1 Wathesalonike
5 Sasa kwa habari ya nyakati na majira, akina ndugu, hamhitaji kuandikiwa kitu. 2 Kwa maana nyinyi wenyewe mwajua vema kabisa kwamba siku ya Yehova inakuja sawasawa kabisa na mwizi usiku. 3 Wakati wowote ule ambao wanasema: “Amani na usalama!” ndipo uharibifu wa ghafula utakapokuwa hapohapo juu yao kama vile maumivu makali ya ghafula ya taabu juu ya mwanamke mwenye mimba; nao hawataponyoka kwa vyovyote. 4 Lakini nyinyi, akina ndugu, hamumo katika giza, hivi kwamba siku hiyo iwafikie nyinyi ghafula kama vile ingekuwa kwa wezi, 5 kwa maana nyinyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wa usiku wala wa giza.
6 Kwa hiyo, basi, acheni tusiendelee kulala usingizi kama wengine, bali acheni tukae macho na kutunza hisi zetu. 7 Kwa maana wale walalao usingizi wana desturi ya kulala usingizi usiku, na kwa kawaida wale walewao hulewa usiku. 8 Lakini kwa habari yetu sisi tulio wa mchana, acheni tutunze hisi zetu na kuwa tumevaa bamba la kifuani la imani na upendo na kama kofia ya chuma lile tumaini la wokovu; 9 kwa sababu Mungu alituhesabu sisi tuwe, si kwenye hasira ya kisasi, bali kwenye kujipatia wokovu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo. 10 Yeye alikufa kwa ajili yetu, ili, kama twakaa macho au tumelala usingizi, tuishi pamoja naye. 11 Kwa hiyo fulizeni kufarijiana na kujengana, kama vile kwa kweli mnavyofanya.
12 Sasa twawaomba nyinyi, akina ndugu, mwe na staha kwa wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu na kuwasimamia nyinyi katika Bwana na kuwaonya nyinyi kwa upole; 13 na mwape ufikirio ambao ni zaidi kuliko ule wa kawaida katika upendo kwa sababu ya kazi yao. Iweni wenye kufanya amani mtu na mwenzake. 14 Kwa upande mwingine, twawahimiza nyinyi kwa bidii, akina ndugu, waonyeni kwa upole wale wasio na utaratibu, semeni kwa kuliwaza nafsi zilizoshuka moyo, tegemezeni walio dhaifu, iweni wenye ustahimilivu kuelekea wote. 15 Angalieni kwamba mtu asilipe ubaya kwa ubaya kwa mwingine yeyote, bali sikuzote fuatieni lililo jema kuelekea mtu na mwenzake na kwa wengine wote.
16 Sikuzote iweni mkishangilia. 17 Salini bila kukoma. 18 Kuhusiana na kila jambo toeni shukrani. Kwa maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu katika muungano na Kristo Yesu kwa habari yenu nyinyi. 19 Msiuzime moto wa ile roho. 20 Msiyatendee kwa dharau yatolewayo unabii. 21 Hakikisheni mambo yote; shikeni sana lililo bora. 22 Jiepusheni na kila namna ya uovu.
23 Mungu yuleyule wa amani na awatakase nyinyi kikamili. Na vikiwa timamu katika kila jambo, roho na nafsi na mwili wenu akina ndugu vipate kuhifadhiwa kwa namna isiyo na lawama kwenye kuwapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye anayewaita nyinyi ni mwaminifu, naye atafanya hilo pia.
25 Akina ndugu, endeleeni katika sala kwa ajili yetu.
26 Salimuni ndugu wote kwa busu takatifu.
27 Nawaweka nyinyi chini ya wajibu mzito kwa Bwana ili barua hii isomwe kwa akina ndugu wote.
28 Fadhili isiyostahiliwa ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.