Wafilipi
2 Basi, ikiwa kuna kitia-moyo chochote katika Kristo, kukiwa na faraja yoyote ya upendo, kukiwa na kushiriki kokote kwa roho, kukiwa na shauku nyororo na huruma zozote, 2 fanyeni shangwe yangu ijae kwa kuwa nyinyi ni wenye akili ileile na wenye upendo uleule, mkiunganishwa pamoja katika nafsi, mkishika fikira moja akilini, 3 bila kufanya jambo lolote kwa ugomvi au kwa majisifu ya bure, bali kwa hali ya akili ya kujishusha chini mkifikiria kwamba wengine ni wakubwa kuliko nyinyi, 4 mkifuliza kuangalia, si masilahi ya kibinafsi ya mambo yenu wenyewe tu, bali pia masilahi ya kibinafsi yale ya wengine.
5 Tunzeni mtazamo huu wa akili ndani yenu uliokuwa pia ndani ya Kristo Yesu, 6 ambaye, ijapokuwa alikuwa akiwako katika umbo la Mungu, hakufikiria upokonyaji, yaani, kwamba yeye awe sawa na Mungu. 7 La, bali alijifanya mwenyewe kuwa mtupu na kuchukua umbo la mtumwa na kuja kuwa katika ufanani wa wanadamu. 8 Zaidi ya hilo, alipojipata mwenyewe katika sura ya kuwa binadamu alijinyenyekeza mwenyewe akawa mtiifu hadi kifo, ndiyo, kifo juu ya mti wa mateso. 9 Kwa sababu hiihii pia Mungu alimkweza kwenye cheo cha juu zaidi akampa kwa fadhili jina lililo juu ya kila jina jingine, 10 ili katika jina la Yesu kila goti likunjwe la wale walio mbinguni na wale walio duniani na wale walio chini ya ardhi, 11 na kila ulimi ukiri waziwazi kwamba Yesu Kristo ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba.
12 Kwa sababu hiyo, wapendwa wangu, kwa jinsi ambavyo mmetii sikuzote, si wakati wa kuwapo kwangu tu, bali kwa utayari zaidi sasa wakati wa kutokuwapo kwangu, fulizeni kufanyiza wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka; 13 kwa maana Mungu ndiye ambaye, kwa ajili ya upendezi wake mwema, anatenda ndani yenu ili nyinyi mwe na nia na kutenda pia. 14 Fulizeni kufanya mambo yote bila manung’uniko na mabishano, 15 ili mpate kuja kuwa bila lawama na wasio na hatia, watoto wa Mungu wasio na waa miongoni mwa kizazi kilicho kombo na kilichopotoka, ambao miongoni mwao mnang’aa mkiwa wamulikaji katika ulimwengu, 16 mkifuliza kushika kwa mkazo neno la uhai, ili kwamba nipate kuwa na sababu ya mchachawo katika siku ya Kristo, kwamba sikukimbia bure wala kufanya kazi kwa bidii bure. 17 Ingawaje, hata ikiwa ninamwagwa kama toleo la kinywaji juu ya dhabihu na utumishi wa watu wote ambako imani imewaongoza nyinyi, mimi naterema nami nashangilia pamoja nanyi nyote. 18 Basi katika njia hiyohiyo nyinyi wenyewe teremeni pia na kushangilia pamoja nami.
19 Kwa upande wangu ninatumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu upesi, ili nipate kuwa nafsi changamfu nipatapo kujua juu ya mambo yanayohusiana nanyi. 20 Kwa maana sina mwingine yeyote mwenye mwelekeo kama wake atakayejali kihalisi mambo yanayohusiana nanyi. 21 Kwa maana wale wengine wote wanatafuta sana masilahi yao wenyewe, si yale ya Kristo Yesu. 22 Lakini nyinyi mwaijua ithibati aliyoitoa juu yake mwenyewe, kwamba kama vile mtoto na baba yeye alitumikia kama mtumwa pamoja nami katika kuendeleza habari njema. 23 Basi, huyu ndiye mtu ninayetumaini kumtuma mara tu nikiisha kuona jinsi mambo yalivyo kuhusu mimi. 24 Kwa kweli, nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe pia nitakuja upesi.
25 Hata hivyo, nafikiria ni lazima nimtume kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mfanyakazi mwenzi na askari-jeshi mwenzi, lakini mjumbe wenu na mtumishi wa faragha kwa uhitaji wangu, 26 kwa kuwa ana hamu sana kuwaona nyinyi nyote na ameshuka moyo kwa sababu mlisikia alikuwa amekuwa mgonjwa. 27 Ndiyo, kwa kweli, alipata kuwa mgonjwa karibu kiasi cha kufa; lakini Mungu alikuwa na rehema juu yake, kwa kweli, si juu yake tu, bali pia juu yangu, ili nisipate kihoro juu ya kihoro. 28 Kwa hiyo kwa hima kubwa zaidi ninamtuma, ili mmwonapo mpate kushangilia tena nami nipate kuwa bila kihoro hata zaidi. 29 Kwa hiyo mpeni karibisho la kidesturi katika Bwana kwa shangwe yote; na fulizeni kuwachukua watu wa namna hiyo kuwa wenye thamani kubwa, 30 kwa sababu kwa ajili ya kazi ya Bwana alikaribia sana kifo, akihatarisha nafsi yake, ili apate kujazia kikamili kutokuwapo kwenu hapa ili kutoa utumishi wa faragha kwangu.