Sura 83
Akirimiwa na Farisayo Mashuhuri
YESU angali yumo nyumbani mwa Farisayo mmoja mashuhuri na ndipo tu ameponya mwanamume mmoja anayetaabishwa na ugonjwa wa istiska. Anapoona wageni wenzake wakichagua mahali pa umashuhuri kwenye mlo, yeye anafundisha somo la unyenyekevu.
“Wakati wewe unapoalikwa na mtu fulani kwenye karamu ya arusi,” ndipo Yesu anapoeleza, “usikae katika mahali penye umashuhuri zaidi ya pote. Pengine mtu fulani mashuhuri zaidi yako huenda akawa wakati huo amealikwa naye, naye aliyekualika wewe na yeye atakuja na kusema kwako, ‘Acha mtu huyu akae mahali hapo.’ Ndipo wewe utaondoka kwa aibu ukachukue mahali pa chini zaidi ya pote.”
Kwa hiyo Yesu anatoa shauri hili: “Wakati wewe unapoalikwa, nenda na kukaa katika mahali pa chini zaidi ya pengine pote, ili wakati yule mtu aliyekualika anapokuja yeye atasema kwako wewe, ‘Rafiki, enda mbele penye heshima zaidi.’ Ndipo wewe utapata heshima machoni pa wageni wenzako wote.” Akimalizia, Yesu anasema: “Kwa kuwa kila mtu ajikwezaye mwenyewe atanyenyekezwa na yeye ambaye hujinyenyekeza atakwezwa.”
Halafu, Yesu anaelekeza maneno kwa yule Farisayo aliyemwalika na kueleza jinsi ya kuandaa mlo mkuu wenye ustahili kwa Mungu. “Wakati unapofanya mlo mkuu au mlo wa jioni, usiite marafiki wako au ndugu zako au watu wa ukoo wako au majirani wenye utajiri. Pengine wakati fulani wao huenda nao wakakualika na ingekuwa ni lipo kwako. Bali wakati wewe uandaapo karamu, alika watu maskini, viwete, walemavu, vipofu; nawe utakuwa mwenye furaha, kwa sababu wao hawana chochote cha kukulipa nacho.”
Kuandaa mlo wa jinsi hiyo kwa ajili ya wasiofanikwa sana kutamletea furaha mwenye kuwaandalia kwa sababu, kama vile Yesu anavyoeleza mkaribishaji wake, “Wewe utalipwa katika ufufuo wa waadilifu.” Elezo la Yesu la mlo huu wenye ustahili wamkumbusha mgeni mwenzake mlo wa aina nyingine. “Mwenye furaha ni yeye alaye mkate katika ufalme wa Mungu,” asema mgeni huyo. Walakini, si wote wanaothamini ifaavyo tazamio hilo lenye furaha, kama Yesu aendeleavyo kuonyesha kwa kielezi kimoja.
“Mwanamume fulani alikuwa akiandaa mlo wa jioni mkubwa, naye akaalika wengi. Naye akatuma mtumwa wake nje . . . akaseme kwa walioalikwa, ‘Njooni, kwa sababu sasa vitu viko tayari.’ Lakini wote kwa ujumla wakaanza kutoa udhuru. Yule wa kwanza akamwambia, ‘Mimi nilinunua shamba na ninahitaji kwenda nikalitazame; nakuomba, Ukaniombee radhi.’ Na mwingine akasema, ‘Mimi nilinunua jozi tano za ng’ombe wa [kufungwa] nira nami naenda kuwachunguza; nakuomba, Ukaniombee radhi.’ Bado mwingine akasema, ‘Mimi ndipo tu nimeoa mke na kwa sababu hiyo siwezi kuja.’”
Ni udhuru usiofaa kama nini! Shamba au mifugo huchunguzwa kwa kawaida kabla ya kununuliwa, hivyo hakuna uharaka halisi uliopo wa kuwaangalia baadaye. Vivyo hivyo, ndoa ya mtu haipasi kumzuia asikubali mwaliko wa maana kama huo. Kwa hiyo anaposikia juu ya udhuru huo, bwana-mkubwa anakasirika na kumwamuru hivi mtumwa wake:
“‘Toka uende nje upesi katika barabara kuu na vijia vya jijini, na kuleta ndani hapa walio maskini na vilema na vipofu na walemavu.’ Baada ya wakati mtumwa yule akasema, ‘Bwana-mkubwa, uliloamuru limefanywa, na bado kuna nafasi.’ Naye bwana-mkubwa akasema kwa yule mtumwa, ‘Toka uende nje barabarani na mahali palipozungushiwa ua, na kuwashurutisha waje ndani, kwamba nyumba yangu ipate kujaa. . . . Hakuna yeyote wa wanaume hao walioalikwa ataonja mlo wa jioni wangu.’”
Ni hali gani inayoelezwa na kielezi hicho? Basi, “bwana-mkubwa” mwenye kuandaa mlo ule anawakilisha Yehova Mungu; “mtumwa” mwenye kutoa mwaliko, Yesu Kristo; na ule “mlo wa jioni mkubwa,” fursa za kuwa katika mstari wa kupata Ufalme wa mbingu.
Zaidi ya watu wengine wote, wale waliokuwa wa kwanza kupokea mwaliko wa kuja katika mstari wa kupata Ufalme walikuwa viongozi wa kidini Wayahudi wa siku ya Yesu. Hata hivyo, wao walikataa mwaliko huo. Hivyo, kuanzia hasa Pentekoste 33 W.K., mwaliko wa pili ulitolewa kwa watu wenye kudharauliwa na walio dhalili wa taifa la Kiyahudi. Lakini walioitikia kujaza zile nafasi 144,000 katika Ufalme wa kimbingu wa Mungu hawakutosha. Kwa hiyo katika 36 W.K., miaka mitatu na nusu baadaye, mwaliko wa tatu na wa mwisho ulitolewa kwa watu wasiotahiriwa wasio Wayahudi, na kukusanywa kwao kumeendelea mpaka kuingia katika siku yetu. Luka 14:1-24, NW.
▪ Yesu anafundisha somo gani la unyenyekevu?
▪ Mkaribishaji anaweza kuandaaje mlo wenye ustahili kwa Mungu, na kwa nini hiyo itamletea furaha?
▪ Kwa nini udhuru wa wageni walioalikwa haufai?
▪ Ni nini kinachowakilishwa na kielezi cha Yesu cha ule “mlo wa jioni mkubwa”?