Mathayo
10 Kwa hiyo akawaita wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapa mamlaka juu ya roho wasio safi, kusudi wawafukuze na kuponya kila namna ya maradhi na kila namna ya udhaifu.
2 Majina ya wale mitume kumi na wawili ni haya: Kwanza, Simoni, aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake; na Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; 3 Filipo na Bartholomayo; Tomasi na Mathayo mkusanya-kodi; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkananayo, na Yudasi Iskariote, ambaye baadaye alimsaliti.
5 Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma, akiwapa maagizo haya: “Msiende zenu katika barabara ya mataifa, na msiingie katika jiji la Wasamaria; 6 bali, badala ya hivyo, nendeni kwa kuendelea kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7 Mwendapo, hubirini, mkisema, ‘Ufalme wa mbingu umekaribia.’ 8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, fanyeni wenye ukoma wawe safi, fukuzeni roho waovu. Mlipokea bure, toeni bure. 9 Msijipatie dhahabu wala fedha wala shaba kwa ajili ya vifuko vyenu vya mshipini, 10 wala mfuko wa chakula kwa ajili ya safari, wala mavazi ya ndani mawili, wala makubazi wala fimbo; kwa maana mfanyakazi astahili chakula chake.
11 “Katika jiji lolote lile au kijiji chochote kile mwingiamo, tafuteni kabisa ni nani humo anayestahili, na mkae humo mpaka mwondokapo. 12 Mnapokuwa mkiingia ndani ya hiyo nyumba, salimuni hao watu wa nyumbani; 13 na ikiwa hiyo nyumba inastahili, acheni amani mwitakiayo ije juu yayo; lakini ikiwa haistahili, acheni amani itokayo kwenu irudi juu yenu. 14 Popote pale ambapo yeyote hawakaribishi nyinyi au hasikilizi maneno yenu, mnapoenda kutoka katika nyumba hiyo au jiji hilo yakung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu. 15 Kwa kweli mimi nawaambia nyinyi, Litakuwa jambo lenye kuvumilika zaidi kwa nchi ya Sodoma na Gomora Siku ya Hukumu kuliko kwa jiji hilo.
16 “Tazama! Mimi ninawatuma nyinyi kama kondoo katikati ya mbwa-mwitu; kwa hiyo jithibitisheni wenyewe kuwa wenye hadhari kama nyoka na bado kuwa wasio na hatia kama njiwa. 17 Jilindeni dhidi ya watu; kwa maana watawakabidhi nyinyi kwenye mahakama za mtaa, nao watawapiga nyinyi mijeledi katika masinagogi yao. 18 Naam, mtaburutwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushahidi kwao na kwa mataifa. 19 Hata hivyo, wakati wawakabidhipo nyinyi, msiwe wenye kuhangaikia jinsi gani au jambo gani mtakalosema; kwa maana lile mtakalosema litapewa kwenu katika saa hiyo; 20 kwa maana wanaosema si nyinyi tu, bali ni roho ya Baba yenu isemayo kupitia nyinyi. 21 Zaidi, ndugu atakabidhi ndugu kwenye kifo, na baba mtoto wake, na watoto watainuka dhidi ya wazazi na kufanya wauawe. 22 Nanyi mtakuwa vitu vya kuchukiwa na watu wote kwa sababu ya jina langu; lakini yeye ambaye amevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokolewa. 23 Wakati wawanyanyasapo nyinyi katika jiji moja, kimbilieni jingine; kwa maana kwa kweli nawaambia nyinyi, hamtakamilisha kwa vyovyote mzunguko wa majiji ya Israeli mpaka Mwana wa binadamu awasili.
24 “Mwanafunzi hayuko juu ya mwalimu wake, wala mtumwa juu ya bwana wake. 25 Yatosha kwa mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kama bwana wake. Ikiwa watu wamemwita mwenye nyumba Beelzebubi, je, si zaidi sana watawaita hivyo wale watu wa nyumbani mwake? 26 Kwa hiyo msiwahofu; kwa maana hakuna kitu chochote kilichofunikwa kabisa ambacho hakitakuwa chenye kufunuliwa, na cha siri ambacho hakitakuwa chenye kujulikana. 27 Lile niwaambialo nyinyi katika giza, lisemeni katika nuru; na lile msikialo lanong’onwa, lihubirini kutoka paa za nyumba. 28 Na msiwe wenye kuwahofu wale wauuao mwili lakini hawawezi kuiua nafsi; lakini badala ya hivyo mhofuni yeye awezaye kuangamiza vyote viwili nafsi na mwili katika Gehena. 29 Je, shore wawili hawauzwi kwa sarafu ya thamani ndogo? Na bado hakuna hata mmoja wao atakayeanguka kwenye ardhi bila Baba yenu kujua. 30 Lakini nywele zenyewe za kichwa chenu zimehesabiwa zote. 31 Kwa hiyo msiwe na hofu: Nyinyi ni bora zaidi kuliko shore wengi.
32 “Basi, kila mtu aungamaye muungano pamoja nami mbele ya wanadamu, mimi pia hakika nitaungama muungano pamoja naye mbele ya Baba yangu aliye katika mbingu; 33 lakini yeyote yule anikanaye mimi mbele ya watu, hakika mimi pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye katika mbingu. 34 Msifikiri nilikuja kuweka amani juu ya dunia; nilikuja kuweka, si amani, bali upanga. 35 Kwa maana nilikuja kusababisha mgawanyiko, na mtu dhidi ya baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mke kijana dhidi ya mama-mkwe wake. 36 Kwa kweli, maadui wa mtu watakuwa watu wa nyumbani mwake mwenyewe. 37 Yeye aliye na shauku kubwa zaidi kwa baba au mama kuliko kwangu hanistahili mimi; na yeye aliye na shauku kubwa zaidi kwa mwana au binti kuliko kwangu hanistahili mimi. 38 Na yeyote yule asiyechukua mti wake wa mateso na kunifuata hanistahili mimi. 39 Yeye apataye nafsi yake ataipoteza, naye apotezaye nafsi yake kwa ajili yangu ataipata.
40 “Yeye awapokeaye nyinyi hunipokea mimi pia, naye anipokeaye mimi humpokea yeye pia aliyenituma. 41 Yeye apokeaye nabii kwa sababu ni nabii atapata thawabu ya nabii, naye apokeaye mtu mwadilifu kwa sababu ni mtu mwadilifu atapata thawabu ya mtu mwadilifu. 42 Na yeyote yule ampaye mmoja wa wadogo hawa kikombe tu cha maji baridi ya kunywa kwa sababu ni mwanafunzi, nawaambia nyinyi kwa kweli, huyo hatapoteza thawabu yake kwa vyovyote.”