Ufunuo
15 Nami nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya ajabu sana, malaika saba wenye tauni saba. Hizi ndizo za mwisho, kwa sababu kwa hizo hasira ya Mungu yaletwa kwenye tamati.
2 Nami nikaona kilichoonekana kuwa bahari iliyo kama kioo iliyochangamana na moto, na wale watokeao wakiwa washindi kutoka kwa hayawani-mwitu na kutoka kwa sanamu yake na kutoka kwa nambari ya jina lake wakiwa wamesimama kando ya bahari iliyo kama kioo, wakiwa na vinubi vya Mungu. 3 Nao wanaimba wimbo wa Musa mtumwa wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema:
“Ni kubwa na za ajabu sana kazi zako, Yehova Mungu, Mweza-Yote. Ni za uadilifu na za kweli njia zako, Mfalme wa umilele. 4 Ni nani ambaye kwa kweli hatakuhofu wewe, Yehova, na kulitukuza jina lako, kwa sababu wewe peke yako ni mwaminifu-mshikamanifu? Kwa maana mataifa yote yatakuja na kuabudu mbele yako, kwa sababu maagizo yako ya uadilifu yamefanywa kuwa dhahiri.”
5 Na baada ya mambo haya nikaona, na patakatifu pa hema ya ushahidi pakafunguliwa mbinguni, 6 na malaika saba wenye tauni saba wakaibuka kutoka katika patakatifu, wamevishwa kitani safi, nyangavu na wamefungwa mishipi ya dhahabu kuzunguka vifua vyao. 7 Na mmoja kati ya wale viumbe hai wanne akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa hasira ya Mungu, aliye hai milele na milele. 8 Na patakatifu pakawa penye kujawa na moshi kwa sababu ya utukufu wa Mungu na kwa sababu ya nguvu yake, na hakuna yeyote aliyeweza kuingia katika patakatifu mpaka tauni saba za hao malaika saba zilipomalizika.