wanawezaje kuiga mfano huo leo? (Kut. 2:9, 10; Kum. 6:6-9; Met. 22:6; Efe. 6:4; 2 Tim. 3:15)
Hadithi ya 29
Sababu Musa Alikimbia
Musa alilelewa wapi, lakini alijua nini kuwahusu wazazi wake?
Musa alifanya nini alipokuwa na umri wa miaka 40?
Musa alimwambia nini Mwisraeli mmoja aliyekuwa akipigana, na mtu huyo alimjibuje?
Kwa nini Musa alikimbia Misri?
Musa alikimbilia wapi, na alikutana na nani kule?
Musa alifanya nini kwa muda wa miaka 40 baada ya kukimbia Misri?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 2:11-25.
Ijapokuwa alikuwa amefundishwa hekima ya Wamisri kwa miaka mingi, Musa alionyeshaje ushikamanifu wake kwa Yehova na kwa watu wake? (Kut. 2:11, 12; Ebr. 11:24)
Soma Matendo 7:22-29.
Tunajifunza nini kutokana na jinsi Musa alivyojaribu kuwakomboa Waisraeli kutoka utumwani huko Misri peke yake? (Mdo. 7:23-25; 1 Pet. 5:6, 10)
Hadithi ya 30
Mti Mdogo Unaowaka Moto
Mlima unaoonekana katika picha unaitwaje?
Eleza jambo lisilo la kawaida ambalo Musa aliliona alipokwenda mlimani na kondoo zake.
Sauti iliyotoka katika kichaka ilisema nini, na sauti hiyo ilikuwa ya nani?
Musa alijibuje Mungu alipomwambia kwamba angewaongoza watu wa Mungu watoke Misri?
Mungu alimwambia Musa awaambie watu nini ikiwa wangemwuliza alitumwa na nani?
Musa angewasadikishaje Waisraeli kwamba Mungu ndiye aliyemtuma?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 3:1-22.
Kisa cha Musa kinatuhakikishiaje kwamba hata kama tunahisi hatuna ustadi wa kutimiza kazi fulani ambayo tumepewa na Mungu, Yehova atatusaidia? (Kut. 3:11, 13; 2 Kor. 3:5, 6)
Soma Kutoka 4:1-20.
Mtazamo wa Musa ulibadilikaje katika ile miaka 40 aliyoishi Midiani, na wale wanaotaka kupata mapendeleo kutanikoni wanaweza kujifunza nini kutokana na jambo hilo? (Kut. 2:11, 12; 4:10, 13; Mika 6:8; 1 Tim. 3:1, 6, 10)
Kisa cha Musa kinatupa uhakika gani hata kama Yehova anatutia nidhamu kwa kutumia tengenezo lake? (Kut. 4:12-14; Zab. 103:14; Ebr. 12:4-11)
Hadithi ya 31
Musa na Haruni Wanamwona Farao
Miujiza ya Musa na Haruni ilikuwa na matokeo gani juu ya Waisraeli?
Musa na Haruni walimwambia Farao nini, na Farao alijibuje?
Kama picha inavyoonyesha, fimbo ya Haruni ikawa nini alipoitupa chini?
Yehova alimwadhibu Farao kwa njia gani, naye Farao alifanya nini?
Ni jambo gani lililotukia baada ya pigo la kumi?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 4:27-31 na 5:1-23.
Farao alimaanisha nini aliposema: “Simjui Yehova hata kidogo”? (Kut. 5:2; 1 Sam. 2:12; Rom. 1:21)
Soma Kutoka 6:1-13, 26-30.
Yehova hakufanya ajulikane kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kwa njia gani? (Kut. 3:13, 14; 6:3; Mwa. 12:8)
Tunahisije tunapojua kwamba Yehova bado alimtuma Musa, hata ingawa Musa alihisi hakustahili kufanya kazi aliyopewa? (Kut. 6:12, 30; Luka 21:13-15)
Soma Kutoka 7:1-13.
Musa na Haruni walipomweleza Farao hukumu za Yehova kwa ujasiri, waliwawekea watumishi wa Mungu leo kielelezo gani? (Kut. 7:2, 3, 6; Mdo. 4:29-31)
Yehova alionyeshaje kwamba yeye ni mkuu sana kuliko miungu ya Misri? (Kut. 7:12; 1 Nya. 29:12)
Hadithi ya 32
Mapigo Kumi
Itazame picha, na ueleze mapigo matatu ya kwanza ambayo Yehova alileta juu ya Misri.
Mapigo matatu ya kwanza yalitofautianaje na yale mapigo mengine?
Eleza pigo la nne, la tano, na la sita.
Eleza pigo la saba, la nane, na la tisa.
Yehova aliwaambia Waisraeli wafanye nini kabla ya pigo la kumi?
Pigo la kumi lilikuwa nini, na ni jambo gani lililotukia baada ya pigo hilo?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 7:19–8:23.
Ijapokuwa makuhani wenye kufanya uchawi waliweza kuiga mapigo mawili ya kwanza ya Yehova, iliwabidi kukubali nini baada ya pigo la tatu? (Kut. 8:18, 19; Mt. 12:24-28)
Pigo la nne lilionyeshaje uwezo wa Yehova wa kulinda watu wake, na kujua jambo hilo kunawapa watu wa Mungu uhakikisho gani wanapokabili “dhiki kuu” iliyotabiriwa? (Kut. 8:22, 23; Ufu. 7:13, 14; 2 Nya. 16:9)
Soma Kutoka 8:24; 9:3, 6, 10, 11, 14, 16, 23-25; na 10:13-15, 21-23.
Ni vikundi viwili vipi vilivyofichuliwa na Mapigo Kumi, na kwa hiyo, sisi tunavionaje vikundi vinavyofanana na vikundi hivyo leo? (Kut. 8:10, 18, 19; 9:14)
Andiko la Kutoka 9:16 linatusaidiaje kuelewa ni kwa nini Yehova amemruhusu Shetani awepo hadi sasa? (Rom. 9:21, 22)
Soma Kutoka 12:21-32.
Pasaka iliwawezeshaje watu wengi kuokoka, nayo ilielekeza fikira kwenye nini? (Kut. 12:21-23; Yoh. 1:29; Rom. 5:18, 19, 21; 1 Kor. 5:7)
Hadithi ya 33
Kuvuka Bahari Nyekundu (ya Shamu)
Ni wanaume Waisraeli wangapi, pamoja na wanawake na watoto, walioondoka Misri, na ni nani waliondoka pamoja nao?
Farao alihisije baada ya kuwaacha Waisraeli waondoke, naye alifanya nini?
Yehova alifanya nini ili kuwazuia Wamisri wasiwashambulie watu wake?
Ni jambo gani lililotukia Musa alipoinua fimbo yake juu ya Bahari Nyekundu, na Waisraeli walifanya nini?
Wamisri walipatwa na nini walipowafuata Waisraeli ndani ya bahari?
Waisraeli walionyeshaje kwamba walifurahi na kumshukuru Yehova kwa wokovu wao?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 12:33-36.
Yehova alihakikishaje kwamba watu wake walilipwa kwa miaka yote ya utumwa chini ya Wamisri? (Kut. 3:21, 22; 12:35, 36)
Soma Kutoka 14:1-31.
Maneno ya Musa yanayopatikana katika Kutoka 14:13, 14 yanawatiaje moyo watumishi wa Yehova leo wanapokabili vita vya Har-magedoni vitakavyokuja? (2 Nya. 20:17; Zab. 91:8)
Soma Kutoka 15:1-8, 20, 21.
Kwa nini watumishi wa Yehova wanapaswa kumwimbia nyimbo za sifa? (Kut. 15:1, 2; Zab. 105:2, 3; Ufu. 15:3, 4)
Miriamu na wanawake waliovuka Bahari Nyekundu waliwawekea wanawake Wakristo leo mfano gani? (Kut. 15:20, 21; Zab. 68:11)
Hadithi ya 34
Aina Mpya ya Chakula
Watu wanaokota kitu gani katika picha hii, na kinaitwaje?
Musa anawapa watu maagizo gani kuhusu kuokota mana?
Yehova anawaambia watu wafanye nini katika siku ya sita, na kwa nini?
Yehova anafanya mwujiza gani wakati mana inapowekwa kwa ajili ya siku ya saba?
Yehova anawalisha watu mana kwa muda gani?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 16:1-36 na Hesabu 11:7-9.
Andiko la Kutoka 16:8 linaonyesha nini kuhusu umuhimu wa kuwaheshimu wale walio na madaraka katika kutaniko la Kikristo? (Ebr. 13:17)
Walipokuwa nyikani, Waisraeli walikumbushwaje kila siku kwamba hawakuweza kuishi bila kumtegemea Yehova? (Kut. 16:14-16, 35; Kum. 8:2, 3)
Yesu alisema mana ni mfano wa nini, nasi tunafaidikaje na “mkate [huo] kutoka mbinguni”? (Yoh. 6:31-35, 40)
Soma Yoshua 5:10-12.
Waisraeli walikula mana kwa miaka mingapi, jambo hilo lilikuwa jaribio kwao kwa njia gani, nasi tunajifunza nini kutokana na masimulizi hayo? (Kut. 16:35; Hes. 11:4-6; 1 Kor. 10:10, 11)
Hadithi ya 35
Yehova Anatoa Sheria Zake
Waisraeli wanapiga kambi wapi miezi miwili hivi baada ya kutoka Misri?
Yehova anasema anawataka watu wafanye nini, nao wanajibuje?
Kwa nini Yehova anampa Musa mabamba mawili ya mawe?
Mbali na Amri Kumi, Yehova anawapa Waisraeli sheria gani nyingine?
Yesu Kristo alisema ni sheria gani mbili zilizo kuu?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 19:1-25; 20:1-21; 24:12-18; na 31:18.
Andiko la Kutoka 19:8 linatusaidiaje kuelewa kinachohusika mtu anapojiweka wakfu ili awe Mkristo? (Mt. 16:24; 1 Pet. 4:1-3)
Soma Kumbukumbu la Torati 6:4-6; Mambo ya Walawi 19:18; na Mathayo 22:36-40.
Wakristo wanaonyeshaje upendo kwa Mungu na jirani? (Marko 6:34; Mdo. 4:20; Rom. 15:2)
Hadithi ya 36
Ndama ya Dhahabu
Watu wanafanya nini katika picha hii, na kwa nini?
Kwa nini Yehova amekasirika, na Musa anafanya nini anapoona kile ambacho watu wanafanya?
Musa anawaambia baadhi ya wanaume hao wafanye nini?
Masimulizi haya yanatufundisha nini?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 32:1-35.
Masimulizi hayo yanaonyeshaje maoni ya Yehova kuhusu kuchanganya dini ya uwongo na ibada ya kweli? (Kut. 32:4-6, 10; 1 Kor. 10:7, 11)
Wakristo wanapaswa kujihadhari na nini wanapofanya uamuzi kuhusu burudani kama vile nyimbo na dansi? (Kut. 32:18, 19; Efe. 5:15, 16; 1 Yoh. 2:15-17)
Kabila la Lawi lilionyeshaje mfano mzuri kwa kuunga mkono uadilifu? (Kut. 32:25-28; Zab. 18:25)
Hadithi ya 37
Hema la Ibada
Ni jengo gani unaloona katika picha, na ni la nini?
Kwa nini Yehova alimwambia Musa hema lijengwe kwa njia ambayo lingeweza kubomolewa kwa urahisi?
Ni sanduku gani lililo katika chumba kidogo kwenye sehemu ya mwisho ya hema, na kuna nini ndani ya sanduku hilo?
Yehova anamchagua nani kuwa kuhani mkuu, na kuhani mkuu anafanya kazi gani?
Taja vile vitu vitatu vilivyo katika chumba kikubwa hemani.
Ni vitu gani viwili vilivyo kwenye ua wa hema, navyo hutumiwa kwa njia gani?
Maswali ya ziada:
Soma Kutoka 25:8-40; 26:1-37; 27:1-8; na 28:1.
Makerubi kwenye “sanduku la ushuhuda” wanawakilisha nini? (Kut. 25:20, 22; Hes. 7:89; 2 Fal. 19:15)
Soma Kutoka 30:1-10, 17-21; 34:1, 2; na Waebrania 9:1-5.
Kwa nini Yehova alikazia umuhimu wa kudumisha usafi wa kimwili kwa makuhani waliotumikia hemani, na jambo hilo linatufundisha nini? (Kut. 30:18-21; 40:30, 31; Ebr. 10:22)
Mtume Paulo anaonyeshaje kwamba hema la kukutania na agano la Sheria hazikuhitajika tena wakati alipowaandikia Wakristo Waebrania barua? (Ebr. 9:1, 9; 10:1)
Hadithi ya 38
Wapelelezi 12
Unakionaje kichala cha zabibu katika picha, nacho kilitoka wapi?
Kwa nini Musa anawatuma wapelelezi 12 Kanaani?
Wapelelezi kumi wanamletea Musa habari gani?
Wapelelezi wawili wanaonyeshaje kwamba wanamtegemea Yehova, nao wanaitwa nani?
Kwa nini Yehova amekasirika, naye anamwambia Musa nini?
Maswali ya ziada:
Soma Hesabu 13:1-33.
Ni akina nani waliochaguliwa kupeleleza nchi, nao walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya nini? (Hes. 13:2, 3, 18-20)
Kwa nini maoni ya Yoshua na Kalebu yalitofautiana na ya wale wapelelezi wengine, na jambo hilo linatufundisha nini? (Hes. 13:28-30; Mt. 17:20; 2 Kor. 5:7)
Soma Hesabu 14:1-38.
Tunapaswa kutii onyo gani juu ya kuwanung’unikia wawakilishi wa Yehova duniani? (Hes. 14:2, 3, 27; Mt. 25:40, 45; 1 Kor. 10:10)
Andiko la Hesabu 14:24 linaonyeshaje kwamba Yehova anapendezwa na kila mmoja wa watumishi wake? (1 Fal. 19:18; Met. 15:3)
Hadithi ya 39
Fimbo ya Haruni Inamea Maua
Ni nani wanaopinga mamlaka ya Musa na Haruni, nao wanamwambia Musa nini?
Musa anamwambia Kora na wafuasi wake 250 wafanye nini?
Musa anawaambia watu nini, na ni jambo gani linalotokea mara anapomaliza kusema?
Kora na wafuasi wake 250 wanapatwa na nini?
Eleazari, mwana wa Haruni, anafanya nini na makoleo ya moto ya watu waliokufa, na kwa nini?
Kwa nini Yehova anafanya fimbo ya Haruni imee maua? (Ona picha.)
Maswali ya ziada:
Soma Hesabu 16:1-49.
Kora na wafuasi wake walifanya nini, na kwa nini hilo lilikuwa tendo la kumwasi Yehova? (Hes. 16:9, 10, 18; Law. 10:1, 2; Met. 11:2)
Kora na wale “wakuu wa kusanyiko” 250 walisitawisha maoni gani yasiyofaa? (Hes. 16:1-3; Met. 15:33; Isa. 49:7)
Soma Hesabu 17:1-11 na 26:10.
Kumea maua kwa fimbo ya Haruni kulionyesha nini, na kwa nini Yehova aliagiza ihifadhiwe katika sanduku? (Hes. 17:5, 8, 10)
Ishara ya fimbo ya Haruni inatufundisha jambo gani muhimu? (Hes. 17:10; Mdo. 20:28; Flp. 2:14; Ebr. 13:17)
Hadithi ya 40
Musa Anaupiga Mwamba
Yehova anawatunzaje Waisraeli wakiwa nyikani?
Waisraeli wanalalamika juu ya nini wanapopiga kambi Kadeshi?
Yehova anawaandaliaje watu na mifugo maji?
Katika picha, mtu anayejielekezea kidole ni nani, na kwa nini anafanya hivyo?
Kwa nini Yehova amewakasirikia Musa na Haruni, na wanaadhibiwa kwa njia gani?
Ni jambo gani linalotendeka kwenye Mlima Hori, na ni nani anayewekwa kuwa kuhani mkuu wa Israeli?
Maswali ya ziada:
Soma Hesabu 20:1-13, 22-29 na Kumbukumbu la Torati 29:5.
Tunajifunza nini kutokana na jinsi Yehova alivyowatunza Waisraeli nyikani? (Kum. 29:5; Mt. 6:31; Ebr. 13:5; Yak. 1:17)
Yehova aliwaonaje Musa na Haruni waliposhindwa kumtukuza mbele ya Waisraeli? (Hes. 20:12; 1 Kor. 10:12; Ufu. 4:11)
Tunaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Musa alivyotenda alipotiwa nidhamu na Yehova? (Hes. 12:3; 20:12, 27, 28; Kum. 32:4; Ebr. 12:7-11)
Hadithi ya 41
Nyoka wa Shaba
Kama picha inavyoonyesha, ni kitu gani ambacho kimezungushwa juu ya mti, na kwa nini Yehova alimwambia Musa akiweke juu ya mti huo?
Watu wanakosaje kumshukuru Mungu kwa yote ambayo amewafanyia?
Watu wanamwomba Musa afanye nini baada ya Yehova kuwatuma nyoka wenye sumu wawaadhibu?
Kwa nini Yehova anamwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba?
Tunajifunza nini kutokana na masimulizi haya?
Maswali ya ziada:
Soma Hesabu 21:4-9.
Tunapata onyo gani kutokana na jinsi Waisraeli wanavyolalamikia maandalizi ya Yehova? (Hes. 21:5, 6; Rom. 2:4)
Katika karne zilizofuata, Waisraeli walitumiaje yule nyoka wa shaba, na Mfalme Hezekia alichukua hatua gani? (Hes. 21:9; 2 Fal. 18:1-4)
Soma Yohana 3:14, 15.
Kuwekwa kwa nyoka wa shaba juu ya mti ili watu wamtazame kunafananishaje vizuri kutundikwa kwa Yesu Kristo kwenye mti wa mateso? (Gal. 3:13; 1 Pet. 2:24)
Hadithi ya 42
Punda Anasema
Balaki ni nani, na kwa nini anamwita Balaamu aje?
Kwa nini punda wa Balaamu amelala njiani?
Balaamu anamsikia punda akisema nini?
Malaika anamwambia Balaamu nini?
Inakuwaje Balaamu anapojaribu kuwalaani Waisraeli?
Maswali ya ziada:
Soma Hesabu 21:21-35.
Kwa nini Waisraeli walimshinda Mfalme Sihoni wa Waamori na Mfalme Ogi wa Bashani? (Hes. 21:21, 23, 33, 34)
Soma Hesabu 22:1-40.
Balaamu alikuwa na nia gani alipojaribu kuwalaani Waisraeli, na tunajifunza nini kutokana na jambo hilo? (Hes. 22:16, 17; Met. 6:16, 18; 2 Pet. 2:15; Yuda 11)
Soma Hesabu 23:1-30.
Ijapokuwa Balaamu aliongea kana kwamba alikuwa mwabudu wa Yehova, matendo yake yalionyeshaje kwamba hakuwa mwabudu wa Yehova? (Hes. 23:3, 11-14; 1 Sam. 15:22)
Soma Hesabu 24:1-25.
Masimulizi haya yanaimarishaje imani yetu kwamba kusudi la Yehova litatimizwa hakika? (Hes. 24:10; Isa. 54:17)
Hadithi ya 43
Yoshua Anakuwa Kiongozi
Watu wawili wanaosimama pamoja na Musa katika picha ni nani?
Yehova anamwambia Yoshua nini?
Kwa nini Musa anapanda hadi kilele cha Mlima Nebo, na Yehova anamwambia nini?
Musa ana umri gani anapokufa?
Kwa nini watu wanahuzunika, lakini wana sababu gani ya kufurahi?
Maswali ya ziada:
Soma Hesabu 27:12-23.
Yehova alimpa Yoshua kazi gani muhimu, na Yehova anawatunzaje watu Wake leo? (Hes. 27:15-19; Mdo. 20:28; Ebr. 13:7)
Soma Kumbukumbu la Torati 3:23-29.
Kwa nini Yehova hakuwaruhusu Musa na Haruni kuingia katika nchi ya ahadi, na jambo hilo linatufunza nini? (Kum. 3:25-27; Hes. 20:12, 13)
Soma Kumbukumbu la Torati 31:1-8, 14-23.
Maneno ya mwisho ya Musa kwa Waisraeli yanaonyeshaje kwamba alikubali nidhamu ya Yehova kwa unyenyekevu? (Kum. 31:6-8, 23)
Soma Kumbukumbu la Torati 32:45-52.
Neno la Mungu linapaswa kuwa na matokeo gani maishani mwetu? (Kum. 32:47; Law. 18:5; Ebr. 4:12)
Soma Kumbukumbu la Torati 34:1-12.
Ijapokuwa Musa hakumwona Yehova kwa macho yake, andiko la Kumbukumbu la Torati 34:10 linaonyesha nini juu ya uhusiano wake pamoja na Yehova? (Kut. 33:11, 20; Hes. 12:8)
Hadithi ya 44
Rahabu Anaficha Wapelelezi
Rahabu anaishi wapi?
Watu wawili katika picha ni nani, na kwa nini wako Yeriko?
Mfalme wa Yeriko anamwamuru Rahabu afanye nini, naye anajibuje?
Rahabu anawasaidiaje watu hao wawili, na anawaomba nini?
Wapelelezi hao wawili wanamwahidi Rahabu nini?
Maswali ya ziada:
Soma Yoshua 2:1-24.
Ahadi ya Yehova iliyoandikwa katika Kutoka 23:28 ilitimizwaje Waisraeli walipozunguka Yeriko? (Yos. 2:9-11)
Soma Waebrania 11:31.
Kisa cha Rahabu kinakaziaje umuhimu wa kuwa na imani? (Rom. 1:17; Ebr. 10:39; Yak. 2:25)
Hadithi ya 45
Kuvuka Mto Yordani
Yehova anafanya mwujiza gani ili Waisraeli waweze kuvuka Mto Yordani?
Inawabidi Waisraeli kuonyesha imani kwa njia gani ili wavuke Mto Yordani?
Kwa nini Yehova anamwambia Yoshua achukue mawe makubwa 12 kutoka mtoni?
Ni jambo gani linalotukia mara makuhani wanapopanda kutoka ndani ya Mto Yordani?
Maswali ya ziada:
Soma Yoshua 3:1-17.
Kama inavyoonyeshwa na masimulizi haya, tunapaswa kufanya nini ili tupate msaada na baraka za Yehova? (Yos. 3:13, 15; Met. 3:5; Yak. 2:22, 26)
Mto Yordani ulikuwa katika hali gani Waisraeli walipouvuka na kuingia Nchi ya Ahadi, na jambo hilo lilitukuzaje jina la Yehova? (Yos. 3:15; 4:18; Zab. 66:5-7)
Soma Yoshua 4:1-18.
Yale mawe 12 yalichukuliwa kutoka katika Mto Yordani na kuwekwa Gilgali kwa kusudi gani? (Yos. 4:4-7)
Hadithi ya 46
Kuta za Yeriko
Yehova anawaambia watu wa vita na makuhani wafanye nini kwa siku sita?
Watu hao wanaambiwa wafanye nini siku ya saba?
Inakuwaje na kuta za Yeriko kama unavyoona katika picha?
Kwa nini kuna kamba nyekundu inayoning’inia katika dirisha moja?
Yoshua anawaambia watu wa vita wafanye nini na watu na mjini, lakini vipi fedha, dhahabu, shaba, na chuma?
Wale wapelelezi wawili wanaambiwa wafanye nini?
Maswali ya ziada:
Soma Yoshua 6:1-25.
Kuzunguka kwa Yeriko katika siku ya saba kunalinganaje na kazi ya kuhubiri ya Mashahidi wa Yehova katika siku hizi za mwisho? (Yos. 6:15, 16; Isa. 60:22; Mt. 24:14; 1 Kor. 9:16)
Unabii ulioandikwa katika Yoshua 6:26 ulitimizwaje miaka 500 baadaye, na jambo hilo linatufundisha nini juu ya neno la Yehova? (1 Fal. 16:34; Isa. 55:11)
Hadithi ya 47
Mwivi Katika Israeli
Katika picha, ni nani mtu huyo anayeficha mali zilizochukuliwa Yeriko, na anasaidiwa na nani?
. Kwa nini tendo hilo la Akani na familia yake ni baya sana?
Yehova anasema nini Yoshua anapomwuliza ni kwa nini Waisraeli walishindwa vitani huko Ai?
Baada ya Akani na familia yake kupelekwa mbele ya Yoshua, wanapatwa na nini?
Adhabu ambayo Akani alihukumiwa inatufundisha jambo gani muhimu?
Maswali ya ziada:
Soma Yoshua 7:1-26.
Sala za Yoshua zilionyesha nini kuhusu uhusiano wake pamoja na Muumba wake? (Yos. 7:7-9; Zab. 119:145; 1 Yoh. 5:14)
Kisa cha Akani kinaonyesha nini, na kinatuonya juu ya nini? (Yos. 7:11, 14, 15; Met. 15:3; 1 Tim. 5:24; Ebr. 4:13)
Soma Yoshua 8:1-29.
Kila mmoja wetu ana wajibu gani kuhusiana na kutaniko la Kikristo leo? (Yos. 7:13; Law. 5:1; Met. 28:13)
Hadithi ya 48
Wagibeoni Wenye Akili
Wagibeoni wanatofautianaje na Wakanaani wanaoishi katika miji jirani?
Kama picha inavyoonyesha, Wagibeoni wanafanya nini, na kwa nini?
Yoshua na viongozi wa Israeli wanawaahidi Wagibeoni nini, lakini wanagundua nini siku tatu baadaye?
Inakuwaje wakati wafalme wa miji jirani wanaposikia kwamba Wagibeoni wamefanya amani pamoja na Waisraeli?
Maswali ya ziada:
Soma Yoshua 9:1-27.
Yehova alionyesha sifa zipi alipowaruhusu Wagibeoni kuishi ijapokuwa alikuwa amewaagiza Waisraeli ‘wawaangamize wakaaji wote wa nchi’? (Yos. 9:22, 24; Mt. 9:13; Mdo. 10:34, 35; 2 Pet. 3:9)
Kwa kushika agano alilofanya pamoja na Wagibeoni, Yoshua aliwawekea Wakristo leo mfano gani mzuri? (Yos. 9:18, 19; Mt. 5:37; Efe. 4:25)
Soma Yoshua 10:1-5.
Umati mkubwa huwaiga Wagibeoni jinsi gani leo, nao hushambuliwa na nani? (Yos. 10:4; Zek. 8:23; Mt. 25:35-40; Ufu. 7:9)
Hadithi ya 49
Jua Linasimama Tu
Yoshua anasema nini katika picha hii, na kwa nini?
Yehova anamsaidiaje Yoshua na watu wake wa vita?
Yoshua anawashinda wafalme maadui wangapi, na jambo hilo linachukua muda gani?
Kwa nini Yoshua anagawanya nchi ya Kanaani?
Yoshua ana umri gani anapokufa, na watu wanafanya nini baadaye?
Maswali ya ziada:
Soma Yoshua 10:6-15.
Sisi tunahakikishiwa nini leo kwa kujua kwamba Yehova alifanya jua na mwezi kusimama tuli kwa ajili ya Waisraeli? (Yos. 10:8, 10, 12, 13; Zab. 18:3; Met. 18:10)
Soma Yoshua 12:7-24.
Ni nani aliyewashinda wale wafalme 31 nchini Kanaani, na kwa nini jambo hili ni muhimu kwetu leo? (Yos. 12:7; 24:11-13; Kum. 31:8; Luka 21:9, 25-28)
Soma Yoshua 14:1-5.
Makabila ya Israeli yaligawanyiwa nchi jinsi gani, na jambo hili linaonyesha nini kuhusu urithi tutakaopata katika Paradiso? (Yos. 14:2; Isa. 65:21; Eze. 47:21-23; 1 Kor. 14:33)
Soma Yoshua 2:8-13.
Ni nani leo wanaozuia uasi-imani kama Yoshua alivyofanya nchini Israeli? (Amu. 2:8, 10, 11; Mt. 24:45-47; 2 The. 2:3-6; Tito 1:7-9; Ufu. 1:1; 2:1, 2)
Hadithi ya 50
Wanawake Hodari Wawili
Waamuzi ni nani, na yule wa kwanza aliitwa nani?
Debora ana pendeleo gani la pekee, nalo linahusisha nini?
Waisraeli wanapotishwa na Mfalme Yabini na mkuu wa jeshi lake, Sisera, Debora anampa Mwamuzi Baraki ujumbe gani kutoka kwa Yehova, na anasema ni nani atakayesifiwa kwa ushindi huo?
Yaeli anaonyeshaje kwamba yeye ni mwanamke hodari?
Hali inakuwaje baada ya kifo cha Mfalme Yabini?
Maswali ya ziada:
Soma Waamuzi 2:14-22.
Waisraeli walijileteaje hasira ya Yehova, na tunajifunza nini kutokana na jambo hili? (Amu. 2:20; Met. 3:1, 2; Eze. 18:21-23)
Soma Waamuzi 4:1-24.
Wanawake Wakristo wanaweza kujifunza nini kuhusu imani na uhodari kutokana na mfano wa Debora na Yaeli? (Amu. 4:4, 8, 9, 14, 21, 22; Met. 31:30; 1 Kor. 16:13)
Soma Waamuzi 5:1-31.
Wimbo wa ushindi wa Baraki na Debora unaweza kutumiwaje kama sala kuhusu vita vya Har-magedoni vinavyokaribia? (Amu. 5:3, 31; 1 Nya. 16:8-10; Ufu. 7:9, 10; 16:16; 19:19-21)
Hadithi ya 51
Ruthu na Naomi
Kwa nini Naomi anaishi katika nchi ya Moabu?
Ruthu na Orpa ni nani?
Ruthu anafanya nini Naomi anapomwambia arudi kwao, Orpa naye anafanya nini?
Boazi ni nani, naye anamsaidiaje Ruthu na Naomi?
Mtoto wa Boazi na Ruthu anaitwa nani, na kwa nini tunapaswa kumkumbuka?
Maswali ya ziada:
Soma Ruthu 1:1-17.
Ruthu anasema maneno gani mazuri yanayoonyesha upendo mshikamanifu? (Rut. 1:16, 17)
Mtazamo wa Ruthu unalinganaje na maoni ya “kondoo wengine” kuwahusu watiwa-mafuta walio duniani leo? (Yoh. 10:16; Zek. 8:23)
Soma Ruthu 2:1-23.
Ruthu aliwekaje mfano mzuri kwa wanawake vijana leo? (Rut. 2:17, 18; Met. 23:22; 31:15)
Soma Ruthu 3:5-13.
Boazi alionaje utayari wa Ruthu kuolewa naye badala ya mwanamume kijana?
Mtazamo wa Ruthu unatufundisha nini kuhusu upendo mshikamanifu? (Rut. 3:10; 1 Kor. 13:4, 5)
Soma Ruthu 4:7-17.
Wanaume Wakristo leo wanawezaje kumwiga Boazi? (Rut. 4:9, 10; 1 Tim. 3:1, 12, 13; 5:8)
Hadithi ya 52
Gideoni na Wanaume Wake 300
Waisraeli wanakabili taabu gani, na kwa nini?
Kwa nini Yehova anamwambia Gideoni kwamba watu wa jeshi lake ni wengi mno?
Ni watu wangapi wanaobaki baada ya Gideoni kuwaambia wale wanaoogopa warudi nyumbani?
Itazame picha na ueleze jinsi Yehova anavyopunguza idadi ya watu katika jeshi la Gideoni hadi wanaume 300 tu.
Gideoni anawapangaje watu wake 300, na Waisraeli wanashindaje vita hivyo?
Maswali ya ziada:
Soma Waamuzi 6:36-40.
Gideoni anafanya nini ili ajue mapenzi ya Yehova?
Tunajuaje mapenzi ya Yehova leo? (Met. 2:3-6; Mt. 7:7-11; 2 Tim. 3:16, 17)
Soma Waamuzi 7:1-25.
Tunajifunza nini kutokana na wale watu 300 waliokuwa macho, tofauti na wale waliokuwa wazembe? (Amu. 7:3, 6; Rom. 13:11, 12; Efe. 5:15-17)
Kama wale 300 walivyojifunza kwa kumtazama Gideoni, tunajifunzaje kwa kumtazama Gideoni Mkuu, Yesu Kristo? (Amu. 7:17; Mt. 11:29, 30; 28:19, 20; 1 Pet. 2:21)
Andiko la Waamuzi 7:21 linatusaidiaje kuridhika na kazi yoyote tunayopewa katika tengenezo la Yehova? (1 Kor. 4:2; 12:14-18; Yak. 4:10)
Soma Waamuzi 8:1-3.
Tunajifunza nini kuhusu jinsi ya kushughulikia mgogoro kati yetu na ndugu au dada kutokana na jinsi Gideoni alivyoshughulikia mzozo uliozushwa na Waefraimu? (Met. 15:1; Mt. 5:23, 24; Luka 9:48)
Hadithi ya 53
Ahadi ya Yeftha
Yeftha ni nani, na aliishi katika kipindi kipi?
Yeftha anamwahidi Yehova nini?
Kwa nini Yeftha anahuzunika anaporudi nyumbani baada ya kuwashinda Waamoni?
Binti ya Yeftha anasema nini anaposikia kuhusu ahadi ya babake?
Kwa nini watu wanampenda binti Yeftha?
Maswali ya ziada:
Soma Waamuzi 10:6-18.
Tunapaswa kutii onyo gani linalopatikana katika masimulizi kuwahusu Waisraeli waliokosa kuwa waaminifu kwa Yehova? (Amu. 10:6, 15, 16; Rom. 15:4; Ufu. 2:10)
Soma Waamuzi 11:1-11, 29-40.
Tunajuaje kwamba Yeftha hakumteketeza kihalisi binti yake motoni alipomtoa kama “toleo la kuteketezwa”? (Amu. 11:31; Law. 16:24; Kum. 18:10, 12)
Yeftha alimtoa binti yake awe dhabihu kwa njia gani?
Tunajifunza nini kutokana na maoni ya Yeftha juu ya ahadi yake kwa Yehova? (Amu. 11:35, 39; Mhu. 5:4, 5; Mt. 16:24)
Kwa nini binti ya Yeftha ni mfano mzuri kwa vijana Wakristo wa kufuatilia utumishi wa wakati wote? (Amu. 11:36; Mt. 6:33; Flp. 3:8)
Hadithi ya 54
Mwanamume Mwenye Nguvu Kuliko Wote
Mtu mwenye nguvu kuliko wote ambao wamewahi kuishi anaitwa nani, na ni nani aliyempa nguvu?
Kama unavyoona katika picha, Samsoni alifanya nini alipokutana na simba mkubwa?
Samsoni anamwambia Delila siri gani katika picha, na jambo hilo linasababishaje kwamba anakamatwa na Wafilisti?
Samsoni alisababishaje vifo vya maadui Wafilisti 3,000 siku aliyokufa?
Maswali ya ziada:
Soma Waamuzi 13:1-14.
Manoa na mkewe wanawawekaje wazazi mfano gani mzuri kuhusu kuwalea watoto? (Amu. 13:8; Zab. 127:3; Efe. 6:4)
Soma Waamuzi 14:5-9 na 15:9-16.
Masimulizi kuhusu jinsi Samsoni anavyomwua simba, anavyokata kamba mpya zilizotumiwa kumfunga, na kutumia taya ya punda-dume kuwaua watu 1,000, yanaonyesha nini kuhusu utendaji wa roho takatifu ya Yehova?
Roho takatifu inatusaidiaje leo? (Amu. 14:6; 15:14; Zek. 4:6; Mdo. 4:31)
Soma Waamuzi 16:18-31.
Samsoni aliathiriwaje kwa kushirikiana na watu wabaya, na tunajifunza nini kutokana na jambo hili? (Amu. 16:18, 19; 1 Kor. 15:33)
Hadithi ya 55
Mvulana Mdogo Anamtumikia Mungu
Mvulana mdogo unayemwona katika picha anaitwaje, na wale wengine ni nani?
Hana anasali kuhusu nini anapotembelea hema la kukutania la Yehova siku moja, na Yehova anamjibuje?
Samweli ana umri gani anapopelekwa kutumikia kwenye hema la Yehova, na mamake anamshonea nini kila mwaka?
Wana wa Eli wanaitwa nani, nao ni watu wa aina gani?
Yehova anamwita Samweli jinsi gani, na anampa ujumbe gani?
Samweli anapokuwa mtu mzima anakuwa nini, na ni jambo gani linalotukia anapokuwa mzee?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 1:1-28.
Elkana anawawekea vichwa wa familia mfano gani mzuri anapoongoza familia yake katika ibada ya kweli? (1 Sam. 1:3, 21; Mt. 6:33; Flp. 1:10)
Tunajifunza nini kutokana na jinsi Hana alivyoshughulikia tatizo kubwa? (1 Sam. 1:10, 11; Zab. 55:22; Rom. 12:12)
Soma 1 Samweli 2:11-36.
Eli aliwaheshimu wanawe kuliko Yehova kwa njia gani, na jambo hili linawezaje kuwa onyo kwetu? (1 Sam. 2:22-24, 27, 29; Kum. 21:18-21; Mt. 10:36, 37)
Soma 1 Samweli 4:16-18.
Ni ujumbe gani juu ya misiba minne unaoletwa kutoka vitani, nao unamwathirije Eli?
Soma 1 Samweli 8:4-9.
Waisraeli walimkasirisha sana Yehova kwa njia gani, nasi tunawezaje kuunga mkono Ufalme wake kwa uaminifu leo? (1 Sam. 8:5, 7; Yoh. 17:16; Yak. 4:4)
Hadithi ya 56
Sauli—Mfalme wa Kwanza wa Israeli
Samweli anafanya nini katika picha, na kwa nini?
Kwa nini Yehova anampenda Sauli, na Sauli ni mtu wa aina gani?
Mwana wa Sauli anaitwa nani, na mwana huyo anafanya nini?
Kwa nini Sauli anatoa dhabihu badala ya kumngoja Samweli aitoe?
Tunajifunza nini kutokana na masimulizi juu ya Sauli?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 9:15-21 na 10:17-27.
Unyenyekevu wa Sauli ulimsaidiaje kuepuka kutenda bila kufikiria wakati wanaume fulani waliposema maneno ya kumvunjia heshima? (1 Sam. 9:21; 10:21, 22, 27; Met. 17:27)
Soma 1 Samweli 13:5-14.
Sauli alitenda dhambi gani huko Gilgali? (1 Sam. 10:8; 13:8, 9, 13)
Soma 1 Samweli 15:1-35.
Sauli alitenda dhambi gani nzito kuhusiana na Agagi, mfalme wa Waamaleki? (1 Sam. 15:2, 3, 8, 9, 22)
Sauli alitoa udhuru gani, na aliwalaumuje wengine kwa kosa lake? (1 Sam. 15:24)
Tunapaswa kutii onyo gani tunaposhauriwa? (1 Sam. 15:19-21; Zab. 141:5; Met. 9:8, 9; 11:2)
Hadithi ya 57
Mungu Anamchagua Daudi
Mvulana katika picha anaitwa nani, na tunajuaje kwamba yeye ni hodari?
Daudi anaishi wapi, na babake na babu yake wanaitwa nani?
Kwa nini Yehova anamwambia Samweli aende nyumbai kwa Yese huko Bethlehemu?
Samweli anasema nini Yese anapowaleta wana saba mbele ya Samweli?
Daudi anapoletwa, Yehova anamwambia Samweli nini?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 17:34, 35.
Matukio hayo yanakaziaje ujasiri wa Daudi na kwamba anamtegemea Yehova? (1 Sam. 17:37)
Soma 1 Samweli 16:1-14.
Maneno ya Yehova kwenye 1 Samweli 16:7 yanatusaidiaje kuepuka ubaguzi na kuwahukumu watu kwa kuangalia tu sura ya nje? (Mdo. 10:34, 35; 1 Tim. 2:4)
Kisa cha Sauli kinaonyeshaje kwamba Yehova anapoondoa roho yake takatifu, mahali pake panaweza kuchukuliwa na roho mbaya, ama tamaa ya kutenda mabaya? (1 Sam. 16:14; Mt. 12:43-45; Gal. 5:16)
Hadithi ya 58
Daudi na Goliathi
Goliathi anawatolea wanajeshi Waisraeli mwito gani wa ushindani?
Goliathi ni mkubwa kadiri gani, na Mfalme Sauli anaahidi kumpa yule atakayemwua Goliathi thawabu gani?
Daudi anasema nini Sauli anapomwambia kwamba hawezi kupigana na Goliathi kwa sababu yeye ni mvulana tu?
Anapomjibu Goliathi, Daudi anaonyeshaje kwamba anamtegemea Yehova?
Kama unavyoona katika picha, Daudi anatumia nini kumwua Goliathi, na Wafilisti wanafanya nini baada ya hapo?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 17:1-54.
Kwa nini Daudi hakuogopa, na tunawezaje kuiga ujasiri wake? (1 Sam. 17:37, 45; Efe. 6:10, 11)
Kwa nini Wakristo wanapaswa kuepuka roho ya kushindana kama ya Goliathi wanaposhiriki katika michezo mbalimbali, au katika burudani yao? (1 Sam. 17:8; Gal. 5:26; 1 Tim. 4:8)
Maneno ya Daudi yanaonyeshaje kwamba aliamini Mungu kwamba angemsaidia? (1 Sam. 17:45-47; 2 Nya. 20:15)
Masimulizi hayo yanaonyeshaje kwamba vita hivyo havikuwa vita kati ya majeshi mawili tu, bali kati ya miungu ya uwongo na Mungu wa kweli, Yehova? (1 Sam. 17:43, 46, 47)
Mabaki ya watiwa-mafuta wanaigaje mfano wa Daudi wa kumtegemea Yehova? (1 Sam. 17:37; Yer. 1:17-19; Ufu. 12:17)
Hadithi ya 59
Sababu Yampasa Daudi Akimbie
Kwa nini Sauli anamwonea Daudi wivu, lakini Yonathani, mwana wa Sauli, ni tofauti kwa njia gani?
Ni jambo gani linalotukia siku moja Daudi anapompigia Sauli kinubi?
Sauli anamwambia Daudi ni lazima afanye nini kabla ya kumwoa binti yake Mikali, na kwa nini Sauli anamwambia jambo hilo?
Daudi anapompigia Sauli kinubi, ni nini kinachotukia kwa mara ya tatu, kama picha inavyoonyesha?
Mikali anasaidiaje kumwokoa Daudi, na Daudi analazimika kufanya nini kwa miaka saba?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 18:1-30.
Upendo usioweza kuvunjwa wa Yonathani kwa Daudi, unafananishaje upendo kati ya “kondoo wengine” na “kundi dogo”? (1 Sam. 18:1; Yoh. 10:16; Luka 12:32; Zek. 8:23)
Ijapokuwa Yonathani alipaswa kurithi ufalme baada ya Sauli, andiko la 1 Samweli 18:4 linaonyeshaje kwamba Yonathani alijitiisha kabisa chini ya yule aliyechaguliwa kuwa mfalme?
Kisa cha Sauli kinaonyeshaje kwamba wivu unaweza kufanya mtu atende dhambi nzito, na jambo hilo linatupa onyo gani? (1 Sam. 18:7-9, 25; Yak. 3:14-16)
Soma 1 Samweli 19:1-17.
Yonathani alihatarisha maisha yake mwenyewe jinsi gani alipokuwa akikabiliana na Sauli? (1 Sam. 19:1, 4-6; Met. 16:14)
Hadithi ya 60
Abigaili na Daudi
Mwanamke anayekuja kumlaki Daudi katika picha anaitwa nani, naye ni mtu wa aina gani?
Nabali ni nani?
Kwa nini Daudi anawatuma baadhi ya watu wake wamwombe Nabali msaada?
Nabali anawaambia watu wa Daudi nini, na Daudi anafanya nini?
Abigaili anaonyeshaje kwamba yeye ni mwenye hekima?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 22:1-4.
Familia ya Daudi ilifanya nini kuonyesha kwamba Wakristo wanapaswa kusaidiana? (Met. 17:17; 1 The. 5:14)
Soma 1 Samweli 25:1-43.
Kwa nini Nabali anaelezwa kuwa mtu anayestahili kudhihakiwa? (1 Sam. 25:2-5, 10, 14, 21, 25)
Wake Wakristo wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Abigaili? (1 Sam. 25:32, 33; Met. 31:26; Efe. 5:24)
Abigaili alimzuia Daudi asifanye mambo gani mawili mabaya? (1 Sam. 25:31, 33; Rom. 12:19; Efe. 4:26)
Wanaume leo wanasaidiwaje kuwa na maoni ya Yehova juu ya wanawake kwa kufikiria jinsi Daudi alivyoitikia maneno ya Abigaili? (Mdo. 21:8, 9; Rom. 2:11; 1 Pet. 3:7)
Hadithi ya 61
Daudi Anafanywa Mfalme
Daudi na Abishai walifanya nini Sauli alipolala usingizi kambini mwake?
Daudi anamwuliza Sauli maswali yapi?
Baada ya kumwacha Sauli, Daudi anakwenda wapi?
Ni nini kinachomhuzunisha Daudi sana, hivi kwamba anatunga wimbo mzuri?
Daudi ana umri gani anapowekwa kuwa mfalme huko Hebroni, na baadhi ya wanawe wanaitwa nani?
Daudi anatawala katika mji gani baadaye?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Samweli 26:1-25.
Maneno ya Daudi katika 1 Samweli 26:11 yanaonyesha maoni gani kuwahusu wale walio na madaraka katika mpango wa Mungu? (Zab. 37:7; Rom. 13:2)
Tunapojitahidi sana kuwaonyesha wengine fadhili zenye upendo lakini hawaitikii, maneno ya Daudi katika 1 Samweli 26:23 yanaweza kutusaidiaje kuwa na maoni yanayofaa? (1 Fal. 8:32; Zab. 18:20)
Soma 2 Samweli 1:26.
Wakristo leo wanawezaje kukuza “upendo mkubwa” kama wa Daudi na Yonathani kwa Wakristo wenzao? (1 Pet. 4:8; Kol. 3:14; 1 Yoh. 4:12)
Soma 2 Samweli 5:1-10.
Daudi alitawala kwa miaka mingapi, naye alitawala katika miji gani miwili na kwa muda gani? (2 Sam. 5:4, 5)
Ukuu wa Daudi ulitokana na nini, na jambo hilo linatukumbusha nini leo? (2 Sam. 5:10; 1 Sam. 16:13; 1 Kor. 1:31; Flp. 4:13)
Hadithi ya 62
Matata Katika Nyumba ya Daudi
Kwa msaada wa Yehova, hatimaye nchi ya Kanaani inamilikiwa na akina nani?
Ni nini kinachotukia jioni moja Daudi anapokuwa kwenye dari la jumba lake la kifalme?
Kwa nini Yehova anamkasirikia Daudi sana?
Kama picha inavyoonyesha, Yehova anamtuma nani amwambie Daudi juu ya dhambi zake, na kulingana na mtu huyo ni nini kitakachompata Daudi?
Daudi anapata matatizo gani?
Ni nani anayewekwa kuwa mfalme wa Israeli baada ya Daudi?
Maswali ya ziada:
Soma 2 Samweli 11:1-27.
Tunalindwa jinsi gani tunapokuwa wenye shughuli nyingi katika utumishi wa Yehova?
Daudi alishawishwaje kufanya dhambi, na jambo hili linawaonya watumishi wa Yehova leo wajihadhari na nini? (2 Sam. 11:2; Mt. 5:27-29; 1 Kor. 10:12; Yak. 1:14, 15)
Soma 2 Samweli 12:1-18.
Wazee na wazazi wanaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Nathani alivyomtolea Daudi ushauri? (2 Sam. 12:1-4; Met. 12:18; Mt. 13:34)
Kwa nini Yehova alimtendea Daudi kwa rehema? (2 Sam. 12:13; Zab. 32:5; 2 Kor. 7:9, 10)
Hadithi ya 63
Sulemani Mfalme Mwenye Akili
Yehova anamwuliza Sulemani nini, naye anajibuje?
Yehova anamwahidi Sulemani nini, kwa sababu anapendezwa na ombi lake?
Wanawake wawili wanamwendea Sulemani ili atatue tatizo gani gumu?
Kama unavyoona katika picha, Sulemani anatatuaje tatizo hilo?
Maisha yakoje chini ya utawala wa Sulemani, na kwa nini?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Wafalme 3:3-28.
Wanaume ambao wamekabidhiwa madaraka katika tengenezo la Mungu wanaweza kujifunza nini kutokana na maneno ya Sulemani yanayopatikana katika 1 Wafalme 3:7? (Zab. 119:105; Met. 3:5, 6)
Ombi la Sulemani linaonyeshaje vizuri mambo yanayofaa ya kumwomba Mungu? (1 Fal. 3:9, 11; Met. 30:8, 9; 1 Yoh. 5:14)
Tunapoona jinsi Sulemani alivyotatua tatizo kati ya wale wanawake wawili kwa hekima sana, tunahakikishiwa nini kuhusu utawala wa wakati ujao wa Sulemani Mkuu, Yesu Kristo? (1 Fal. 3:28; Isa. 9:6, 7; 11:2-4)
Soma 1 Wafalme 4:29-34.
Yehova alijibuje ombi la Sulemani la moyo mtiifu? (1 Fal. 4:29)
Tukifikiria jinsi watu walivyojitahidi sana kwenda kusikia hekima ya Sulemani, tunapaswa kuwa na maoni gani kuhusu kujifunza Neno la Mungu? (1 Fal. 4:29, 34; Yoh. 17:3; 2 Tim. 3:16)
Hadithi ya 64
Sulemani Anajenga Hekalu
Inamchukua Sulemani muda gani kujenga hekalu la Yehova, na kwa nini ujenzi huo unagharimu pesa nyingi sana?
Kuna vyumba vikubwa vingapi hekaluni, na ni nini kinachowekwa katika chumba cha ndani?
Sulemani anasema nini anaposali baada ya ujenzi wa hekalu kumalizika?
Yehova anaonyeshaje kwamba amependezwa na sala ya Sulemani?
Wake wa Sulemani wanamshawishi afanye nini, na Sulemani anafanya nini hatimaye?
Kwa nini Yehova anamkasirikia Sulemani, na Yehova anamwambia nini?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Mambo ya Nyakati 28:9, 10.
Tukifikiria maneno ya Daudi katika 1 Mambo ya Nyakati 28:9, 10, tunapaswa kujitahidi kufanya nini kila siku maishani mwetu? (Zab. 19:14; Flp. 4:8, 9)
Soma 2 Mambo ya Nyakati 6:12-21, 32-42.
Sulemani alionyeshaje kwamba hakuna jengo lililojengwa na binadamu ambalo linaweza kumtosha Mungu Aliye Juu Zaidi? (2 Nya. 6:18; Mdo. 17:24, 25)
Maneno ya Sulemani katika 2 Mambo ya Nyakati 6:32, 33 yanaonyesha nini kumhusu Yehova? (Mdo. 10:34, 35; Gal. 2:6)
Soma 2 Mambo ya Nyakati 7:1-5.
Kama Waisraeli walivyosukumwa na mioyo yao kumsifu Yehova walipoona utukufu wake, sisi tunapaswa kuvutiwa kufanya nini tunapofikiria baraka za Yehova juu ya watu wake? (2 Nya. 7:3; Zab. 22:22; 34:1; 96:2)
Soma 1 Wafalme 11:9-13.
Maisha ya Sulemani yanaonyeshaje kwamba ni muhimu kuwa mwaminifu hadi mwisho? (1 Fal. 11:4, 9; Mt. 10:22; Ufu. 2:10)
Hadithi ya 65
Ufalme Unagawanywa
Watu wawili unaowaona katika picha wanaitwaje, nao ni nani?
Ahiya anafanya nini na vazi lake, na tendo hilo linamaanisha nini?
Sulemani anajaribu kumtenda Yeroboamu nini?
Kwa nini watu wanamweka Yeroboamu kuwa mfalme wa makabila kumi?
Kwa nini Yeroboamu anatengeneza ndama wawili wa dhahabu, na hali inakuwaje nchini muda mfupi baadaye?
Ni mambo gani yanayopata ufalme wa makabila mawili na hekalu la Yehova huko Yerusalemu?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Wafalme 11:26-43.
Yeroboamu alikuwa mtu wa aina gani, na Yehova alimwahidi nini kama angeshika sheria za Mungu? (1 Fal. 11:28, 38)
Soma 1 Wafalme 12:1-33.
Wazazi na wazee wa kutaniko wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano mbaya wa Rehoboamu kuhusu kutumia mamlaka vibaya? (1 Fal. 12:13; Mhu. 7:7; 1 Pet. 5:2, 3)
Vijana wanapaswa kumwendea nani ili wapate mwongozo mzuri wanapohitaji kufanya maamuzi mazito maishani? (1 Fal. 12:6, 7; Met. 1:8, 9; 2 Tim. 3:16, 17; Ebr. 13:7)
Ni nini kilichomchochea Yeroboamu aanzishe ibada ya ndama kwenye sehemu mbili, na jambo hilo lilionyeshaje kwamba hakumtegemea Yehova hata kidogo? (1 Fal. 11:37; 12:26-28)
Ni nani aliyewaongoza watu wa makabila kumi waasi ibada ya kweli? (1 Fal. 12:32, 33)
Hadithi ya 66
Yezebeli—Malkia Mbaya Sana
Yezebeli ni nani?
Kwa nini Mfalme Ahabu anahuzunika siku moja?
Yezebeli anafanya nini ili ampe mumewe Ahabu shamba la mizabibu la Nabothi?
Yehova anamtuma nani ili amwadhibu Yezebeli?
Inakuwaje Yehu anapofika kwenye jumba la kifalme la Yezebeli kama unavyoona katika picha?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Wafalme 16:29-33 na 18:3, 4.
Hali zilikuwa mbaya kadiri gani katika nchi ya Israeli Mfalme Ahabu alipotawala? (1 Fal. 14:9)
Soma 1 Wafalme 21:1-16.
Nabothi alionyeshaje ujasiri na uaminifu kwa Yehova? (1 Fal. 21:1-3; Law. 25:23-28)
Tunaweza kujifunza nini kutokana na kisa cha Ahabu kuhusu jinsi ya kukabiliana na hali zenye kuvunja moyo? (1 Fal. 21:4; Rom. 5:3-5)
Soma 2 Wafalme 9:30-37.
Tunaweza kujifunza nini kutokana na bidii ya Yehu ya kufanya mapenzi ya Yehova? (2 Fal. 9:4-10; 2 Kor. 9:1, 2; 2 Tim. 4:2)
Hadithi ya 67
Yehoshafati Anamtumaini Yehova
Yehoshafati ni nani, naye anaishi wakati gani?
. Kwa nini Waisraeli wanaogopa, na wengi wao wanafanya nini?
Yehova anajibuje sala ya Yehoshafati?
Yehova anasababisha hali gani kutokea kabla ya vita kuanza?
Tunajifunza nini kutoka kwa Yehoshafati?
Maswali ya ziada:
Soma 2 Mambo ya Nyakati 20:1-30.
Yehoshafati alionyeshaje kile ambacho watumishi waaminifu wa Mungu wanapaswa kufanya wanapokabili hatari? (2 Nya. 20:12; Zab. 25:15; 62:1)
Kwa kuwa, sikuzote Yehova ametumia njia maalumu ili kuwasiliana na watu wake, anatumia njia gani leo? (2 Nya. 20:14, 15; Mt. 24:45-47; Yoh. 15:15)
Mungu atakapoanzisha “vita vya ile siku kuu ya Mungu Mweza-Yote,” hali yetu itafananaje na ile ya Yehoshafati? (2 Nya. 20:15, 17; 32:8; Ufu. 16:14, 16)
Kama Walawi, mapainia na mishonari wanasaidiaje kuendeleza kazi ya kuhubiri ulimwenguni pote leo? (2 Nya. 20:19, 21; Rom. 10:13-15; 2 Tim. 4:2)
Hadithi ya 68
Wavulana Wawili Wanaokuwa Hai Tena
Wale watu watatu katika picha ni nani, na huyo mvulana mdogo anapatwa na nini?
Eliya anamwomba Mungu nini kumhusu mvulana huyo, na ni jambo gani linalotukia?
Msaidizi wa Eliya anaitwa nani?
Kwa nini Elisha anaitwa kwenda kwenye nyumba ya mwanamke wa Shunemu?
Elisha anafanya nini, na inakuwaje kwa mtoto huyo aliyekufa?
Yehova ana nguvu gani, kama Eliya na Elisha wanavyoonyesha?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Wafalme 17:8-24.
Utii na imani za Eliya zilijaribiwa jinsi gani? (1 Fal. 17:9; 19:1-4, 10)
Kwa nini imani ya mjane wa Zarefati inavutia sana? (1 Fal. 17:12-16; Luka 4:25, 26)
Jambo lililompata yule mjane wa Zarefati linaonyeshaje kwamba maneno ya Yesu katika Mathayo 10:41, 42 ni ya kweli? (1 Fal. 17:10-12, 17, 23, 24)
Soma 2 Wafalme 4:8-37.
Mwanamke wa Shunemu anatufundisha nini juu ya ukarimu? (2 Fal. 4:8; Luka 6:38; Rom. 12:13; 1 Yoh. 3:17)
Tunawezaje kuwatendea watumishi wa Mungu kwa fadhili leo? (Mdo. 20:35; 28:1, 2; Gal. 6:9, 10; Ebr. 6:10)
Hadithi ya 69
Msichana Anamsaidia Mwanamume Mwenye Nguvu
Yule msichana mdogo unayemwona katika picha anamwambia yule mama nini?
Mama huyo ni nani, na msichana huyo anafanya nini katika nyumba ya mama huyo?
Elisha anamweleza mtumishi wake amwambie Naamani nini, na kwa nini Naamani anakasirika?
Ni jambo gani linalotokea Naamani anapofanya kama watumishi wake wanavyopendekeza?
Kwa nini Elisha anakataa zawadi ya Naamani, lakini Gehazi anafanya nini?
Ni nini kinachompata Gehazi, na tunajifunza nini kutokana na jambo hilo?
Maswali ya ziada:
Soma 2 Wafalme 5:1-27.
Mfano wa yule msichana mdogo Mwisraeli unawezaje kuwatia vijana moyo leo? (2 Fal. 5:3; Zab. 8:2; 148:12, 13)
Kwa nini ni vizuri kukumbuka kisa cha Naamani tunapopata ushauri unaotegemea Maandiko? (2 Fal. 5:15; Ebr. 12:5, 6; Yak. 4:6)
Tunaweza kujifunza nini kwa kulinganisha mwenendo wa Elisha na wa Gehazi? (2 Fal. 5:9, 10, 14-16, 20; Mt. 10:8; Mdo. 5:1-5; 2 Kor. 2:17)
Hadithi ya 70
Yona na Samaki Mkubwa
Yona ni nani, na Yehova anamwambia afanye nini?
Yona anafanya nini kwa sababu hataki kwenda mahali ambapo Yehova anamwambia aende?
Yona anawaambia mabaharia wafanye nini ili upepo utulie?
Kama unavyoona katika picha, ni jambo gani linalotukia Yona anapozama majini?
Yona yumo ndani ya samaki mkubwa kwa muda gani, na anafanya nini akiwa humo?
Yona anakwenda wapi baada ya kutoka katika tumbo la samaki, na jambo hilo linatufundisha nini?
Maswali ya ziada:
Soma Yona 1:1-17.
Yona alihisije alipotumwa awahubirie Waninawi? (Yona 1:2, 3; Met. 3:7; Mhu. 8:12)
Soma Yona 2:1, 2, 10.
Yaliyompata Yona yanatuhakikishaje kwamba Yehova hujibu sala zetu? (Zab. 22:24; 34:6; 1 Yoh. 5:14)
Soma Yona 3:1-10.
Tunatiwaje moyo kwa kujua kwamba Yehova hakumtupilia mbali Yona ijapokuwa mwanzoni alikataa kufanya kazi aliyotumwa kufanya? (Zab. 103:14; 1 Pet. 5:10)
Mambo ambayo Yona aliona kuhusiana na Waninawi yanatuonyeshaje kwamba hatupaswi kuwa na maoni yasiyofaa juu ya watu katika eneo letu? (Yona 3:6-9; Mhu. 11:6; Mdo. 13:48)
Hadithi ya 71
Mungu Anatoa Ahadi ya Paradiso
Isaya alikuwa nani, aliishi wakati gani, na Yehova alimwonyesha nini?
Neno “paradiso” linamaanisha nini, na neno hilo linakukumbusha nini?
Yehova alimwambia Isaya aandike nini kuhusu Paradiso itakayokuja?
Kwa nini Adamu na Hawa walipoteza makao yao mazuri?
Yehova anawaahidi wale wanaompenda nini?
Maswali ya ziada:
Soma Isaya 11:6-9.
Neno la Mungu linaelezaje amani itakayokuwapo kati ya wanyama na wanadamu katika ulimwengu mpya? (Zab. 148:10, 13; Isa. 65:25; Eze. 34:25)
Maneno ya Isaya yanatimizwaje kwa njia ya kiroho miongoni mwa watu wa Yehova leo? (Rom. 12:2; Efe. 4:23, 24)
Ni nani anayepaswa kusifiwa kwa sababu ya mabadiliko ambayo watu hufanya kuhusiana na nyutu zao sasa na mabadiliko watakayofanya katika ulimwengu mpya? (Isa. 48:17, 18; Gal. 5:22, 23; Flp. 4:7)
Soma Ufunuo 21:3, 4.
Maandiko yanaonyeshaje kwamba Mungu atakaa pamoja na wanadamu kwa njia ya mfano, wala hatakaa duniani kihalisi? (Law. 26:11, 12; 2 Nya. 6:18; Isa. 66:1; Ufu. 21:2, 3, 22-24)
Ni machozi na maumivu ya aina gani ambayo hayatakuwapo tena? (Luka 8:49-52; Rom. 8:21, 22; Ufu. 21:4)
Hadithi ya 72
Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia
Mtu unayemwona katika picha ni nani, na kwa nini yuko tabaani?
Ni barua gani ambazo Hezekia ameweka mbele za Mungu, na Hezekia anamwomba Yehova nini?
Je, Hezekia ni mfalme mzuri au mbaya, na Yehova anamtuma Isaya ampelekee ujumbe gani?
Kama picha inavyoonyesha, malaika wa Yehova anawafanya Waashuru nini?
Ijapokuwa ufalme wa makabila mawili una amani kwa muda, ni nini kinachotokea baada ya kifo cha Hezekia?
Maswali ya ziada:
Soma 2 Wafalme 18:1-36.
Msemaji wa Waashuru anayeitwa Rabshake alijaribu kudhoofisha imani ya Waisraeli jinsi gani? (2 Fal. 18:19, 21; Kut. 5:2; Zab. 64:3)
Mashahidi wa Yehova hufuataje mfano wa Hezekia wanapokabili wapinzani? (2 Fal. 18:36; Zab. 39:1; Met. 26:4; 2 Tim. 2:24)
Soma 2 Wafalme 19:1-37.
Watu wa Yehova humwigaje Hezekia wakati wa taabu? (2 Fal. 19:1, 2; Met. 3:5, 6; Ebr. 10:24, 25; Yak. 5:14, 15)
Mfalme Senakeribu alishindwaje kwa njia tatu, naye anamfananisha nani kinabii? (2 Fal. 19:32, 35, 37; Ufu. 20:2, 3)
Soma 2 Wafalme 21:1-6, 16.
Kwa nini tunaweza kusema kwamba Manase alikuwa mmojawapo wa wafalme wabaya zaidi ambao walitawala huko Yerusalemu? (2 Nya. 33:4-6, 9)
Hadithi ya 73
Mfalme Mzuri wa Mwisho wa Israeli
Yosia ana umri gani anapowekwa kuwa mfalme, naye anaanza kufanya nini baada ya kutawala kwa miaka saba?
Unamwona Yosia akifanya nini katika picha ya kwanza?
Kuhani Mkuu anapata nini watu wanapotengeneza hekalu?
Kwa nini Yosia anararua mavazi yake?
Nabii wa kike Hulda anampa Yosia ujumbe gani kutoka kwa Yehova?
Maswali ya ziada:
Soma 2 Mambo ya Nyakati 34:1-28.
Kwa nini Yosia ni mfano mzuri kwa wale waliovumilia hali ngumu utotoni? (2 Nya. 33:21-25; 34:1, 2; Zab. 27:10)
Yosia alichukua hatua gani muhimu ili kuendeleza ibada ya kweli katika mwaka wa 8, 12, na 18 wa utawala wake? (2 Nya. 34:3, 8)
Mfalme Yosia na Kuhani Mkuu Hilkia wanatufundisha nini kuhusu kudumisha majengo yetu ya ibada katika hali nzuri? (2 Nya. 34:9-13; Met. 11:14; 1 Kor. 10:31)
Hadithi ya 74
Mwanamume Asiyeogopa
Mwanamume kijana katika picha ni nani?
Yeremia anaonaje anapowekwa kuwa nabii, lakini Yehova anamwambia nini?
Yeremia anaendelea kuwaambia watu ujumbe gani?
Makuhani wanajaribu kumzuia Yeremia kwa njia gani, lakini anaonyeshaje kwamba haogopi?
Ni jambo gani linalowapata Waisraeli kwa sababu hawaachi njia zao mbaya?
Maswali ya ziada:
Soma Yeremia 1:1-8.
Kama kisa cha Yeremia kinavyoonyesha, ni nini kinachomstahilisha mtu kuwa mtumishi wa Yehova? (2 Kor. 3:5, 6)
Mfano wa Yeremia unawatiaje vijana Wakristo moyo leo? (Mhu. 12:1; 1 Tim. 4:12)
Soma Yeremia 10:1-5.
Yeremia anatoa mfano gani ili kuonyesha ubatili wa kutegemea sanamu? (Yer. 10:5; Isa. 46:7; Hab. 2:19)
Soma Yeremia 26:1-16.
Mabaki ya watiwa-mafuta wanapotoa onyo leo, wametii jinsi gani agizo la Yehova kwa Yeremia la ‘kutoondoa hata neno moja’? (Yer. 26:2; Kum. 4:2; Mdo. 20:27)
Yeremia aliwawekea mfano gani mzuri Mashahidi wa Yehova leo wanaotangazia mataifa onyo la Yehova? (Yer. 26:8, 12, 14, 15; 2 Tim. 4:1-5)
Soma 2 Wafalme 24:1-17.
Wayahudi walipatwa na mambo gani yenye kuhuzunisha kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Yehova? (2 Fal. 24:2-4, 14)
Hadithi ya 75
Wavulana Wanne Babeli
Wale wavulana wanne unaowaona katika picha ni nani, na kwa nini wako Babeli?
Nebukadneza anawapangia wavulana hao nini, na anawapa watumishi wake amri gani?
Danieli anaomba nini kuhusu chakula na vinywaji kwa niaba yake mwenyewe na rafiki zake watatu?
Baada ya kula mboga tu kwa siku kumi, afya ya Danieli na ya rafiki zake ikoje ikilinganishwa na ya wale wanaume wengine vijana?
Kwa nini Danieli na rafiki zake watatu wako katika jumba la mfalme, na wanawashindaje makuhani na watu wenye akili?
Maswali ya ziada:
Soma Danieli 1:1-21.
Ni jitihada ya aina gani inayohitajika tukitaka kushinda vishawishi na udhaifu mbalimbali? (Dan. 1:8; Mwa. 39:7, 10; Gal. 6:9)
Vijana leo wanaweza kushawishiwa au kushurutishwa kwa njia zipi wafurahie kile ambacho wengine huenda wakasema ni vitu “vitamu”? (Dan. 1:8; Met. 20:1; 2 Kor. 6:17–7:1)
Masimulizi ya Biblia kuhusu wale vijana wanne Waebrania yanatusaidia kuelewa nini kuhusu elimu ya ulimwengu? (Dan. 1:20; Isa. 54:13; 1 Kor. 3:18-20)
Hadithi ya 76
Yerusalemu Unaharibiwa
Ni nini kinachopata Yerusalemu na Waisraeli unaowaona katika picha?
Ezekieli ni nani, na Yehova anamwonyesha mambo gani yenye kushtua?
Yehova anasema atafanya nini kwa sababu Waisraeli hawamheshimu?
Mfalme Nebukadneza anafanya nini baada ya Waisraeli kumwasi?
Kwa nini Yehova anaruhusu uharibifu huo mkubwa kuwapata Waisraeli?
Nchi ya Israeli inaachwa bila watu jinsi gani, na kwa muda gani?
Maswali ya ziada:
Soma 2 Wafalme 25:1-26.
Zedekia alikuwa nani, alipatwa na nini, na jambo hilo lilitimizaje unabii wa Biblia?
Yehova aliwalaumu nani kwa makosa yote ambayo Waisraeli walikuwa wametenda? (2 Fal. 25:9, 11, 12, 18, 19; 2 Nya. 36:14, 17)
Soma Ezekieli 8:1-18.
Dini zinazojidai kuwa za Kikristo zimeigaje Waisraeli waasi walioabudu jua? (Eze. 8:16; Isa. 5:20, 21; Yoh. 3:19-21; 2 Tim. 4:3)
Hadithi ya 77
Walikataa Kuabudu
Mfalme Nebukadneza wa Babeli amewapa watu amri gani?
Kwa nini rafiki watatu za Danieli hawaiabudu sanamu ya dhahabu?
Nebukadneza anapowapa wale Waebrania watatu nafasi nyingine ya kuabudu, wanaonyeshaje kwamba wanamtegemea Yehova?
Nebukadneza anawaamuru watu wake wawachukulie Shadraka, Meshaki, na Abednego hatua gani?
Nebukadneza anaona nini anapochungulia ndani ya tanuru?
Kwa nini mfalme anamsifu Mungu wa Shadraka, Meshaki, na Abednego, nao ni mfano kwetu kwa njia gani?
Maswali ya ziada:
Soma Danieli 3:1-30.
Wale vijana watatu Waebrania walikuwa na mtazamo gani ambao watumishi wote wa Mungu wanapaswa kuiga wanapokabili majaribu ya imani yao? (Dan. 3:17, 18; Mt. 10:28; Rom. 14:7, 8)
Yehova Mungu alimfundisha Nebukadneza jambo gani muhimu? (Dan. 3:28, 29; 4:34, 35)
Hadithi ya 78
Mwandiko wa Mkono Ukutani
Ni jambo gani linalotokea mfalme wa Babeli anapofanya karamu kubwa na kutumia mabakuli na vikombe vilivyochukuliwa kutoka katika hekalu la Yehova Yerusalemu?
Belshaza anawaambia watu wenye akili nini, nao wanashindwa kufanya nini?
Mamake mfalme anamwambia afanye nini?
Kama Danieli anavyomwambia mfalme, kwa nini Mungu ametuma mkono uandike ukutani?
Danieli anafafanuaje maana ya maneno yaliyoandikwa ukutani?
Ni jambo gani linalotukia huku Danieli akiongea?
Maswali ya ziada:
Soma Danieli 5:1-31.
Onyesha tofauti kati ya woga wa Kimungu na woga ambao Belshaza alihisi alipoona maandishi ukutani? (Dan. 5:6, 7; Zab. 19:9; Rom. 8:35-39)
Danieli alionyeshaje ujasiri mwingi alipoongea na Belshaza na wakuu katika utawala wake? (Dan. 5:17, 18, 22, 26-28; Mdo. 4:29)
Sura ya 5 ya kitabu cha Danieli inakaziaje enzi kuu ya Yehova? (Dan. 4:17, 25; 5:21)
Hadithi ya 79
Danieli Katika Shimo la Simba
Dario ni nani, naye anamwonaje Danieli?
Watu fulani wenye wivu wanamshawishi Dario afanye nini?
Danieli anafanya nini anaposikia kuhusu ile sheria mpya?
Kwa nini Dario ana wasiwasi sana hivi kwamba anakosa usingizi, na anafanya nini asubuhi inayofuata?
Danieli anamjibuje Dario?
Inakuwaje kwa wale watu wabaya waliojaribu kumwua Danieli, na Dario anawaandikia watu wote katika ufalme wake barua kuhusu nini?
Maswali ya ziada:
Soma Danieli 6:1-28.
Njama iliyotungwa juu ya Danieli inatukumbushaje kile ambacho wapinzani wamefanya ili kuzuia kazi ya Mashahidi wa Yehova siku hizi? (Dan. 6:7; Zab. 94:20; Isa. 10:1; Rom. 8:31)
Watumishi wa Mungu leo wanawezaje kumwiga Danieli kwa kuendelea kujitiisha kwa “mamlaka zilizo kubwa”? (Dan. 6:5, 10; Rom. 13:1; Mdo. 5:29)
Tunawezaje kumwiga Danieli kwa kumtumikia Yehova “daima”? (Dan. 6:16, 20; Flp. 3:16; Ufu. 7:15)
Hadithi ya 80
Watu wa Mungu Wanatoka Babeli
Kama picha inavyoonyesha, Waisraeli wanafanya nini?
Koreshi alitimizaje unabii wa Yehova uliotolewa na Isaya?
Koreshi anawaambia Waisraeli wasioweza kurudi Yerusalemu nini?
Koreshi anawapa watu vitu gani ili wavirudishe Yerusalemu?
Inawachukua Waisraeli muda gani kurudi Yerusalemu?
Ni miaka mingapi ambayo imepita tangu nchi ilipoachwa bila watu?
Maswali ya ziada:
Soma Isaya 44:28 na 45:1-4.
Yehova alikaziaje kwamba unabii kumhusu Koreshi ungetimizwa hakika? (Isa. 55:10, 11; Rom. 4:17)
Unabii wa Isaya kumhusu Koreshi unaonyesha nini kuhusu uwezo wa Yehova Mungu wa kutabiri mambo ya wakati ujao? (Isa. 42:9; 45:21; 46:10, 11; 2 Pet. 1:20)
Soma Ezra 1:1-11.
Kwa kufuata mfano wa wale ambao hawakuweza kurudi Yerusalemu, tunawezaje ‘kuitia nguvu mikono’ ya wale ambao wanaweza kuwa watumishi wa wakati wote? (Ezra 1:4, 6; Rom. 12:13; Kol. 4:12)
Hadithi ya 81
Kuutumainia Msaada wa Mungu
Ni watu wangapi wanaofunga safari ndefu kutoka Babeli hadi Yerusalemu, lakini wanakuta hali gani wanapofika?
Waisraeli wanaanza kujenga nini baada ya kufika, lakini adui zao wanafanya nini?
Hagai na Zekaria ni nani, nao wanawaambia watu nini?
Kwa nini Tatenai anatuma barua hadi Babeli, na anapata jibu gani?
Ezra anafanya nini anaposikia kwamba hekalu la Mungu linahitaji kutengenezwa?
Ezra anasali kuhusu nini katika picha, sala yake inajibiwaje, na jambo hilo linatufundisha nini?
Maswali ya ziada:
Soma Ezra 3:1-13.
Tukijikuta katika eneo ambako hakuna kutaniko la watu wa Mungu, tunapaswa kuendelea kufanya nini? (Ezra 3:3, 6; Mdo. 17:16, 17; Ebr. 13:15)
Soma Ezra 4:1-7.
Zerubabeli aliwawekea watu wa Yehova mfano gani kuhusu kuchanganya dini? (Kut. 34:12; 1 Kor. 15:33; 2 Kor. 6:14-17)
Soma Ezra 5:1-5, 17 na 6:1-22.
Kwa nini wapinzani hawakufaulu kuzuia ujenzi wa hekalu? (Ezra 5:5; Isa. 54:17)
Hatua ya wanaume wazee wa Wayahudi inawatiaje wazee Wakristo moyo watafute mwongozo wa Yehova wanapokabili wapinzani? (Ezra 6:14; Zab. 32:8; Rom. 8:31; Yak. 1:5)
Soma Ezra 8:21-23, 28-36.
Kabla hatujachukua hatua fulani, ingekuwa jambo la hekima kuiga mfano gani wa Ezra? (Ezra 8:23; Zab. 127:1; Met. 10:22; Yak. 4:13-15)
Hadithi ya 82
Mordekai na Esta
Mordekai na Esta ni nani?
Kwa nini Mfalme Ahasuero anataka mke mpya, na anamchagua nani?
Hamani ni nani, na kwa nini amekasirika sana?
Ni sheria gani inayotungwa, na Esta anafanya nini baada ya kupata ujumbe kutoka kwa Mordekai?
Inakuwaje kwa Hamani na Mordekai?
Waisraeli wanaepukaje kuuawa na adui zao?
Maswali ya ziada:
Soma Esta 2:12-18.
Esta alionyeshaje faida ya kuwa na “roho ya utulivu na ya upole”? (Esta 2:15; 1 Pet. 3:1-5)
Soma Esta 4:1-17.
Kama Esta alivyopata nafasi ya kuchukua hatua ili kutetea ibada ya kweli, sisi tuna nafasi gani ya kuonyesha ujitoaji na uaminifu wetu kwa Yehova leo? (Esta 4:13, 14; Mt. 5:14-16; 24:14)
Soma Esta 7:1-6.
Wengi kati ya watu wa Mungu leo wamekabilije mateso kama Esta? (Esta 7:4; Mt. 10:16-22; 1 Pet. 2:12)
Hadithi ya 83
Kuta za Yerusalemu
Waisraeli walihisije kuhusu kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomoka?
Nehemia ni nani?
Nehemia anafanya kazi gani, na kwa nini kazi hiyo ni muhimu?
Ni habari gani inayomhuzunisha Nehemia, na anafanya nini?
Mfalme Artashasta anamtendeaje Nehemia kwa fadhili?
Nehemia anapangaje ujenzi ili adui za Waisraeli wasiweze kuuzuia?
Maswali ya ziada:
Soma Nehemia 1:4-6 na 2:1-20.
Nehemia alitafutaje mwongozo wa Yehova? (Neh. 2:4, 5; Rom. 12:12; 1 Pet. 4:7)
. Soma Nehemia 3:3-5.
Wazee na watumishi wa huduma wanaweza kujifunza nini kutokana na tofauti iliyokuwapo kati ya Watekoa na watu wao “walio mashuhuri”? (Neh. 3:5, 27; 2 The. 3:7-10; 1 Pet. 5:5)
Soma Nehemia 4:1-23.
Ni nini kilichowasukuma Waisraeli waendelee kujenga licha ya upinzani mkali? (Neh. 4:6, 8, 9; Zab. 50:15; Isa. 65:13, 14)
Mfano wa Waisraeli unatutiaje moyo leo?
Soma Nehemia 6:15.
Ujenzi wa kuta za Yerusalemu uliochukua muda usiozidi miezi miwili unaonyesha nini kuhusu nguvu ya imani? (Zab. 56:3, 4; Mt. 17:20; 19:26)
Hadithi ya 84
Malaika Anamtembelea Mariamu
Mwanamke unayemwona katika picha ni nani?
Gabrieli anamwambia Mariamu nini?
Gabrieli anamwelezaje Mariamu kwamba atapata mimba na kuzaa mtoto ijapokuwa hajaishi pamoja na mwanamume?
Ni jambo gani linalotukia Mariamu anapomtembelea Elisabeti?
Yusufu anafikiri nini anapoelezwa kwamba Mariamu ana mimba, lakini kwa nini anabadili maoni yake?
Maswali ya ziada:
Soma Luka 1:26-56.
Andiko la Luka 1:35 linaonyeshaje kwamba kutokamilika kunakotokana na Adamu hakuathiri yai la Mariamu wakati uhai wa Mwana wa Mungu ulipohamishwa kutoka mbinguni? (Hag. 2:11-13; Yoh. 6:69; Ebr. 7:26; 10:5)
Yesu aliheshimiwaje hata kabla hajazaliwa? (Luka 1:41-43)
Mariamu ni mfano mzuri jinsi gani kwa Wakristo wanaopewa mapendeleo ya pekee ya utumishi? (Luka 1:38, 46-49; 17:10; Met. 11:2)
Soma Mathayo 1:18-25.
Ijapokuwa Yesu hakuitwa Imanueli, alitimizaje maana ya jina hilo alipokuwa mwanadamu? (Mt. 1:22, 23; Yoh. 14:8-10; Ebr. 1:1-3)
Hadithi ya 85
Yesu Anazaliwa Katika Boma la Ng’ombe
Mtoto mchanga katika picha ni nani, na Mariamu anamweka wapi?
Kwa nini Yesu alizaliwa katika boma la ng’ombe?
Katika picha, watu wanaoingia katika boma la ng’ombe ni nani, na malaika alikuwa amewaambia nini?
Kwa nini Yesu ni mtoto wa pekee?
Kwa nini tunaweza kumwita Yesu Mwana wa Mungu?
Maswali ya ziada:
Soma Luka 2:1-20.
Kaisari Augusto alisaidiaje kutimiza unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu? (Luka 2:1-4; Mika 5:2)
Mtu anapataje kuwa miongoni mwa wale wanaoitwa “watu wa nia njema”? (Luka 2:14; Mt. 16:24; Yoh. 17:3; Mdo. 3:19; Ebr. 11:6)
Ikiwa wale wachungaji wapole Wayahudi walikuwa na sababu ya kushangilia wakati Mwokozi alipozaliwa, watumishi wa Mungu wana sababu gani kuu zaidi ya kushangilia leo? (Luka 2:10, 11; Efe. 3:8, 9; Ufu. 11:15; 14:6)
Hadithi ya 86
Wanaume Walioongozwa na Nyota
Wanaume walio katika picha ni nani, na kwa nini mmoja wao anaelekeza kidole kwenye nyota nyang’avu?
. Kwa nini Mfalme Herode anakasirika, na anafanya nini?
Nyota hiyo nyang’anvu inawaongoza wanaume hao wapi, lakini kwa nini wanapitia njia nyingine wanaporudi nchini mwao?
Herode anatoa amri gani, na kwa nini?
Yehova anamwambia Yusufu afanye nini?
. Ni nani aliyefanya nyota hiyo mpya ing’ae, na kwa nini?
Swali la ziada:
Soma Mathayo 2:1-23.
Yesu alikuwa na umri gani na aliishi wapi wakati wanajimu walipomtembelea? (Mt. 2:1, 11, 16))
Hadithi ya 87
Kijana Yesu Katika Hekalu
Yesu ana umri gani katika picha hii, na yuko wapi?
Yusufu huipeleka familia yake wapi kila mwaka?
Baada ya kusafiri kwa siku moja kurudi nyumbani, kwa nini Yusufu na Mariamu wanarudi Yerusalemu?
Yusufu na Mariamu wanampata Yesu wapi, na kwa nini watu wanashangaa?
Yesu anamwambia mamake Mariamu nini?
Tunawezaje kumwiga Yesu kwa kujifunza juu ya Mungu?
Maswali ya ziada:
Soma Luka 2:41-52.
Ijapokuwa Sheria iliagiza wanaume tu wahudhurie sherehe za kila mwaka, Yusufu na Mariamu waliweka mfano gani mzuri kwa wazazi leo? (Luka 2:41; Kum. 16:16; 31:12; Met. 22:6)
Yesu aliwawekeaje vijana leo mfano mzuri kuhusiana na kutii wazazi wao? (Luka 2:51; Kum. 5:16; Met. 23:22; Kol. 3:20)
Soma Mathayo 13:53-56.
Ndugu wanne wa Yesu wanaotajwa katika Biblia wanaitwa nani, na wawili kati yao walipata mapendeleo gani katika kutaniko la Kikristo? (Mt. 13:55; Mdo. 12:17; 15:6, 13; 21:18; Gal. 1:19; Yak. 1:1; Yuda 1)
Hadithi ya 88
Yohana Anambatiza Yesu
Wale watu wawili katika picha ni nani?
Mtu hubatizwa jinsi gani?
Yohana huwa anabatiza akina nani?
Yesu anamwomba Yohana ambatize kwa sababu gani ya pekee?
Mungu anaonyeshaje kwamba anapendezwa na ubatizo wa Yesu?
Ni jambo gani linalotokea Yesu anapokwenda mahali pasipo na watu kwa siku 40?
Baadhi ya wafuasi, au wanafunzi wa kwanza wa Yesu ni nani, na mwujiza wake wa kwanza ni gani?
Maswali ya ziada?
Soma Mathayo 3:13-17.
Yesu aliwekeaje mfano wa jinsi wanafunzi wake walivyopaswa kubatizwa? (Zab. 40:7, 8; Mt. 28:19, 20; Luka 3:21, 22)
Soma Mathayo 4:1-11.
Tunatiwaje moyo kujifunza Biblia kwa ukawaida kutokana na jinsi Yesu alivyotumia Maandiko kwa ustadi sana? (Mt. 4:5-7; 2 Pet. 3:17, 18; 1 Yoh. 4:1)
. Soma Yohana 1:29-51.
Yohana Mbatizaji aliwaelekeza wanafunzi wake kwa nani, na tunawezaje kumwiga leo? (Yoh. 1:29, 35, 36; 3:30; Mt. 23:10)
Soma Yohana 2:1-12.
Mwujiza wa kwanza wa Yesu unaonyeshaje kwamba Yehova hawanyimi watu Wake vitu vizuri? (Yoh. 2:9, 10; Zab. 84:11; Yak. 1:17)
Hadithi ya 89
Yesu Anasafisha Hekalu
Kwa nini wanyama wanauzwa hekaluni?
Yesu anakasirishwa na nini?
Yesu anafanya nini kama unavyoona katika picha, na anawaamuru watu wanaowauza njiwa wafanye nini?
Wafuasi wa Yesu wanakumbuka nini wanapoona jambo hilo?
Yesu anapitia wilaya gani anaporudi Galilaya?
Swali la ziada:
Soma Yohana 2:13-25.
Tukifikiria jinsi Yesu alivyokasirika kwa sababu watu walibadili pesa hekaluni, je, tunapaswa kuwa na maoni gani kuhusu kushughulikia mambo ya biashara kwenye Jumba la Ufalme? (Yoh. 2:15, 16; 1 Kor. 10:24, 31-33)
Hadithi ya 90
Pamoja na Mwanamke Penye Kisima
Kwa nini Yesu ametua kwenye kisima huko Samaria, na anamwambia mwanamke mmoja nini?
Kwa nini mwanamke huyo anashangaa, Yesu anamwambia nini, na kwa nini?
Mwanamke huyo anafikiri Yesu anaongea kuhusu maji ya aina gani, lakini Yesu anaongea juu ya maji gani?
. Kwa nini mwanamke huyo anashangaa kusikia kwamba Yesu anajua mambo mengi kumhusu, na Yesu anajuaje mambo hayo?
Tunaweza kujifunza nini kutokana na masimulizi kumhusu mwanamke huyo kwenye kisima?
Maswali ya ziada:
Soma Yohana 4:5-43.
Kwa kufuata mfano wa Yesu, tunapaswa kuwa na maoni gani kuwahusu watu wa rangi au jamii nyingine? (Yoh 4:9; 1 Kor. 9:22; 1 Tim. 2:3, 4; Tito 2:11)
Mtu ambaye anakuwa mwanafunzi wa Yesu anapata faida gani za kiroho? (Yoh. 4:14; Isa. 58:11; 2 Kor. 4:16)
Tunawezaje kuonyesha uthamini kama mwanamke huyo Msamaria, aliyekuwa na hamu ya kuwaambia wengine yale aliyojifunza? (Yoh. 4:7, 28; Mt. 6:33; Luka 10:40-42)
Hadithi ya 91
Yesu Anafundisha Juu ya Mlima
Yesu anafundisha akiwa wapi kama picha inavyoonyesha, na wale ambao wameketi karibu naye ni nani?
Mitume 12 wanaitwa nani?
Ufalme ambao Yesu anahubiri kuuhusu ni nini?
Yesu anawafundisha watu kusali kuhusu mambo gani?
Yesu anasema nini juu ya jinsi watu wanavyopaswa kutendeana?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 5:1-12.
Tunaweza kuonyesha kwa njia zipi kwamba tunatambua uhitaji wetu wa kiroho? (Mt. 5:3; Rom. 10:13-15; 1 Tim. 4:13, 15, 16)
Soma Mathayo 5:21-26.
Andiko la Mathayo 5:23, 24 linakaziaje kwamba uhusiano wetu pamoja na Yehova unaweza kuathiriwa tusipokuwa na uhusiano mzuri pamoja na ndugu zetu? (Mt. 5:23, 24; 6:14, 15; Zab. 133:1; Kol. 3:13; 1 Yoh. 4:20)
Soma Mathayo 6:1-8.
Wakristo wanapaswa kuepuka kujivunia uadilifu wao kuhusiana na mambo gani? (Luka 18:11, 12; 1 Kor. 4:6, 7; 2 Kor. 9:7)
Soma Mathayo 6:25-34.
Yesu alifundisha nini kuhusu uhitaji wa kumtegemea Yehova ili tupate mahitaji ya kimwili? (Kut. 16:4; Zab. 37:25; Flp. 4:6)
Soma Mathayo 7:1-11.
Mfano unaovutia sana katika Mathayo 7:5 unatufundisha nini? (Met. 26:12; Rom. 2:1; 14:10; Yak. 4:11, 12)
Hadithi ya 92
Yesu Anawafufua Wafu
Ni nani baba ya msichana unayemwona katika picha, na kwa nini yeye na mkewe walikuwa na wasiwasi mwingi sana?
Yairo anafanya nini anapompata Yesu?
Ni jambo gani linalotukia Yesu anapoelekea nyumbani kwa Yairo, na Yairo anapata ujumbe gani njiani?
Kwa nini watu walio nyumbani kwa Yairo wanamcheka Yesu?
Yesu anafanya nini baada ya kuingia katika chumba cha msichana pamoja na mitume watatu na baba na mama ya msichana huyo?
Yesu amemfufua nani mwingine, na jambo hilo linaonyesha nini?
Maswali ya ziada:
. Soma Luka 8:40-56.
Yesu alionyeshaje huruma na usawaziko alipomponya mwanamke mwenye mtiririko wa damu, na wazee Wakristo wanaweza kujifunza nini kutokana na jambo hilo? (Luka 8:43, 44, 47, 48; Law. 15:25-27; Mt. 9:12, 13; Kol. 3:12-14)
Soma Luka 7:11-17.
Kwa nini wale waliofiwa na wapendwa wao wanaweza kufarijiwa sana na jinsi Yesu alivyomtendea mjane wa Naini? (Luka 7:13; 2 Kor. 1:3, 4; Ebr. 4:15)
Soma Yohana 11:17-44.
Yesu alionyeshaje kwamba ni jambo la kawaida kuhuzunika mpendwa anapokufa? (Yoh. 11:33-36, 38; 2 Sam. 18:33; 19:1-4)
Hadithi ya 93
Yesu Analisha Watu Wengi Chakula
Ni jambo gani baya sana ambalo limempata Yohana Mbatizaji, na Yesu anahisije?
Yesu anawalishaje watu wengi ambao wamemfuata, na ni kiasi gani cha chakula kinachobaki?
Kwa nini wanafunzi wanaogopa usiku, na Petro anafanya nini?
Yesu anawalishaje maelfu ya watu kwa mara ya pili?
Kwa nini tutafurahi sana Yesu atakapoitawala dunia akiwa Mfalme aliyewekwa na Mungu?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 14:1-32.
Masimulizi katika Mathayo 14:23-32 yanatusaidia kujua sifa gani ya Petro?
Maandiko yanaonyeshaje kwamba Petro alikomaa na kuacha kutenda bila kufikiri? (Mt. 14:27-30; Yoh. 18:10; 21:7; Mdo. 2:14, 37-40; 1 Pet. 5:6, 10)
Soma Mathayo 15:29-38.
Yesu alionyeshaje heshima kwa vitu vya kimwili ambavyo Baba yake aliandaa? (Mt. 15:37; Yoh. 6:12; Kol. 3:15)
Soma Yohana 6:1-21.
Wakristo leo wanawezaje kuiga mfano wa Yesu katika mambo yanayohusisha serikali? (Yoh. 6:15; Mt. 22:21; Rom. 12:2; 13:1-4)
Hadithi ya 94
Anawapenda Watoto Wadogo
Mitume wanabishania nini wanaporudi nyumbani baada ya safari ndefu?
Kwa nini Yesu anamwita mtoto mdogo na kumleta katikati ya mitume?
Mitume wanapaswa kujizoeza kuwa kama watoto kwa njia gani?
Miezi michache baadaye, Yesu anaonyeshaje kwamba anawapenda watoto?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 18:1-4.
Kwa nini Yesu alitumia vielelezi alipofundisha? (Mt. 13:34, 36; Marko 4:33, 34)
Soma Mathayo 19:13-15.
Ni lazima tuziige sifa gani za watoto wadogo tukitaka kupata baraka za Ufalme? (Zab. 25:9; 138:6; 1 Kor. 14:20)
Soma Marko 9:33-37.
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake nini kuhusu kutamani vyeo vya umashuhuri? (Marko 9:35; Mt. 20:25, 26; Gal. 6:3; Flp. 2:5-8)
Soma Marko 10:13-16.
Watu walijisikia huru kadiri gani kumwendea Yesu, na wazee Wakristo wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano wake? (Marko 6:30-34; Flp. 2:1-4; 1 Tim. 4:12)
Hadithi ya 95
Namna Yesu Anavyofundisha
. Mwanamume mmoja anamwuliza Yesu swali gani, na kwa nini?
Yesu anatumia nini mara kwa mara anapofundisha, na tayari tumejifunza nini kuwahusu Wayahudi na Wasamaria?
Katika hadithi ya Yesu, ni jambo gani linalompata Myahudi aliye njiani kwenda Yeriko?
Ni jambo gani linalotukia wakati kuhani Myahudi na Mlawi wanapopita kwenye njia hiyo?
Ni nani anayemsaidia Myahudi aliyeumia, kama picha inavyoonyesha?
. Baada ya Yesu kumaliza kusimulia hadithi hiyo, anauliza swali gani, na mtu huyo anajibuje?
Maswali ya ziada:
Soma Luka 10:25-37.
Badala ya kumjibu moja kwa moja, Yesu alimsaidiaje mtu anayejua Sheria vizuri kufikiria habari fulani ili yeye mwenyewe afikie mkataa? (Luka 10:26; Mt. 16:13-16)
Yesu alitumiaje mifano ili kuwasaidia wasikilizaje wake waache ubaguzi? (Luka 10:36, 37; 18:9-14; Tito 1:9)
Hadithi ya 96
Yesu Anaponya Wagonjwa
Yesu anafanya nini anapotembea huku na huku nchini?
Miaka mitatu hivi baada ya ubatizo wake, anawaambia mitume wake nini?
Watu unaowaona katika picha ni nani, na Yesu anamsaidiaje mwanamke huyo?
Kwa nini jibu la Yesu linawaaibisha viongozi wa dini wanaolalamikia mwujiza wa Yesu?
Yesu na mitume wake wanapokaribia Yeriko, Yesu anawasaidiaje vipofu wawili wanaoomba-omba?
Kwa nini Yesu anafanya miujiza?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 15:30, 31.
Yesu anaonyeshaje nguvu za Yehova kwa njia ya ajabu, nasi tunapaswa kuonaje yale ambayo Yehova ameahidi kuhusu ulimwengu mpya? (Zab. 37:29; Isa. 33:24)
Soma Luka 13:10-17.
Yesu alifanya baadhi ya miujiza yake yenye kuvutia sana katika siku za Sabato. Jambo hilo linaonyesha nini kuhusu kitulizo ambacho atawaletea wanadamu wakati wa Utawala wake wa Miaka Elfu? (Luka 13:10-13; Zab. 46:9; Mt. 12:8; Kol. 2:16, 17; Ufu. 21:1-4)
Soma Mathayo 20:29-34.
Masimulizi haya yanaonyeshaje kwamba Yesu hakujihisi kuwa na shughuli nyingi mno asiweze kuwasaidia watu, na tunaweza kujifunza nini kutokana na jambo hilo? (Kum. 15:7; Yak. 2:15, 16; 1 Yoh. 3:17)
Hadithi ya 97
Yesu Aja Kama Mfame
Yesu anapofika kwenye kijiji kidogo karibu na Yerusalemu, anawaambia wanafunzi wake wafanye nini?
Kama unavyoona katika picha, ni jambo gani linalotukia Yesu anapokaribia mji wa Yerusalemu?
Watoto wadogo wanafanya nini wanapomwona Yesu akiwaponya watu walio vipofu na vilema?
Yesu anawaambia nini makuhani ambao wamekasirika?
Tunawezaje kuwa kama wale watoto wanaomsifu Yesu?
Wanafunzi wanataka kujua nini?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 21:1-17.
Yesu aliingiaje Yerusalemu akiwa Mfalme kwa njia tofauti sana kulinganishwa na majemadari washindi nyakati za Waroma? (Mt. 21:4, 5; Zek 9:9; Flp. 2:5-8; Kol. 2:15)
Vijana wanaweza kujifunza nini kutokana na wavulana Waisraeli walionukuu maneno ya Zaburi 118 Yesu alipoingia hekaluni? (Mt. 21:9, 15; Zab. 118:25, 26; 2 Tim. 3:15; 2 Pet. 3:18)
Soma Yohana 12:12-16.
Matawi ya mitende ambayo watu walitumia kumlaki Yesu yanafananisha nini? (Yoh. 12:13; Flp. 2:10; Ufu. 7:9, 10)
Hadithi ya 98
Juu ya Mlima wa Mizeituni
Katika picha, Yesu ni nani, na ni nani walio pamoja naye?
Makuhani walijaribu kumfanya Yesu nini hekaluni, lakini Yesu akawaambia nini?
Mitume wanamwuliza Yesu nini?
Kwa nini Yesu anawatajia mitume wake baadhi ya mambo yangetokea duniani wakati ambapo angeanza kutawala akiwa Mfalme mbinguni?
Yesu anasema ni nini kitakachotukia kabla hajakomesha maovu yote duniani?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 23:1-39.
Ijapokuwa Maandiko yanaonyesha kwamba huenda ikafaa kuwaita watu wenye mamlaka majina ya cheo, maneno ya Yesu katika Mathayo 23:8-11 yanaonyesha nini kuhusu matumizi ya majina ya cheo katika kutaniko la Kikristo? (Mdo. 26:25; Rom. 13:7; 1 Pet. 2:13, 14)
Mafarisayo walitumia nini ili kujaribu kuwazuia watu wasiwe Wakristo, na viongozi wa dini wametumiaje mbinu mbalimbali kama hizo siku hizi? (Mt. 23:13; Luka 11:52; Yoh. 9:22; 12:42; 1 The. 2:16)
Soma Mathayo 24:1-14.
Umuhimu wa uvumilivu umekaziwaje katika Mathayo 24:13?
Neno “mwisho” katika Mathayo 24:13 linamaanisha nini? (Mt. 16:27; Rom. 14:10-12; 2 Kor. 5:10)
Soma Marko 13:3-10.
Ni maneno yapi katika Marko 13:10 yanayoonyesha uharaka wa kuhubiri habari njema, na maneno hayo ya Yesu yanapaswa kutuchochea tufanye nini? (Rom. 13:11, 12; 1 Kor. 7:29-31; 2 Tim. 4:2)
Hadithi ya 99
Katika Chumba cha Juu
Kama picha inavyoonyesha, kwa nini Yesu na mitume wake 12 wako katika chumba kikubwa kwenye orofa ya juu?
Mtu anayeondoka ni nani, na anakwenda kufanya nini?
Yesu anaanzisha mlo upi baada ya kula chakula cha Kupitwa?
Sherehe ya Kupitwa iliwakumbusha Waisraeli kuhusu tukio gani, na mlo huu mpya wa pekee unawakumbusha wafuasi wa Yesu kuhusu nini?
Baada ya Mlo wa Jioni wa Bwana, Yesu anawaambia wafuasi wake nini, nao wanafanya nini?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 26:14-30.
Andiko la Mathayo 26:15 linaonyeshaje kwamba Yuda alimsaliti Yesu kimakusudi?
Yesu alimwaga damu yake kwa sababu gani mbili? (Mt. 26:27, 28; Yer. 31:31-33; Efe. 1:7; Ebr. 9:19, 20)
Soma Luka 22:1-39.
Shetani alimwingia Yuda katika maana gani? (Luka 22:3; Yoh. 13:2; Mdo. 1:24, 25)
Soma Yohana 13:1-20.
Tukifikiria andiko la Yohana 13:2, je, Yuda anapaswa kulaumiwa kwa matendo yake, na watumishi wa Mungu wanaweza kujifunza nini kutokana na jambo hilo? (Mwa. 4:7; 2 Kor. 2:11; Gal. 6:1; Yak. 1:13, 14)
Yesu alifundisha jambo gani muhimu kwa matendo? (Yoh. 13:15; Mt. 23:11; 1 Pet. 2:21)
Soma Yohana 17:1-26.
Yesu alisali kwamba wafuasi wake wawe “kitu kimoja” katika maana gani? (Yoh. 17:11, 21-23; Rom. 13:8; 14:19; Kol. 3:14)
Hadithi ya 100
Yesu Katika Bustani
Yesu na mitume wake wanakwenda wapi baada ya kutoka katika kile chumba kwenye orofa ya juu, naye anawaambia wafanye nini?
Yesu anapata mitume wakifanya nini anaporudi mahali alipowaacha, na jambo hilo linatukia mara ngapi?
Ni nani wanaoingia bustanini, na Yuda Iskariote anafanya nini, kama picha inavyoonyesha?
Kwa nini Yuda anambusu Yesu, na Petro anafanya nini?
Yesu anamwambia Petro nini, lakini kwa nini Yesu hamwombi Mungu awatume malaika?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 26:36-56.
Wazee Wakristo leo wanaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Yesu alivyowashauri wanafunzi wake? (Mt. 20:25-28; 26:40, 41; Gal. 5:17; Efe. 4:29, 31, 32)
Yesu alionaje matumizi ya silaha halisi ili kupigana na wanadamu wengine? (Mt. 26:52; Luka 6:27, 28; Yoh. 18:36)
Soma Luka 22:39-53.
Malaika alipotokea katika bustani ya Gethsemane ili kumwimarisha Yesu, je, jambo hilo lilionyesha kwamba Yesu alikosa imani? Eleza. (Luka 22:41-43; Isa. 49:8; Mt. 4:10, 11; Ebr. 5:7)
Soma Yohana 18:1-12.
Yesu aliwalindaje wanafunzi wake dhidi ya wapinzani wake, na tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wake? (Yoh. 10:11, 12; 18:1, 6-9; Ebr. 13:6; Yak. 2:25)
Hadithi ya 101
Yesu Anauawa
Ni nani hasa anayepaswa kulaumiwa kwa kifo cha Yesu?
Mitume wanafanya nini Yesu anapokamatwa na viongozi wa dini?
Ni jambo gani linalotukia katika nyumba ya kuhani mkuu Kayafa?
Kwa nini Petro alitoka nje na kulia?
Baada ya Yesu kurudishwa kwa Pilato, makuhani wakuu wanasema nini kwa sauti kubwa?
Yesu anafanywa nini mapema alasiri siku ya Ijumaa, naye anamwahidi nini mkosaji aliyetundikwa mtini kando yake?
Paradiso ambayo Yesu aliahidi itakuwa wapi?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 26:57-75.
Wanachama wa mahakama kuu ya Wayahudi walionyeshaje kwamba walikuwa waovu moyoni? (Mt. 26:59, 67, 68)
Soma Mathayo 27:1-50.
Kwa nini tunaweza kusema kwamba Yuda hakujuta moyoni kwa sababu ya kile alichokuwa amefanya? (Mt. 27:3, 4; Marko 3:29; 14:21; 2 Kor. 7:10, 11)
Soma Luka 22:54-71.
Tunaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Petro alivyomkana Yesu usiku aliposalitiwa na kukamatwa? (Luka 22:60-62; Mt. 26:31-35; 1 Kor. 10:12)
Soma Luka 23:1-49.
Yesu alifanya nini alipotendwa isivyo haki, na tunaweza kupata somo gani kutokana na hilo? (Luka 23:33, 34; Rom. 12:17-19; 1 Pet. 2:23)
Soma Yohana 18:12-40.
Ijapokuwa Petro alishtuka kwa muda mfupi kwa sababu ya kuwaogopa watu, baadaye akawa mtume aliyestahili sifa. Jambo hilo linaonyesha nini? (Yoh. 18:25-27; 1 Kor. 4:2; 1 Pet. 3:14, 15; 5:8, 9)
Soma Yohana 19:1-30.
Yesu alikuwa na maoni gani yanayofaa kuhusu vitu vya kimwili? (Yoh. 2:1, 2, 9, 10; 19:23, 24; Mt. 6:31, 32; 8:20)
Maneno ambayo Yesu alisema kabla tu ya kufa, yalionyeshaje kwamba alikuwa ameshinda kwa kuunga mkono enzi kuu ya Yehova hadi mwisho? (Yoh. 16:33; 19:30; 2 Pet. 3:14; 1 Yoh. 5:4)
Hadithi ya 102
Yesu Yuko Hai
Mwanamke unayemwona katika picha ni nani, wale wanaume wawili ni nani, na wako wapi?
Kwa nini makuhani wanamwambia Pilato awatume askari walinde kaburi la Yesu?
Malaika mmoja anafanya nini mapema siku ya tatu baada ya kifo cha Yesu, lakini makuhani wanafanya nini?
Kwa nini wanawake fulani wanashangaa wanapokwenda kwenye kaburi la Yesu?
Kwa nini Petro na Yohana wanakimbia hadi kwenye kaburi la Yesu, nao wanapata nini huko?
Mwili wa Yesu ulienda wapi, lakini Yesu anafanya nini ili awaonyeshe wanafunzi wake kwamba yu hai?
Maswali ya ziada:
Soma Mathayo 27:62-66 na 28:1-15.
Wakati wa ufufuo wa Yesu, makuhani wakuu, Mafarisayo, na wazee, walifanyaje dhambi dhidi ya roho takatifu? (Mt. 12:24, 31, 32; 28:11-15)
Soma Luka 24:1-12.
Masimulizi kuhusu ufufuo wa Yesu yanaonyeshaje kwamba Yehova anawaona wanawake kuwa mashahidi wanaoaminika? (Luka 24:4, 9, 10; Mt. 28:1-7)
Soma Yohana 20:1-12.
Andiko la Yohana 20:8, 9 linatusaidiaje kuona umuhimu wa kuwa na subira ikiwa hatuelewi kikamili unabii fulani wa Biblia? (Met. 4:18; Mt. 17:22, 23; Luka 24:5-8; Yoh. 16:12)
Hadithi ya 103
Ndani ya Chumba Kilichofungwa
Mariamu anamwambia nini mtu ambaye anafikiri ni mtunza bustani, lakini ni jambo gani linalomfanya atambue kwamba ndiye Yesu?
Ni jambo gani linalotukia wakati ambapo wanafunzi wawili wako njiani kwenda hadi kijiji cha Emau?
. Ni jambo gani la ajabu linalotukia wakati wanafunzi wawili wanapowaeleza mitume kwamba walimwona Yesu?
Yesu amejitokeza kwa wafuasi wake mara ngapi?
Tomaso anasema nini anaposikia kwamba wanafunzi wamemwona Bwana, lakini ni jambo gani linalotukia baada ya siku nane?
Maswali ya ziada:
Soma Yohana 20:11-29.
Je, maneno ya Yesu katika Yohana 20:23 yanamaanisha kwamba wanadamu wana uwezo wa kusamehe dhambi? Eleza. (Zab. 49:2, 7; Isa. 55:7; 1 Tim. 2:5, 6; 1 Yoh. 2:1, 2)
Soma Luka 24:13-43.
Tunawezaje kutayarisha moyo wetu ili ukubali kweli za Biblia kwa urahisi? (Luka 24:32, 33; Ezra 7:10; Mt. 5:3; Mdo. 16:14; Ebr. 5:11-14)
Hadithi ya 104
Yesu Anarudi Mbinguni
Ni wanafunzi wangapi wanaomwona Yesu katika pindi fulani, na anazungumzia habari gani pamoja nao?
Ufalme wa Mungu ni nini, na maisha yatakuwaje duniani Yesu atakapotawala akiwa Mfalme kwa miaka elfu?
Yesu amekuwa akijitokeza kwa wanafunzi wake kwa siku ngapi, lakini sasa umewadia wakati wake wa kufanya nini?
Kabla tu ya kuwaacha wanafunzi wake, Yesu anawaambia wafanye nini?
Ni jambo gani linalotukia katika picha, na Yesu anafichwa na nini wasimwone?
Maswali ya ziada:
Soma 1 Wakorintho 15:3-8.
Kwa nini Paulo aliweza kusema kwa uhakika sana kuhusu ufufuo wa Yesu, na Wakristo wanaweza kuhubiri kuhusu nini kwa uhakika? (1 Kor. 15:4, 7, 8; Isa. 2:2, 3; Mt. 24:14; 2 Tim. 3:1-5)
Soma Matendo 1:1-11.
Kazi ya kuhubiri ilienea hadi wapi, kama andiko la Matendo 1:8 linavyoonyesha? (Mdo. 6:7; 9:31; 11:19-21; Kol. 1:23)
Hadithi ya 105
Kungojea Yerusalemu
Kama picha inavyoonyesha, ni jambo gani linalowapata wafuasi wa Yesu ambao wamekuwa wakingoja Yerusalemu?
Kwa nini watu wa mataifa mengine wanaokuja Yerusalemu wanashangaa?
Petro anawaeleza watu nini?
Watu wanahisije baada ya kumsikiliza Petro, naye anawaambia wafanye nini?
Ni watu wangapi wanaobatizwa siku ya Pentekoste, mwaka wa 33 W.K.?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 2:1-47.
Maneno ya Petro katika Matendo 2:23, 36 yanaonyeshaje kwamba taifa zima la Wayahudi linalaumiwa kwa kifo cha Yesu? (1 The. 2:14, 15)
Petro aliwekaje mfano mzuri kwa kutoa sababu kwa kutumia Maandiko? (Mdo. 2:16, 17, 29, 31, 36, 39; Kol. 4:6)
Petro alitumiaje ufunguo wa kwanza kati ya “funguo za ufalme wa mbinguni,” ambazo Yesu alimwahidi atampa? (Mdo. 2:14, 22-24, 37, 38; Mt. 16:19)
Hadithi ya 106
Wanafunguliwa Katika Gereza
Ni jambo gani linalowapata Petro na Yohana alasiri moja wanapoingia hekaluni?
Petro anamwambia kilema fulani nini, na Petro anampa nini kilicho cha maana zaidi kuliko fedha?
Kwa nini viongozi wa dini wanakasirika, nao wanawatendaje Petro na Yohana?
Petro anawaambia viongozi wa dini nini, na mitume wanapewa onyo gani?
Kwa nini viongozi wa dini wanaona wivu, lakini ni jambo gani linalotukia wakati mitume wanapofungwa gerezani mara ya pili?
Mitume wanajibuje wanapopelekwa hadi jumba la Baraza Kuu?
Maswali ya ziada:
. Soma Matendo 3:1-10.
Ijapokuwa hatuna nguvu ya kufanya miujiza leo, maneno ya Petro katika Matendo 3:6 yanatusaidiaje kuelewa umuhimu wa ujumbe wa Ufalme? (Yoh. 17:3; 2 Kor. 5:18-20; Flp. 3:8)
Soma Matendo 4:1-31.
Tunapopingwa katika utumishi wetu, tunapaswa kuwaiga ndugu zetu Wakristo wa karne ya kwanza kwa njia gani? (Mdo. 4:29, 31; Efe. 6:18-20; 1 The. 2:2)
Soma Matendo 5:17-42.
Baadhi ya watu wasio Mashahidi, zamani na sasa, wamekuwa na maoni gani yanayofaa kuhusu kazi ya kuhubiri? (Mdo. 5:34-39)
Hadithi ya 107
Stefano Anapigwa kwa Mawe
Stefano ni nani, na Mungu amekuwa akimsaidia kufanya nini?
Stefano anasema nini kinachowakasirisha sana viongozi wa dini?
Baada ya kumburuta Stafano nje ya mji, wanaume hao wanamfanya nini?
Mwanamume kijana unayemwona karibu na nguo ni nani?
Kabla ya kufa, Stefano anamwomba Yehova nini?
Kwa kumwiga Stefano, tunapaswa kufanya nini mtu anapotukosea?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 6:8-15.
Viongozi wa dini wametumia mbinu gani za udanganyifu ili kujaribu kukomesha kazi ya kuhubiri ya Mashahidi wa Yehova? (Mdo. 6:9, 11, 13)
Soma Matendo 7:1-60.
Ni nini kilichomsaidia Stefano kutetea habari njema kwa matokeo mazuri mbele ya Baraza Kuu, na tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wake? (Mdo. 7:51-53; Rom. 15:4; 2 Tim. 3:14-17; 1 Pet. 3:15)
Tunapaswa kuwa na maoni gani kuwahusu wale wanaopinga kazi yetu? (Mdo. 7:58-60; Mt. 5:44; Luka 23:33, 34)
Hadithi ya 108
Wakienda Damasko
Sauli anafanya nini baada ya Stefano kuuawa?
Ni jambo gani la ajabu linalotukia wakati Sauli yuko njiani kwenda Damasko?
Yesu anamwambia Sauli afanye nini?
Yesu anampa Anania maagizo gani, na Sauli anarudishwaje uwezo wa kuona?
Sauli anakuja kujulikana kwa jina gani, naye anatumwa hasa kuwahubiria nani?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 8:1-4.
Mateso yaliyolikumba kutaniko jipya la Kikristo yalisaidiaje kueneza imani ya Kikristo, na jambo kama hilo limetukiaje siku hizi? (Mdo. 8:4; Isa. 54:17)
Soma Matendo 9:1-20.
Yesu alifunua kwamba alikuwa amekusudia kumpa Sauli ujumbe gani wenye sehemu tatu? (Mdo. 9:15; 13:5; 26:1; 27:24; Rom. 11:13)
Soma Matendo 22:6-16.
Tunawezaje kumwiga Anania, na kwa nini jambo hilo ni muhimu? (Mdo. 22:12; 1 Tim. 3:7; 1 Pet. 1:14-16; 2:12)
Soma Matendo 26:8-20.
Wale walio na wenzi wa ndoa wasioamini wanatiwaje moyo na jinsi Sauli alivyogeuka kuwa Mkristo? (Mdo. 26:11; 1 Tim. 1:14-16; 2 Tim. 4:2; 1 Pet. 3:1-3)
Hadithi ya 109
Petro Anamtembelea Kornelio
Ni nani anayeinama kwenye picha?
Malaika anamwambia Kornelio nini?
Mungu anamwonyesha Petro nini akiwa kwenye dari la nyumba ya Simoni huko Yopa?
Kwa nini Petro anamwambia Kornelio kwamba hapaswi kumwinamia na kumwabudu?
Kwa nini wanafunzi Wayahudi walio pamoja na Petro wanashangaa?
Tunapaswa kujifunza jambo gani muhimu kutokana na ziara ya Petro kwa Kornelio?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 10:1-48.
Maneno ya Petro katika Matendo 10:42 yanaonyesha nini kuhusu kazi ya kuhubiri habari njema ya Ufalme? (Mt. 28:19; Marko 13:10; Mdo. 1:8)
Soma Matendo 11:1-18.
Petro alionyesha mtazamo gani alipoelewa wazi mwongozo wa Yehova kuwahusu watu wa mataifa, na tunawezaje kumwiga? (Mdo. 11:17, 18; 2 Kor. 10:5; Efe. 5:17)
Hadithi ya 110
Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo
Kijana unayemwona katika picha ni nani, anaishi wapi, na mamake na nyanya yake wanaitwa nani?
Timotheo anasema nini Paulo anapomwuliza kama angetaka kujiunga na Sila na Paulo kuwahubiria watu katika maeneo ya mbali?
Wafuasi wa Yesu wanaitwa Wakristo kwa mara ya kwanza wapi?
Ni baadhi ya majiji gani ambayo Paulo, Sila, na Timotheo wanatembelea baada ya kutoka Listra?
Timotheo anamsaidiaje Paulo, na vijana wanapaswa kujiuliza maswali gani leo?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 9:19-30.
Mtume Paulo alionyeshaje busara alipokabili upinzani kwa sababu ya habari njema? (Mdo. 9:22-25, 29, 30; Mt. 10:16)
Soma Matendo 11:19-26.
Masimulizi ya Matendo 11:19-21, 26 yanaonyeshaje kwamba roho ya Yehova ndiyo inayoongoza na kuelekeza kazi ya kuhubiri?
Soma Matendo 13:13-16, 42-52.
Andiko la Matendo 13:51, 52 linaonyeshaje kwamba wanafunzi hawakuvunjika moyo kwa sababu ya upinzani? (Mt. 10:14; Mdo. 18:6; 1 Pet. 4:14)
Soma Matendo 14:1-6, 19-28.
Maneno ‘waliwakabidhi kwa Yehova’ yanatusaidiaje tusiwe na wasiwasi sana tunapoendelea kuwasaidia wapya? (Mdo. 14:21-23; 20:32; Yoh. 6:44)
Soma Matendo 16:1-5.
Utayari wa Timotheo wa kutahiriwa unakaziaje umuhimu wa ‘kufanya mambo yote kwa ajili ya habari njema’? (Mdo. 16:3; 1 Kor. 9:23; 1 The. 2:8)
Soma Matendo 18:1-11, 18-22.
Andiko la Matendo 18:9, 10 linaonyesha nini kuhusu jinsi Yesu mwenyewe anavyoongoza kazi ya kuhubiri, na jambo hilo linatuhakikishia nini leo? (Mt. 28:20)
Hadithi ya 111
Mvulana Aliyelala Usingizi
Ni nani mvulana anayelala chini katika picha, na ni jambo gani ambalo limetukia?
Paulo anafanya nini anapoona kwamba mvulana huyo amekufa?
Paulo, Timotheo, na wale wanaosafiri pamoja nao wanaelekea wapi, na ni nini kinachotukia wanapotua Mileto?
Nabii Agabo anamwonya Paulo juu ya nini, na jambo ambalo nabii huyo anatabiri linatukiaje?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 20:7-38.
Tunawezaje kubaki “safi kutokana na damu ya watu wote,” kulingana na maneno ya Paulo katika Matendo 20:26, 27? (Eze. 33:8; Mdo. 18:6, 7)
Kwa nini wazee wanapaswa ‘kulishika imara neno la uaminifu’ wanapofundisha? (Mdo. 20:17, 29, 30; Tito 1:7-9; 2 Tim. 1:13)
Soma Matendo 26:24-32.
Paulo alitumiaje uraia wake wa milki ya Roma ili kutimiza kazi ya kuhubiri aliyopewa na Yesu? (Mdo. 9:15; 16:37, 38; 25:11, 12; 26:32; Luka 21:12, 13)
Hadithi ya 112
Meli Inaharibika Katika Kisiwa
Inakuwaje na meli ambayo Paulo anasafiri nayo inapopita karibu na kisiwa cha Krete?
Paulo anawaambia wale walio melini nini?
Kwa nini meli inavunjika-vunjika?
Mkuu wa jeshi anatoa maagizo gani, na watu wangapi wanafika kisiwani salama?
Kisiwa hicho kinaitwaje, na ni jambo gani linalompata Paulo hali ya hewa inapokuwa nzuri?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 27:1-44.
Tunasaidikishwaje kwamba masimulizi ya Biblia ni sahihi tunaposoma kuhusu safari ya Paulo ya kwenda Roma? (Mdo. 27:16-19, 27-32; Luka 1:3; 2 Tim. 3:16, 17)
Soma Matendo 28:1-14.
Ikiwa watu wapagani wa Malta walisukumwa na mioyo yao kuwatendea Paulo na wenzake waliovunjikiwa meli kwa “fadhili za kibinadamu zisizo za kawaida,” Wakristo wanapaswa kusukumwa kuonyesha nini na hasa kwa njia gani? (Mdo. 28:1, 2; Ebr. 13:1, 2; 1 Pet. 4:9)
Hadithi ya 113
Paulo Katika Roma
Paulo anamhubiria nani akiwa kifungoni Roma?
Kama unavyoona katika picha, ni nani mgeni ambaye ameketi mezani, na anamsaidia Paulo kufanya nini?
Epafrodito ni nani, naye anaporudi Filipi anapeleka nini huko?
Kwa nini Paulo anamwandikia rafiki yake mkubwa Filemoni barua?
Paulo anafanya nini anapoachiliwa, na ni jambo gani linalompata baadaye?
Yehova anamwongoza nani kuandika vitabu vya mwisho vya Biblia, na kitabu cha Ufunuo kinaeleza juu ya mambo gani?
Maswali ya ziada:
Soma Matendo 28:16-31 na Wafilipi 1:13.
Paulo alifanya nini alipokuwa gerezani Roma, na kutaniko la Kikristo lilitiwaje moyo kwa imani yake yenye nguvu? (Mdo. 28:23, 30; Flp. 1:14)
Soma Wafilipi 2:19-30.
Paulo alisema nini kuonyesha kwamba alimthamini Timotheo na Epafrodito, na tunawezaje kuiga mfano wa Paulo? (Flp. 2:20, 22, 25, 29, 30; 1 Kor. 16:18; 1 The. 5:12, 13)
Soma Filemoni 1-25.
Paulo alimhimiza Filemoni kufanya yaliyo mema kwa msingi gani, na jambo hilo linatoa mwongozo gani kwa wazee leo? (Flm. 9; 2 Kor. 8:8; Gal. 5:13)
Maneno ya Paulo katika Filemoni 13, 14 yanaonyeshaje kwamba aliheshimu dhamiri za wengine kutanikoni? (1 Kor. 8:7, 13; 10:31-33)
Soma 2 Timotheo 4:7-9.
Kama Paulo, tunawezaje kuwa na hakika kwamba Yehova atatupa thawabu tukiendelea kuwa waaminifu hadi mwisho? (Mt. 24:13; Ebr. 6:10)
Hadithi ya 114
Mwisho wa Mabaya Yote
Kwa nini Biblia inazungumzia farasi mbinguni?
Vita vya Mungu dhidi ya watu wote wabaya duniani inaitwaje, na kusudi la vita hiyo ni nini?
Yule atakayeongoza vita ni nani kama picha inavyoonyesha, kwa nini amevalia taji, na upanga wake unamaanisha nini?
Kwa kufikiria Hadithi ya 10, 15, na 33, kwa nini hatupaswi kushangaa kujua kwamba Mungu atawaangamiza watu waovu?
Hadithi ya 36 na 76 zinatuonyeshaje kwamba Mungu atawaangamiza watu waovu hata kama wanasema kwamba wanamwabudu?
Maswali ya ziada:
Soma Ufunuo 19:11-16.
Maandiko yanaonyeshaje kwamba Yesu Kristo ndiye anayepanda farasi mweupe? (Ufu. 1:5; 3:14; 19:11; Isa. 11:4)
Damu ambayo imenyunyizwa kwenye vazi la nje la Yesu inahakikishaje kwamba ushindi wake ni hakika na kamili kabisa? (Ufu. 14:18-20; 19:13)
Yaelekea majeshi yanayomfuata Yesu akiwa amepanda farasi wake mweupe wanatia ndani akina nani? (Ufu. 12:7; 19:14; Mt. 25:31, 32)
Hadithi ya 115
Paradiso Mpya Duniani
Biblia inaonyesha kwamba tutafurahia hali gani katika Paradiso duniani?
Biblia inawaahidi wale watakaoishi katika Paradiso nini?
Yesu ataleta mabadiliko hayo mazuri lini?
Yesu alipokuwa duniani, alifanya nini kuonyesha kile ambacho atafanya atakapokuwa Mfalme katika Ufalme wa Mungu?
Yesu na watawala wenzake wa mbinguni watahakikisha nini watakapotawala dunia wakiwa mbinguni?
Maswali ya ziada:
Soma Ufunuo 5:9, 10.
Kwa nini tunaweza kuwa na hakika kwamba wale watakaotawala dunia kwa miaka elfu watakuwa wafalme na makuhani wenye kujali na wenye huruma? (Efe. 4:20-24; 1 Pet. 1:7; 3:8; 5:6-10)
Soma Ufunuo 14:1-3.
Kuandikwa kwa jina la Baba na jina la Mwana-Kondoo kwenye vipaji vya wale 144,000 kunaonyesha nini? (1 Kor. 3:23; 2 Tim. 2:19; Ufu. 3:12)
Hadithi ya 116
Tunavyoweza Kuishi Milele
Tunahitaji kujua nini tukitaka kuishi milele?
Tunawezaje kujifunza kumhusu Yehova Mungu na Yesu, kama msichana huyu mdogo na rafiki zake katika picha wanavyofanya?
Unakiona kitabu kingine gani katika picha, na kwa nini tunapaswa kukisoma kwa ukawaida?
Mbali na kujifunza kumhusu Yehova na Yesu, tunahitaji kufanya nini kingine ili tupate uzima wa milele?
Tunajifunza nini katika Hadithi ya 69?
Mfano mzuri wa mvulana mdogo Samweli katika Hadithi ya 55 unaonyesha nini?
Tunawezaje kufuata mfano wa Yesu Kristo, na tukiufuata, tutaweza kufanya nini wakati ujao?
Maswali ya ziada:
Soma Yohana 17:3.
Maandiko yanaonyeshaje kwamba kupata ujuzi kumhusu Yehova Mungu na Yesu Kristo hakumaanishi tu kusoma na kukumbuka habari kuwahusu? (Mt. 7:21; Yak. 2:18-20; 1 Yoh. 2:17)
Soma Zaburi 145:1-21.
Baadhi ya sababu za kumsifu Yehova ni zipi? (Zab. 145:8-11; Ufu. 4:11)
Yehova ni “mwema kwa wote” kwa njia gani, na kwa nini jambo hilo linapaswa kutuvutia tumkaribie zaidi na zaidi? (Zab. 145:9; Mt. 5:43-45)
Ikiwa tunampenda Yehova moyoni mwetu, tutasukumwa kufanya nini? (Zab. 119:171, 172, 175; 145:11, 12, 21)