Mathayo
4 Ndipo Yesu akaongozwa na roho kuingia nyikani ili kushawishwa na Ibilisi. 2 Baada ya yeye kuwa amefunga siku arobaini mchana na usiku, ndipo akahisi njaa. 3 Pia, Mshawishi akaja na kumwambia: “Ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, yaambie mawe haya yawe mikate.” 4 Lakini kwa kujibu yeye akasema: “Imeandikwa, ‘Binadamu lazima aishi, si kwa mkate pekee, bali kwa kila tamko linalokuja kupitia kinywa cha Yehova.’”
5 Ndipo Ibilisi akamchukua kwenda pamoja naye kuingia lile jiji takatifu, naye akamsimamisha juu ya buruji ya hekalu 6 na kumwambia: “Ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, jivurumishe chini; kwa maana imeandikwa, ‘Yeye atawapa malaika zake agizo kukuhusu wewe, nao watakuchukua mikononi mwao, ili usipate kupiga mguu wako dhidi ya jiwe wakati wowote.’” 7 Yesu akamwambia: “Tena imeandikwa, ‘Lazima usimtie Yehova Mungu wako kwenye jaribu.’”
8 Tena Ibilisi akamchukua kwenda pamoja naye kwenye mlima ulioinuka juu isivyo kawaida, na kumwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wazo, 9 naye akamwambia: “Hakika nitakupa mambo yote haya ukianguka chini na kunifanyia tendo la ibada.” 10 Ndipo Yesu akamwambia: “Enda zako, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Ni Yehova Mungu wako ambaye lazima uabudu, na ni kwake peke yake lazima utoe utumishi mtakatifu.’” 11 Ndipo Ibilisi akamwacha, na, tazama! malaika wakaja na kuanza kumhudumia.
12 Sasa aliposikia kwamba Yohana alikuwa amekamatwa, aliondoka akaingia Galilaya. 13 Zaidi, baada ya kuondoka Nazareti, alikuja na kufanya makao katika Kapernaumu kando ya bahari katika wilaya za Zebuloni na Naftali, 14 ili kupate kutimizwa lile lililosemwa kupitia Isaya nabii, akisema: 15 “Ewe nchi ya Zebuloni na nchi ya Naftali, kando ya barabara ya bahari, katika upande ule mwingine wa Yordani, Galilaya ya mataifa! 16 watu wenye kuketi katika giza waliona nuru kubwa, na kwa habari ya wale wenye kuketi katika mkoa wa kivuli cha kifo, nuru iliwazukia.” 17 Kutoka wakati huo na kuendelea Yesu alianza kuhubiri na kusema: “Tubuni, nyinyi watu, kwa maana ufalme wa mbingu umekaribia.”
18 Alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro na Andrea ndugu yake, wakishusha wavu wa kuvulia samaki ndani ya bahari, kwa maana walikuwa wavuvi. 19 Naye akawaambia: “Njoni mnifuate mimi, nami hakika nitawafanya nyinyi kuwa wavuvi wa watu.” 20 Mara moja wakiziacha nyavu, wakamfuata. 21 Akiendelea mbele pia kutoka hapo akaona wengine wawili waliokuwa ndugu, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake, katika mashua pamoja na Zebedayo baba yao, wakitengeneza nyavu zao, naye akawaita. 22 Mara moja wakiacha ile mashua na baba yao wakamfuata.
23 Ndipo akaenda akizunguka kotekote katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao na kuhubiri habari njema ya ufalme na kuponya kila namna ya maradhi na kila namna ya udhaifu miongoni mwa watu. 24 Na ripoti juu yake ikatoka kwenda katika Siria yote; nao wakamletea wote wale wenye hali mbaya, wenye kutaabishwa na maradhi na kuteswa-teswa kwa namna mbalimbali, wenye kupagawa na roho waovu na wenye kifafa na watu waliopooza, naye akawaponya. 25 Kwa sababu hiyo umati mkubwa ukamfuata kutoka Galilaya na Dekapolisi na Yerusalemu na Yudea na kutoka upande ule mwingine wa Yordani.