Mika
Wanampiga mwamuzi wa Israeli shavuni kwa fimbo.+
2 Na wewe, Ee Bethlehemu Efratha,+
Uliye mdogo sana usiweze kuwa miongoni mwa maelfu ya* Yuda,+
Kutoka kwako atatoka kwa ajili yangu yule atakayekuwa mtawala katika Israeli,
Ambaye asili yake ni ya tangu nyakati za kale, tangu siku za zamani za kale.
3 Kwa hiyo atawaacha
Mpaka wakati ambapo mwanamke anayepaswa kuzaa atakapozaa.
Na wale ndugu zake wengine watarudi kwa watu wa Israeli.
Mwashuru akiivamia nchi yetu na kukanyaga-kanyaga minara yetu yenye ngome,+
Tutawainua wachungaji saba dhidi yake, naam, wakuu* wanane wanadamu.
Naye atatuokoa kutoka kwa Mwashuru,+
Anapoivamia nchi yetu na kulikanyaga-kanyaga eneo letu.
7 Waliobaki wa Yakobo watakuwa miongoni mwa mataifa mengi
Kama umande kutoka kwa Yehova,
Kama manyunyu ya mvua juu ya mimea
Ambayo hayamtumaini mwanadamu
Wala kuwangojea wana wa wanadamu.
8 Waliobaki wa Yakobo watakuwa miongoni mwa mataifa,
Miongoni mwa mataifa mengi,
Kama simba miongoni mwa wanyama wa mwituni,
Kama mwanasimba* miongoni mwa makundi ya kondoo,
Ambaye hupita na kurukia na kurarua vipandevipande;
Wala hakuna yeyote wa kuwaokoa.
9 Mkono wako utainuliwa juu ya maadui wako,
Na maadui wako wote wataangamizwa.”
10 “Siku hiyo,” asema Yehova,
“Nitawaangamiza kabisa farasi wako na kuharibu magari yako ya vita.
11 Nitaharibu majiji yaliyo katika nchi yako
Na kubomoa ngome zako zote.
15 Kwa hasira na ghadhabu nitalipiza kisasi
Dhidi ya mataifa ambayo hayajatii.”